Raha na Vioja vya disko na mikusanyiko ya kidini shule za bweni(Boarding Schools)

wazee wa feedback sio mchezo umenikumbusha mbalii. enzi hizo old boys ilikuwa ni disco na machame girls weruweru au kibosho girls. Hata mabinti wakija kwenye debate patamalizwa na mziki. na hata uweke ndomboloo watu kucheza ni ZERO DISTANCE
 
Dah Mkuu umenifanya nivute hisia za mbali...Mimi hayo mambo ya disco niliyaanza O-Level iliyokuwa mixture. Siku zilizosubiriwa kwa hamu ilikuwa graduation ya TYCS, graduation ya shule na kali zaidi, CULTURAL DAY.Muziki unaanza saa 12:30 jioni baada ya cha jioni hadi 00:00 usiku,,,,kwenye uwanja wa assembly penye mwanga hafifu uliotoroka madarasani kupitia madirisha maana taa za nje zilizimwa(ona jinsi watu walivyo na roho mbaya).

Mkizidiwa mnamtoa mlinzi 1000-2000 anawachia funguo za store...kama ni zamu ya mlinzi mnoko basi barff likutie nguvu.
 
Hatukuwai kualika shule jiran ila jiran zetu walikua Machame dadaz na kwa mbali weruweru dadaz.

Disco tulikua tunachapa wenyewe tuu labda tualike wanakijiji tena ilikua ni inversely proportional boys 1000 girls 2

Nyimbo zilikua zinatawala hip hop Dj ukiweka bluz unatafuta ubaya watu mwanzo mwsho ni Tupac,Notorious big, snoopy dog dog,nas coba,kibongobongo kala pina pinna jabo watu wa Ar walikua hawampendi

Mwishoni kbsa watu wanachana free style dj anatoa biti kali unateleza tu

Kweli kila kipind na historia yake
 
Bila shaka hamtaki blues sbb mwajiona ni hard-Cores!!Ha ha ha ha ha ha
 
Bila shaka hamtaki blues sbb mwajiona ni hard-Cores!!Ha ha ha ha ha ha
Aisee ilikua zaidi za hardcores hakuna mambo za unyunyu/perfumes labda wachache sanaa...hahaha
 
Daah nakumbuka kuna siku tulikuwa na disco LA wanaume tupu. Jamaa moja kapinda aliingia uchi halafu akaapanda juu ya meza ukumbi mzima tunamwona halafu akaanza kupiga mapanga ya TMK. Mkuu wa shule kuja aliishia kucheka tu.
Daah tkm!
 
Daaah viongozi ndo walikuwa wanawawahi visichana ili wacheze nao halafu baadae wachuke contact

Sisi wengine tulikuwa maOBSERVER tu
 
Kumbe mambo hata hayabadiliki, vyote tumevifanya wakati wa simu na barua stamp 300 baasha 200 [emoji38]
 
Wapi hi? mungo au umbwe?
 
Daaaaah aiseeee kumbe matengo yalikuwepo tangu enzi za mwalimu aiseee....shukrani mkuu umenifurahisha sana...maana uliyoyasema hapo yote hayo niliyaona shuleni kwetu pia hahaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…