Mimi ngoja nikumbushie
matukio kama yupo mwenye kuyajua haya tutakuwa tumesoma shule moja:
1. Maharage yanaburuzwa kutoka stoo na kumiminwa kwenye sufuria zilizo jikoni tayari, yakipanda yakashuka sufuria linaepuliwa yameiva hayo!
2. Mzee saidi anasonga ugali huku jasho kama mvua kutoka kwenye madevu yake likichuruzikia kwenye sufuria, na mwiko ukizungushwa mara tano tu sufuria lishawekwa chini umeiva huo.
3. Una bifu na mwenye zamu ya kugawa msosi siku hiyo anakupiga ubao (slesi) ya ugali na maharage mawili na juice (mchuzi wa maharage)
4. Inagongwa kengere ya kuchukua msosi unakumbana na sahani tupu, ikiwa imekumbwa na wazee wa midabo!
5. Headmaster anasimama mlangoni kuchagua wa kuingia disko kama una bifu naye huoni ndani hata kama una kiingilio!
6. New comers wote kufikishiwa toilet kwa maana ndio nyumba ya wageni ………