Rai kwa vyama vya upinzani Tanzania: Daini Tume Huru ya Uchaguzi kabla ya 2020!

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
98,439
Reaction score
145,410
Sabalkheri na masalkheri mabibi na mabwana popote pale mlipo kwenye pembe ya dunia hii.

Natumai nyote mna na mmekuwa na Jumapili njema kabisa kama ilivyo kwangu.

Baada ya salamu ngoja nizame sasa kwenye hoja ya mada husika.

Tayari kuna minong'ono ya hapa na pale iliyoanza kusikika kuhusu nani labda atagombea urais kupitia kile chama kikubwa cha upinzani au kupitia mwamvuli wa UKAWA.

Jambo ambalo linanishangaza ni ukimya wa vyama vya upinzani kuhusu chombo kinachoendesha na kusimamia chaguzi zetu, tume ya taifa ya uchaguzi.

Wengi tunajua jinsi ambavyo uongozi wa hicho chombo unavyoundwa. Na naamini tupo kadhaa ambao hatuna imani kivile na hicho chombo kutokana na ukweli kuwa huwa kinaundwa na rais aliyeko madarakani na ambaye mpaka sasa amekuwa ndiyo mwenyekiti wa chama tawala cha CCM.

Kwa mtaji huo, baadhi yetu huona dosari iliyopo katika muundo mzima wa hicho chombo. Binafsi naamini rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania/ mwenyekiti wa CCM huwa anaweka makada wa chama chake pale ili kulinda na kuhifadhi maslahi ya chama chake endapo ikibidi kufanya hivyo.

Tayari tumeshaona aliyekuwa makamu mwenyekiti wa tume hiyo hapo zamani, Jaji Agustino Ramadhani, alipotangaza nia ya kugombea urais kupitia CCM. Huyu mtu mimi naamini hata alipokuwa makamu mwenyekiti wa hiyo tume ya uchaguzi, pia alikuwa kada wa chama chake kwa wakati huo huo.

Sasa sijui hivi vyama vyetu vya upinzani vimejipangaje kuhusu hilo suala la tume ya uchaguzi. Tume ya uchaguzi inayoundwa na mtu mmoja, tena mtu mwenyewe ndiye mwenyekiti wa chama tawala na mgombea mtarajiwa wa urais kupitia chama chake, haiwezi kuwa huru hata kidogo.

Haiwezi kuwa huru kwa sababu ina wiwa [beholden] na shukurani kwake yeye huyo aliyeiunda.

Mimi ningependa kuona vyama vya upinzani vikisusia kabisa chaguzi kuu zote zijazo hadi hapo tutapokuja na njia ya kuunda chombo kilicho huru cha kuendesha na kusimamia chaguzi zetu.

Kinyume na hapo, wapinzani daima watakuwa wanainsindikiza CCM ikulu halafu baadaye watajifanya kuyasusia matokeo, kutokumtambua rais, na mwisho wao wenyewe kuachia msimamo wao na kumkubali rais aliyepo ikulu.

Sioni kabisa sababu ya kushiriki chaguzi ambazo zinasimamiwa na chombo kisicho huru. Kwa jinsi ilivyo sasa hivi, wapinzani kamwe hawatoiona ikulu. Hata uwingi wa wabunge watauona kwa CCM tu.

Tume ya taifa ya uchaguzi iliyopo sasa hivi haipo kwa ajili manufaa ya Watanzania wote. Ipo kwa ajili ya manufaa ya CCM. Hivyo ndivyo niaminivyo.

*Angalizo*

[Kuwa na tume huru ya uchaguzi haimaanishi moja kwa moja kuwa CCM itashindwa na wapinzani watashinda kwenye chaguzi kuu. Tunachotaka baadhi yetu ni kuwa na tume huru inayoaminika.]
 
Ni kwel kabisa ulichosema ila kususia uchaguzi itakuwa ni moja ya njia ya kujiua kisiasa, hii tume ya uchaguzi ni kweli inasimamishwa na mtu mmoja na ni ngumu sana wakamsaliti yule aliyewapa madaraka.

Nikirudi Tz nitaongea mengi sana (samaki mwenye maji mdomoni ana mengi ya kuongea)
 
Masakheri!

Hawawezi kususia uchaguzi ni sawa sawa kumuachia nguruwe akuchomee mishikaki.

Kingine hawa viongozi wa kudumu wa vyama vya upinzani wameishayazoea hayo maisha ya kuwa wapinzani wa kudumu.

Hata wakishindwa kwao uwa siyo tatizo wafuasi wao ndiyo wanaoumia.
 
Hili nalo neno, mgombea urais anapochagua wajumbe wa tume ya uchaguzi NEC, ila suala la kususia uchaguzi sioni mwafaka wake na faida yake.
 
