Rage: Simba nendeni Kwa Eng. Hersi awafundishe kusajili

Rage: Simba nendeni Kwa Eng. Hersi awafundishe kusajili

Rage ndio mbumbu namba moja. Hivi Simba umekuwa sehemu ya kujifunza uongozi, swala la wachezaji wazee limepigiwa kelele muda mrefu sana
 
Ndiyo huyu aliyewaita mbumbumbu wanachama na mashabiki wa simba?

Kama ni huyo aisee nashauri viongozi, wanachama na mashabiki wampuuze mpaka hapo atakapo omba msamaha kutokana na yale maneno yake makali.
Aliwaita wanachama Ila alikuwa sahihi kwani hao ndio walimchagua Mangungu kwa kudanganywa kuletewa Manzoki.
Kuna kipindi Simba walimchagua mwenyekiti fundi cherehani akakaa wiki mbili wakamtoa.
 
RAGE: SIMBA NENDENI KWA ENGINEER AWAFUNDISHE KUSAJILI.

“Usajili wa dirisha dogo unakuja, wakae watafakari waangalie wachezaji wa kusajili. Nawasisitiza viongozi, waangalie sana umri wa wachezaji.”

“Yanga wamefanikiwa kwa sababu wachezaji wengi waliowasajili ni vijana wadogo na wale wenye umri mkubwa karibia wote wamewaacha.”

“Ukiona mwenzako kasajili vizuri, basi na wewe jitahidi usajili wachezaji wengine wazuri. Kuna wakati kulikuwa na tetesi Simba ingewasajili Adebayor na Manzoki lakini kwa sasa hawasikiki tena lakini kuna tetesi huenda wakasajiliwa wakati wa dirisha dogo.”

“Viongozi wetu wanapaswa kuwa waangalifu sana kwa sababu Adebayor na Manzoki hawachezi kwa sasa, unawezaje kujua viwango vyao? Wanapaswa kusajili wachezaji wanaocheza kwa sasa na wana umri mdogo.”

- Ismail Aden Rage, Mwenyekiti wa zamani Simba.

#FutbalPlanetUpdatesView attachment 2810347
Kwa msoamali mwenzake. Hivi Chadema wanaweza kwenda CCM kuomba msaada?
 
Back
Top Bottom