Hii mada imenigusa sana, maana nilikuwa domo zege na vibuti nilikuwa nachezea vibaya mno.
Kuna mtu mmoja alifundisha vizuri sana, namna nzuri ya kuongea na wanawake, jaribu kutengeneza dialogue make her comfortable around you. First impressions matter, usilete topic/maswali yenye "Yes/No". Sio unafika tu, "Dada nimekupenda, naomba namba yako ya simu", akisema hana simu gearbox inakuwa imeingia kokoto.
Kuna manzi nilikuwa nasoma naye chuo, wakishua, halafu ana akili kinoma. Ana jamaa yake ana mpunga kweli kweli. Siku moja nikakutana nae mtaanai, nikamsalim then nikamwabia something simple, "Unajua kila nikikuona huwa najiuliza maswali mengi sana", alipotaka kujua ni maswali gani, nikamwambia "never mind".
Tukabadilishana namba, usiku alikuwa wa kwanza kunipigia (nilitengeneza the need to know, na binadamu hapendi kutojua), anataka ajue ni maswali gani hayo? bahati nzuri sana nilikuwa na safari, tukaongea/chat sana. Actually I was surprised, hakuwa na nyodo kama tulivyokuwa tunadhani; nilivyorudi nikwambia nimekuletea zawadi(uongo mtupu).Zawadi gani, nikamwabia siri yangu, njoo home uchukue, alivyokubali tu, mimi huyo Mwenge vinyago kuchukua zawadi kutoka "Arusha"
The rest is history....
Talk to her about anything without direct requests, mpaka atakapojisikia huru na wewe; Angalia mazingira, unawezaje kumfanya awe comfortable na wewe hapo mlipo?. Kuna demu mmoja nilimpataga kiulaini Mlimani City. Nimekutana nae Mr Price, nikamsalimia, nikajitambulisha [Respectfully]. Then nikamwomba msaada (Point to note: surprisingly wanawake wanapenda sana kutoa msaada), anisaidie kutafuta zawadi nzuri ya birthday ya dada yangu wakati sina dada wala birthday.
Nikawa nimeua ndege watatu kwa jiwe moja
1. Nimetengeneza dialogue without looking like an jerk.
2. Kwa kumuamini na kumpa kazi ya kutafuta zawadi, nimetengeneza trust between us; inaondoa natural defenses za mwanamke
3. Nimeonyesha kwamba I do care (kumtafutia zawadi sister yangu)
The rest is history....
Kuna actions wanawake wanazipenda naturally mfano taking care of children. Siku moja moja toka na vitoto vyako or vya any close relative, approach any lady, lazima moyo wake u-melt; anaanza kumuona baba wa watoto wake wakati wewe ni fisi tu. (Msije anza kuzungusha juani watoto wa ndugu zenu)
Kutongoza ni science. Wanaume tujue wanawake wanatongoza kila siku na kila mtu; how do you stand out? Nini kitamfanya asikusahau wewe? Jifunze, practise, utafanikiwa.