Ni kwel kabisa ulichosema ila kususia uchaguzi itakuwa ni moja ya njia ya kujiua kisiasa, hii tume ya uchaguzi ni kweli inasimamishwa na mtu mmoja na ni ngumu sana wakamsaliti yule aliyewapa madaraka.

Nikirudi Tz nitaongea mengi sana (samaki mwenye maji mdomoni ana mengi ya kuongea)

Sidhani kama kususia itakuwa ni kujiua kisiasa.

Kwa sababu, kwa nini mtu ushiriki uchaguzi huku ukijua kuwa tume ya uchaguzi haiko huru, halafu ukishindwa ndo uanze kulalamika eti tume yenyewe haiko huru?

Kwa nini ushiriki uchaguzi ambao unajua unaendeshwa na tume isiyo huru?

Sioni kabisa sababu aisee.

Ukishaamua kushiriki kwenye uchaguzi unaoendeshwa na hiyo tume maana yake ni umeikubali hata tume yenyewe na hivyo kuja kulalamika kuwa haiko huru baada ya kushindwa unakuwa huna mamlaka ya kimaadili na unaonekana mzushi tu.
 
Kwa historia tume huru huletwa na maamuzi ya wengi!! Kwamba ikifika hatua watanganyika wakiamua sasa tunataka tume huru itakuja!!

Wasichokijua wengi ni kuwa kwa miaka mingi huku bara CCM hushinda kwa haki kabisa!! Nasema kwa haki kwa sababu watu wengi wa bara ni maamuma na wajinga wa kutupwa!! Huichagua CCM kwa ridhaa yao kabisa!!

Ni huku bara tu ndio CCM huwa na hofu sana na chaguzi tofauti na Zanzibar!! Nakuhakikishia kwa tume hii hii iliyopo watanganyika wakiamua sasa CCM baas itakua hivyo!!

Taratibu naona ngosha akiziangusha nguzo zilizokua mhimili wa ushindi wa CCM kule chini!! Taratibu akili zinawarudia wadanganyika....

Kule Kenya mzee moi na Jeuri yake yote alisalimu amri KANU iende na maji wakenya walipoamua!!!

So hatuhitaji tume huru kwanza, tunahitaji mbumbumbu wa Tanganyika watupe mishipi yao hapo CCM itaondoka na tume huru itakuja.
 
Sidhani kama kususia itakuwa ni kujiua kisiasa.

Kwa sababu, kwa nini mtu ushiriki uchaguzi huku ukijua kuwa tume ya uchaguzi haiko huru, halafu ukishindwa ndo uanze kulalamika eti tume yenyewe haiko huru?

Kwa nini ushiriki uchaguzi ambao unajua unaendeshwa na tume isiyo huru?

Sioni kabisa sababu aisee.

Ukishaamua kushiriki kwenye uchaguzi unaoendeshwa na hiyo tume maana yake ni umeikubali hata tume yenyewe na hivyo kuja kulalamika kuwa haiko huru baada ya kushindwa unakuwa huna mamlaka ya kimaadili na unaonekana mzushi tu.

Hahah ni sahihi kabisa yote unayosema ila ngoja nikupe msemo mmoja wa waswahili unasema kuwa "ukisusa sie twala".
 
Naunga mkono hoja. Wapinzani wetu wako bize na mambo mengine mpaka kampeni za uchaguzi wa mwaka 2020 zitakapo tangazwa.
Pasco

Saa ingine wanakuwa wanang'ang'ana na mambo ya ajabu ajabu tu halafu yale ya msingi wanayasahau.

Mwaka sasa umepita tokea tumalize uchaguzi mkuu na sijaona kampeni yoyote ile ya kutanabaisha umma kuhusu umuhimu wa tume huru ya uchaguzi.

Hebu ona kwa mfano yale mambo ya UKUTA uliobomoka. Watu waliwapandisha ari wenzao halafu wakaishia kuwaacha wakining'inia baada ya kutishiwa virungu na upupu.

Hii nchi bana...
 
Cha kushangaza hawa jamaa hawajawahi kuitisha maandamano au kususia bunge linapokuja suala la usimamizi wa uchaguzi...

Nikitafakari suala na tume huru ya uchaguzi na suala la wakurugenzi wa halmashauri kuwa wasimamizi wa uchaguzi, hadi huwa nahisi hivi vyama ni mawakala wa chama kile ila wanakuja kwetu kubalance equation Tu. In actual fact kwa muundo wa tume na usimamizi wa uchaguzi hawa jamaa wameshindwa kabla hata uchaguzi haujaitishwa
 
Nikirudi Tz nitaongea mengi sana (samaki mwenye maji mdomoni ana mengi ya kuongea)
Kwani ukirudi utaongelea wapi majukwaani au kwenye vipindi vya TV, kama ni humu humu JF kwani inashindikana nini kuongeza saa hizi.
 
