Rage: Simba nendeni Kwa Eng. Hersi awafundishe kusajili

Rage: Simba nendeni Kwa Eng. Hersi awafundishe kusajili

RAGE: SIMBA NENDENI KWA ENGINEER AWAFUNDISHE KUSAJILI.

“Usajili wa dirisha dogo unakuja, wakae watafakari waangalie wachezaji wa kusajili. Nawasisitiza viongozi, waangalie sana umri wa wachezaji.”

“Yanga wamefanikiwa kwa sababu wachezaji wengi waliowasajili ni vijana wadogo na wale wenye umri mkubwa karibia wote wamewaacha.”

“Ukiona mwenzako kasajili vizuri, basi na wewe jitahidi usajili wachezaji wengine wazuri. Kuna wakati kulikuwa na tetesi Simba ingewasajili Adebayor na Manzoki lakini kwa sasa hawasikiki tena lakini kuna tetesi huenda wakasajiliwa wakati wa dirisha dogo.”

“Viongozi wetu wanapaswa kuwa waangalifu sana kwa sababu Adebayor na Manzoki hawachezi kwa sasa, unawezaje kujua viwango vyao? Wanapaswa kusajili wachezaji wanaocheza kwa sasa na wana umri mdogo.”

- Ismail Aden Rage, Mwenyekiti wa zamani Simba.

#FutbalPlanetUpdatesView attachment 2810347
Ndiyo huyu aliyewaita mbumbumbu wanachama na mashabiki wa simba?

Kama ni huyo aisee nashauri viongozi, wanachama na mashabiki wampuuze mpaka hapo atakapo omba msamaha kutokana na yale maneno yake makali.
 
IMG-20231105-WA0079.jpg
 
Mafanikio ya Yanga si wachezaji bora pekee bali pia kuna uongozi wa kisasa wenye akili uliojaa vijana, benchi bora la ufundi na mashabiki wenye mzuka na njaa ya mafanikio! Timu ikifunga bao nne tunaanza kuimba Bado moja Bado moja!!

Hivyo vyote hakuna Simba pale wapo viongozi wahuni, mashabiki mbumbumbu, Mo kanjibai na Dem wake Barbar alietimkia Yanga kimyakimya!
Barbra yupo Yanga?
 
Back
Top Bottom