Raha na Vioja vya disko na mikusanyiko ya kidini shule za bweni(Boarding Schools)

Raha na Vioja vya disko na mikusanyiko ya kidini shule za bweni(Boarding Schools)

Nakumbuka kipindi hicho nasoma Nganza girls tukaenda Nsumba boys disco kulikuwa na mwalimu anatusindikiza anaingia disco hakuna kumsogelea mwanaume sasa mi si nikaona mwalimu yupo busy kule katikati mi nikasogea kwa Dj nilipata kiboko cha Uti wa mgongo sitasahau.
Sasa kwanini Walimu wawachape?Raha ya disko kukumbatia na kukumbatiwa!!Duuuh mwalimu wenu alikuwa mkuda sana
 
Bila shaka hamtaki blues sbb mwajiona ni hard-Cores!!Ha ha ha ha ha ha
Jamaa sio kwamba walikua ni ma-hard cores, Bali walikuwa hawependi blues kwasababu walikua boys tuu.so mambo ya zero distance yalikuwa hayana nafasi zao ilikuwa ni Hiphop.
 
Mimi ngoja nikumbushie
matukio kama yupo mwenye kuyajua haya tutakuwa tumesoma shule moja:
1. Maharage yanaburuzwa kutoka stoo na kumiminwa kwenye sufuria zilizo jikoni tayari, yakipanda yakashuka sufuria linaepuliwa yameiva hayo!

2. Mzee saidi anasonga ugali huku jasho kama mvua kutoka kwenye madevu yake likichuruzikia kwenye sufuria, na mwiko ukizungushwa mara tano tu sufuria lishawekwa chini umeiva huo.

3. Una bifu na mwenye zamu ya kugawa msosi siku hiyo anakupiga ubao (slesi) ya ugali na maharage mawili na juice (mchuzi wa maharage)
4. Inagongwa kengere ya kuchukua msosi unakumbana na sahani tupu, ikiwa imekumbwa na wazee wa midabo!
5. Headmaster anasimama mlangoni kuchagua wa kuingia disko kama una bifu naye huoni ndani hata kama una kiingilio!
6. New comers wote kufikishiwa toilet kwa maana ndio nyumba ya wageni ………
 
Duuh hiyo shule balaa!!Mpaka HM ana beef na wanafunzi?
 
Watu mnazungumzi madisko ya nyimbo za West life za jana!!?Wakati watu tumecheza nyimbo za OSS (Orchestra Safari Sound) na Mangelepaa!!!
 
Inanikumbusha jamaa yangu ambaye tulikuwa bweni moja akijiita Mchungaji tena mwenye msimamamo mkali akiwasimamamisha wenzake has a wenye viçhwa viwili(nadhani naeleweka) lakini Siku ya Siku tukamkuta jamaaa anambato muumini mwenzake darasani umeme tanesco waliutaifisha Siku hiyo. Tulipo muuliza mbona Kazini nawe wawakataza wenzako kuyafanya haya akamnukuu nabii petrol kwamba kama huwezi kuvumilia basi Fanya (rejea biblia kwa andiko hilo) na kuweka msisitizo akauliza kwani nina utofauti gani na nyie. Maisha ya ujana raha sana
 
hahaha hakika nimekumbuka M bali sana pia kuna kitu iliitwa disco vumbi nomads
 
mimi ambaye bado nina alama za fimbo ngoja nisome replies zenu
 
Mkuu barafu mbona una viashiria vyote kuwa ulisoma shule yangu, ile shule iliyo na pacha mwenzake katika mkoa wa Prof. Lipumba, Mzee Sita na Prof. Kapuya?
 
Daah! Siwezi sahau enzi zile na UHIMA! walikua wananiboa, wanafuatilia maisha yako hadi chooni! Sijui nini kilinipelekaga? Nikaona miaka miwili mirefu.
Siku nikasimamishwaga shule.... Yaani nilionekana kama mdogo wake Lucifer!
 
Daah nakumbuka kuna siku tulikuwa na disco LA wanaume tupu. Jamaa moja kapinda aliingia uchi halafu akaapanda juu ya meza ukumbi mzima tunamwona halafu akaanza kupiga mapanga ya TMK. Mkuu wa shule kuja aliishia kucheka tu.
Yaani madisco ya peke yenu yanakuaga fun sana! Kukiwa na boys full ufeki
 
Back
Top Bottom