Rafiki yangu ni Wakala wa huduma za kifedha kwa mitandao ya simu ila katapeliwa kwa njia hii

Rafiki yangu ni Wakala wa huduma za kifedha kwa mitandao ya simu ila katapeliwa kwa njia hii

Mkogoti

TAPELI Mkubwa
Joined
May 3, 2020
Posts
2,415
Reaction score
3,924
Habari zenu wote humu ndani?

Kisa kipo hivi Rafiki angu anasimulia kwamba alikuja jamaa kibandani kwake akasema kwamba kuna mtu wake anataka kumtumia hela ila hana simu ila ana namba ya jamaa kichwani, na pia ni namba ya voda.

Rafiki angu huyo akamwambia chukua namba yangu hii ya Wakala (zile code zao za kuweka na kutoa) mtumie huyo ndugu yako na jina ninalotumia hapa ili atume hapo jamaa, "sawa"

Kawasiliana kupitia simu ya rafiki angu hiyo ya Uwakala karudisha kamwambia atatuma chap, mara mlio wa sms kwenye simu ya Rafiki yangu" umepokea laki moja na tisini, kaihakikisha kila kitu jina na namba na salio limeongezeka kweli, katoa hela kampa jamaa huyo kasepa,

Kimbembe kinakuja kesho kaweka kama laki moja hivi ya flot ila akashangaa imekatwa, kupiga makao makuu na kuwaelezea imekuwaje? Wanasema kwamba kuna mtu alituma hela kwenye namba yako ila ali cancel muamala kwenye menu ya M-pesa ndo tumeirudisha kwake baada ya masaa 24 rafiki aaah😳 ndo kawaelezea kila kitu jinsi ilivyokuwa ila mpaka leo Ni majibu yao ni subiri subiri tatizo tunashughulikia,

Na rafiki anakatwa mshahara kidogo kidogo na mwajili wake mwenye kibanda.

Swali!: Je, ata kwenye Code za wakala mtu anaweza tuma pesa harafu akaizuia huku wakala asijue wala kuletewa sms kwamba muamala umezuiwa kutoka namba flani ili kuepuka uhuni wa namna hii?
 
Asante kwa taarifa!

Ajifunze! siyo kila mtu ni wa kimuamini!

Voda hawawezi kumrudishia kizembe! Imeisha hiyoo!

Everyday is Saturday................................😎
 
Unapotuma pesa kwa code ya wakala maana yake ni kwamba pesa umeitoa, na si kwamba umetuma, hivyo huwezi kurudishiwa pesa amabyo umeshachukua cash physically, hiyo haiwezekani, waliofanya huo utapeli ni hao hao voda, otherwise hata mimi si naweza kwenda kwenye kibamda chochote, nikatoa hela napewa cash then nasepa na kucancel muamala, matapeli ni hao voda, akomae nao.
 
siku zote tafrani kama hiyo ikitokea kinachoangaliwa hapo ni location

jamaa alifanya kosa kumpa code mtu aliyeko mbali na ofisi yake atoe pesa, kwasababu huyo mtu akipiga simu kuisitisha hiyo pesa basi wahudumu kwa wateja ni rahisi kuizuia pasipo hata kufanya mawasiliano na wewe uliye pokea kwakua distance inaonesha huyo mteja hakua ofisin kwako probably ni mkoa tofauti na wako
 
Unapotuma pesa kwa code ya wakala maana yake ni kwamba pesa umeitoa, na si kwamba umetuma, hivyo huwezi kurudishiwa pesa amabyo umeshachukua cash physically, hiyo haiwezekani, waliofanya huo utapeli ni hao hao voda, otherwise hata mimi si naweza kwenda kwenye kibamda chochote, nikatoa hela napewa cash then nasepa na kucancel muamala, matapeli ni hao voda, akomae nao.
Wanaludishaga kwa mtoaji kutokana na distance ndio maana mawakala wanazuiliwa kufanya transaction za mbali
 
Voda hawana makosa huyo wakala ndio ana makosa

Voda wanaamini wateja wote unao wahudumia wapo hapo ofisini kwako na laini zako hivyo muamala kati ya wakala na mteja umefanyika katika mnara mmoja

