Renegade
JF-Expert Member
- Mar 18, 2009
- 7,221
- 6,940
Raha nyingine ni pale kitanda kinapokuwa kiti. Matokeo had uipanga yenyewe.Unajua bwana kila kitu kina raha na karaha zake. Sasa kupanga na kuishi ndani ya chumba kimoja, kuna raha na karaha zake pia.
Kwa ufupi karaha zake ni kama pale itokeapo ukapata ugeni jinsia tofauti na wewe (siyo mpenzi wako) hapo lazima kichwa iwake
Tukirudi kunako raha za kupanga chumba kimoja, raha ni nyingi, ila raha na duraha iliyo kuu ni pale unapoamka asubuhi, YAANI VITU VYAKO VYOTE UNAVIONA.
Sent using Jamii Forums mobile app