Unamtongoza mwanamke umekwisha kata tamaa huku umeangalia chini, ndiyomaana wanakuchukulia poa na kukupa majibu mepesi.
Je unamtongoza ili uzini naye muishane, au unamtongoza kumfanya awe hawara yako, au unamtongoza kutaka uchumba kuoa?
Maswali hayo, kila stage ina utongozaji wake.
Kutongoza mchepuko ama hawara: kama utakuwa na umri wa makamo kisha una kitambi, usisimamishe mwanamke njiani, utaonekana ni mzee hujatulia.
Mchague kisha tuma mtu akakuitie kisha mtongozee mahali patulivu umepumzika, lazima mtafikia muafaka mzuri tu.
Ukiona vipi, tumia kuwadi kama wanavyofanya waheshimiwa wakware, ili upate thamani halisi ya matumizi ya fedha zako.
Lakini kama kuoa, nyenyekea na usitangulize ukware wako.
Badilisha haiba yako, ongea naye kipole kwa maneno machache, kisha tumbukiza gia, usitume mtu wala usitongezewe.
Nenda mwenyewe hata kama ni domo zege,wewe nenda tu hivyohivyo maana ni maisha yako halisi hayo kajisemee.
Kwa kuwa ni jambo jema huwa halina utata sana, inategemea na mazingira, utakubaliwa tu.
Lakini sisi mahangaya, ninamtongoza mwanamke yeyote mwenye haiba yoyote popote pale.
Tena likija suala la kutongoza, hupandisha jazba kichwani bila kujua inapotokea.
Hiyo hasira hunisaidia kuniamria wa kuchukua ama wa kuacha.
Kwa kuwa jambo hilo hulichukulia kama ligi ya kutafuta mshindi, basi ninapenda wanawake wagumu, wenye maringo na majigambo ama wenye matusi, ili anikashifu ama anitukane mbele za watu, nipate sababu ya kuhangaika naye.
Nikiishalianzisha, huwa sirudi nyuma na popote tutafika tu, iwe kwa mjumbe hata mahakamani, kesi madai itaunguruma.
Atakapojutia matusi yake na kutaka issue tuimalize nje ya mahakama. Hapo hapo huwa ninamtamkia wazi njia gani itumike ili kumaliza kesi kabisa.
Njia hiyo ndiyo hupelekea kuanza mafungamano yasiyo na mwisho na mshindi mara zote huwa ni mimi.
Na kwa anayenijibu kipole na kwa heshima kuwa yupo kwenye mahusiano na mtu, huyaheshimu majibu yake na kuachana naye kistaarabu sana.
Sent using
Jamii Forums mobile app