Wakala analindwa kuliko unavoandika hapa,,Mimi nina uzoefu ndo kazi yangu,,hela inapotelewa kimakosa voda wanapokwambia subiri masaa 72 ni kwamba wanafanya mawasiliano na wakala,,kwanza watapiga simu wakala usipopokea watakutumia sms kukuelekeza kuna muamala umeripotiwa kama kweli hujumuhudumia mteja kwa zamani ilikuwa wanarudisha wenyewe ila kwa sasa hivi Watakwambia wakala kama ni Mpesa upige menu ya mpesa utachagua namba sita MIAMALA ILIYOTOLEWA KIMAKOSA UTAINGIZA RISITI NAMBA utasibitisha hela itarudi na kama wakala utasema nilimuhudumia mteja hata kama hukumuhudumia kinachofata ni watamwambia mteja achukue hatua za kisheria aende polisi na Voda watatoa ushirikiano wa kuwapa location ulipo,,,mfano katika kazi yangu hii imeshanitokea mara kadhaa jamaa wanatoa kimakosa hata siwajui na napigiwa nawapa ushirikiano wanarudisha,,kuna siku kuna jamaa alitoa kiasi kama 260k akaondoka kesho yake nikakuta mised call ya huduma kwa wateja mara wakatuma sms nipokee simu kwa ajili ya kutoa ushirikiano wa muamala ulotolewa kimakosa,,walivopiga kupokea wakaniuliza na uzuri nilikuwa nakumbuka nikawaambia nimemuhudumia wakashukuru kwa ushirikiano na wakanambia watampigia na kumtumia sms ya Onyo.....
NIHITIMISHE kwa Kusema
Hakuna uwezekano wa mteja kurudishiaa fedha bila wakala kuthibitisha