Raha ya kupanga chumba kimoja

Raha ya kupanga chumba kimoja

Unajua bwana kila kitu kina raha na karaha zake. Sasa kupanga na kuishi ndani ya chumba kimoja, kuna raha na karaha zake pia.

Kwa ufupi karaha zake ni kama pale itokeapo ukapata ugeni jinsia tofauti na wewe (siyo mpenzi wako) hapo lazima kichwa iwake

Tukirudi kunako raha za kupanga chumba kimoja, raha ni nyingi, ila raha na duraha iliyo kuu ni pale unapoamka asubuhi, YAANI VITU VYAKO VYOTE UNAVIONA.
Raha nyingine ni pale kitanda kinapokuwa kiti. Matokeo had uipanga yenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona kuna walio oa wanaishi chumba kimoja na unaambiwa baba mkwe ni mgonjwa amepata rufaa kwenda Muhimbili kutokea Nanjilinji.

Anakuja yeye na mama mkwe na wanakaa miezi sita. Cha ajabu kabla hawajaondoka wanawauliza mna tatizo gani mbona hakuna dalili ya uzazi.
Jibu ni moja tu USITUKANE WAGUMBA NA UZAZI UNGALIPO

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunaishi hivyo wangu, tena tume up grade kila chumba kina huko la gesi na mtungi wake. Kwenye corridor labda kukaanga samaki tu kwani wana shombo. Shangaa wewe fire extinguishers hatuzijui lakini tunala na mabomu.

😀😀😀.... haya mkuu! ila raha ya chumba kimoja kinatakiwa kama chumba cha hotel... nionavyo mimi... raha ya chumba lazima kiwe na space na hewa ya kutosha, sio kachumba unajaza vitu kama store
 
😀😀😀.... haya mkuu! ila raha ya chumba kimoja kinatakiwa kama chumba cha hotel... nionavyo mimi... raha ya chumba lazima kiwe na space na hewa ya kutosha, sio kachumba unajaza vitu kama store
Karibu kwetu Kwamtogole uyaone. Kuna kitanda, seti ya makochi, kabati la nguo, coffee table ambayo pia ndiyo dining table. Pembeni kuna meza ina jiko la gesi chini ya meza ndoo ya unga na mchele na galoni ya mafuta ya kupikia.
 
Chumba Kimoja Noma, Hapohapo Sebule. Bedroom, Jiko, Sitting Room Na Stoo. Vitu Vimejaa Hakuna Nafasi Ya Kudeki
 
Back
Top Bottom