Sasa kama mteja amepiga simu kuwa amekosea muamala na voda wakiangalia katika system wakaona mteja yupo Kawe na wakala yupo Mbagala hawana hata haja ya kumuuliza wakala wanamrudishia tu mteja pesa yake

Ilitakiwa ampe huyo tapeli namba yake ya kawaida itumiwe hiyo pesa alafu yeye atoe katika hiyo code yake ya uwakala ampe pesa yake kama aliamua kumsaidia
 
Wanaludishaga kwa mtoaji kutokana na distance ndio maana mawakala wanazuiliwa kufanya transaction za mbali
Transaction za mbali kivipi? Wakati pesa inaweza kutumwa kutoka eneo lolote. Mimi niko Dar, anayenitumia pesa yuko Mara labda, nikaomba code ya wakala aliyeko Dar. Hapo tatizo nn, mpk useme transaction za mbali?
 
Hivi ikitokea mteja akaja akasema atoe pesa ukamruhusu badala yake pesa ikatolewa kutoka mbali na ikaingia kwako na jamaa akakutajia jina na kiasi kilichoingia wewe kama mtoa huduma utafanyaje?

Maana kutoa hela akiwa mbali inawezekana kabisa bila hata wewe kukishirikisha,

Solution mitandao ya simu walete utambuzi wa location kwa watoa huduma ili kuepusha hili janga
 
Transaction za mbali kivipi? Wakati pesa inaweza kutumwa kutoka eneo lolote. Mimi niko Dar, anayenitumia pesa yuko Mara labda, nikaomba code ya wakala aliyeko Dar. Hapo tatizo nn, mpk useme transaction za mbali?
Mkuu wanasoma geolocation, kama miamala iko geolocation tofauti, mnara wa Dar mwingine mnara wa Tunduru, basi imekula kwa wakala.

Wakala anatakiwa kufanya muamala na mteja aliye naye kibandani siyo vinginevyo.

Na hii imekuwa hivyo ili kuzuia huo utapeli.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Voda hawana makosa huyo wakala ndio ana makosa

Voda wanaamini wateja wote unao wahudumia wapo hapo ofisini kwako na laini zako hivyo muamala kati ya wakala na mteja umefanyika katika mnara mmoja

Sasa kama mteja amepiga simu kuwa amekosea muamala na voda wakiangalia katika system wakaona mteja yupo Kawe na wakala yupo Mbagala hawana hata haja ya kumuuliza wakala wanamrudishia tu mteja pesa yake

Ilitakiwa ampe huyo tapeli namba yake ya kawaida itumiwe hiyo pesa alafu yeye atoe katika hiyo code yake ya uwakala ampe pesa yake kama aliamua kumsaidia
Hao Voda nao wapumbavu kama ni hivyo, nachojua system ya M-pesa wakati unatoa pesa mwishoni kuna mambo ya confirmation. Sasa mtu anawapigia wanarudisha pesa ni uzembe wanafanya.
 
Transaction za mbali kivipi? Wakati pesa inaweza kutumwa kutoka eneo lolote. Mimi niko Dar, anayenitumia pesa yuko Mara labda, nikaomba code ya wakala aliyeko Dar. Hapo tatizo nn, mpk useme transaction za mbali?
Wakala hatakiwi kuruhusu mtu aliye mbali na office yake kutoa pesa au yeye kumtumia pesa mtu aliyembali. Ukiruhusu mtu aliyembali kutoa pesa akitaka kuzuia muamala wanauzuia haraka na pesa inarudishwa kwake sababu mimi mwenyewe nilishawahi kukosea kutoa pesa kwa wakala nikawapigia voda wakuangalia location yang na wakala pesa ikarushwa haraka haikuchukua hata masaa 24
 
Transaction za mbali kivipi? Wakati pesa inaweza kutumwa kutoka eneo lolote. Mimi niko Dar, anayenitumia pesa yuko Mara labda, nikaomba code ya wakala aliyeko Dar. Hapo tatizo nn, mpk useme transaction za mbali?
Transactions za mbali zinazo ruhusiwa ni kati ya mteja na mteja sio mteja na wakala

Wakala anatakiwa amuhudumie mtu ambae yupo ofisini kwake na laini yake

Tatizo wabongo tunapenda short kati na matapeli wanajua huo udhaifu wa mawakala hivyo wanautumia kikamilifu
 
Back
Top Bottom