Raha na Vioja vya disko na mikusanyiko ya kidini shule za bweni(Boarding Schools)

Old is Gold Disko nimeanza ingia nipo shule ya msingi nyimbo zilizobamba ni za Awilo lolongomba,wenge bcbg na nk sekondari ndo ikawa zaidi kwenye kuhudhuria mambo ya TYCS hasa zile za kikanda ambazo mnaweka kambi na kukutana na shule mbalimbali hapo usipong'oa mwanamke we ni kilaza(baba jesca voice) huku tukinogesha na ile kauli mbiu ya "Mapendo" watu mnaitikia "Daima" huku taratibu viuno mmeviweka sawa kwa ajili ya kuyarudi
 
Me sikusoma zamani sana, hivyo shule yetu watu walikuwa na simu. Nakumbuka disco moja ile mida ya nyimbo za mwisho ndo muda wa kupeana namba za simu.. msichana mmoja akampa jamaa namba ya baba yake.. kilichofuatia.......
 
Kuna mambo yanaenda na umri tenda haki kwa umri wako ukijibana bana xana ukiwa shule/chuo ukimaliza chuo ndo unajiona sasa uko huru kufanya mambo yako kumbe unakuwa ndo umeshachelewa hayo ilitakiwa uwe umeyafanya huko ulipotoka huko n ukubwan kupambana na majukum ili kuwa mama au baba bora kwa wale waliomaliza michezo huwa na dspln
 
Dah.. Hii inanikumbusha sana EASTER CONFERENCE za TYCS tulikuwa tunafanyia Marangu Sec. YCS toka Sekondari schools za Moshi tunakutana pale.. Ushindani mkubwa ulikwa kwa Umbwe High school na giants wengine kama St. James Seminary, Old Moshi, Tarakea high school, Lyamungo na wenyeji wenyewe Marangu sec..
Sitasahau siku nlivochana pale RAP ya Yesu nliyoiita Son of God beat ya break yo neck by Busta Rhymes nkajipatia mtoto mmoja mkali sana kutoka Kiraeni Sec.
Plus nawakumbuka sana watoto wazuri wa Visitation na msala wa boksi la takataka kwenye Jenga YCS ile siku ya mwisho wa mkutano..
Old days are truly the Golden ones
 
Daaaah UKWATA walinitenga sana ikafika kipindi tunakaribia kupga pepa la six UKWATA ikabakiwa na viongozi tu km 6 ikabidi waanze kutuomba turudi kundini.
Ishu ilikuwa siku ya graduation full vituko yaani njemba zinabana pua kuimba kwaya na kata k kubwaaaah, daaah nikikumbuka those days raha saaana
 
Aisee mkubwa uzi wako umenikumbusha maisha ya Tanga Technical School aka Kiungani aka wazee wa Kwanjeka chini ya Disco la Mwl Kijazi,uzi umetulia sana aisee mkuu.....
 
Nakumbuka kipindi hicho nasoma Nganza girls tukaenda Nsumba boys disco kulikuwa na mwalimu anatusindikiza anaingia disco hakuna kumsogelea mwanaume sasa mi si nikaona mwalimu yupo busy kule katikati mi nikasogea kwa Dj nilipata kiboko cha Uti wa mgongo sitasahau.
 
Umenikumbusha mbali sana, wakati wa maulid ilikuwa kama fashion kuvaa khanga mbili, sasa wakati ule nilinunuliwa pair ya khanga mama alidhibiti ninapewa kipande kimoja kuendea shule mpaka term nyingine. Likizo hiyo niliweka ngumu kuwa lazima nipate pair ya khanga, niliulizwa unahitaji pair kwaajili gani? Nilijibu "baba wenzetu wakifa inabidi tuvae khanga kwenye msiba" mzee uso ulimbadilika lakini hakuhoji zaidi alininunulia tu pair ya khanga.
 
Nakumbuka enzi hizo nipo form six Iyunga tech siku ya mahafali yetu tuliwaalika madada zetu wa loleza girls bahati mbaya mnyamwezi sikuwa na pesa ya kuingilia disco basi nikaishia tu kuchungulia mlangoni kesho yake mshikaji wangu akaniambia kuna demu mmoja anakusalimia anaitwa fulani unamjua? nikamwambia ndio namjua tulisoma wote o level basi mshikaji akaniambia nimemtongoza na kakubali basi akaniuliza vp katulia?nikamjibu achana nae huyo demu ni kicheche.NISAMEHE DEVI KWA KUKULUSHIA NDEGE WAKO ZILIKUWA NI HASIRA TU ZA KUTOSWA NA HUYO DEMU O LEVER
 
Shikamoo barafu. Wewe Kama si class mate basi ni school mate. Pesa ilikuwa mwendo wa TMO , zikisomwa hadi karatasi ya mwisho bila jina lako unahsi kuzimia, simu ilikuwa mwendo wa riverse call ama radio kituo cha polisi, mzee umenichosha kwenye viwalo huku ukitishia mademu WA watu Kama una walk man Yuko na headphone basi huambiwi kitu - baadae ya jumamosi ya disco Ukwata mahubiri hutawaliwa na ama kondoo kuwa moto ama baridi Ili mradi wanoko wafikishe ujumbe. You made my day wallah
 
Bhuahahahahaha we jamaa ulitisha asee
 
Ha ha ha nakumbuka kuna Dada nilimkamatia mpaka MGOMBEA AKASIMAMAA, sa kumbe yule kilaza ni mjanjaa akawa anapitisha kidole kiaina hivi ili kuthibitisha kwamba kweli kanidatisha au... Toka hapo nikawa nikiingia disko lazima nimbane yule jamaa kwenye mkanda ili asijezua balaa tena
 
Mkuu umesahau segments ya tv.. baada ya disco kwenye huko ni changanyikeni.. kuna watu walikuwa wakikesha kuangalia tv tangu ijmaa jioni mpaka jumatatu usiku
 
Umenikumbusha sie shuleni disco ilikuwa kila mwisho wa mwezi na kiingilio sh.500 na tulikuwa mchanganyiko yani siku hiyo ilikuwa inasubiriwa kama dhahabu.Nakumbuka tulikuwa tunaita "DEBE"
 
Aiseeee nouma sana, ukiona vyaelea jua vimeundwa............. afu siku hiyo hata menu ni tofauti na katikati ya week........old good days!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…