Hawawezi kususia uchaguzi ni sawa sawa kumuachia nguruwe akuchomee mishikaki.

Kingine hawa viongozi wa kudumu wa vyama vya upinzani wameishayazoea hayo maisha ya kuwa wapinzani wa kudumu.

Hata wakishindwa kwao uwa siyo tatizo wafuasi wao ndiyo wanaoumia.

Ebana eeh umesema ukweli ulio mchungu mno.

Hapo kwenye viongozi wa kudumu umeua mbaya.

Na ni kweli, wanaoumiaga zaidi baada ya kushindwa ni wafuasi.

Too much truth!
 
Sabalkheri na masalkheri mabibi na mabwana popote pale mlipo kwenye pembe ya dunia hii.

Natumai nyote mna na mmekuwa na Jumapili njema kabisa kama ilivyo kwangu.

Baada ya salamu ngoja nizame sasa kwenye hoja ya mada husika.

Tayari kuna minong'ono ya hapa na pale iliyoanza kusikika kuhusu nani labda atagombea urais kupitia kile chama kikubwa cha upinzani au kupitia mwamvuli wa UKAWA.

Jambo ambalo linanishangaza ni ukimya wa vyama vya upinzani kuhusu chombo kinachoendesha na kusimamia chaguzi zetu, tume ya taifa ya uchaguzi.

Wengi tunajua jinsi ambavyo uongozi wa hicho chombo unavyoundwa. Na naamini tupo kadhaa ambao hatuna imani kivile na hicho chombo kutokana na ukweli kuwa huwa kinaundwa na rais aliyeko madarakani na ambaye mpaka sasa amekuwa ndiyo mwenyekiti wa chama tawala cha CCM.

Kwa mtaji huo, baadhi yetu huona dosari iliyopo katika muundo mzima wa hicho chombo. Binafsi naamini rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania/ mwenyekiti wa CCM huwa anaweka makada wa chama chake pale ili kulinda na kuhifadhi maslahi ya chama chake endapo ikibidi kufanya hivyo.

Tayari tumeshaona aliyekuwa makamu mwenyekiti wa tume hiyo hapo zamani, Jaji Agustino Ramadhani, alipotangaza nia ya kugombea urais kupitia CCM. Huyu mtu mimi naamini hata alipokuwa makamu mwenyekiti wa hiyo tume ya uchaguzi, pia alikuwa kada wa chama chake kwa wakati huo huo.

Sasa sijui hivi vyama vyetu vya upinzani vimejipangaje kuhusu hilo suala la tume ya uchaguzi. Tume ya uchaguzi inayoundwa na mtu mmoja, tena mtu mwenyewe ndiye mwenyekiti wa chama tawala na mgombea mtarajiwa wa urais kupitia chama chake, haiwezi kuwa huru hata kidogo.

Haiwezi kuwa huru kwa sababu ina wiwa [beholden] na shukurani kwake yeye huyo aliyeiunda.

Mimi ningependa kuona vyama vya upinzani vikisusia kabisa chaguzi kuu zote zijazo hadi hapo tutapokuja na njia ya kuunda chombo kilicho huru cha kuendesha na kusimamia chaguzi zetu.

Kinyume na hapo, wapinzani daima watakuwa wanainsindikiza CCM ikulu halafu baadaye watajifanya kuyasusia matokeo, kutokumtambua rais, na mwisho wao wenyewe kuachia msimamo wao na kumkubali rais aliyepo ikulu.

Sioni kabisa sababu ya kushiriki chaguzi ambazo zinasimamiwa na chombo kisicho huru. Kwa jinsi ilivyo sasa hivi, wapinzani kamwe hawatoiona ikulu. Hata uwingi wa wabunge watauona kwa CCM tu.

Tume ya taifa ya uchaguzi iliyopo sasa hivi haipo kwa ajili manufaa ya Watanzania wote. Ipo kwa ajili ya manufaa ya CCM. Hivyo ndivyo niaminivyo.
Ndugu yangu Nyani Ngabu kwa akili yako kuna Chama gani cha kukikabidhi Nchi hii zaidi ya CCM? Hatuwezi kuiweka Nchi hii rehani kwa kuwapa watu walioachwa na CCM kwa rekodi mbaya ya ama utendaji au Ufisadi!
 
Suala la kudai tume huru ya uchaguzi limekuwa kama wimbo wa taifa .wapinzani wameimba mpaka wamekata tamaa CCM hawataki. Hakuna namna mimi nashauri wasisue uchaguzi.kususia uchaguzi ndio kujimaliza kabisa. Waendelee tu kushiriki mbona CCM yenyewe imeshaelekea qibla.kila mwaka wafuasi wanaisapoti ccm wanapungua. Naamini 2020 racing itakuwa very tight.
 
Cha kushangaza hawa jamaa hawajawahi kuitisha maandamano au kususia bunge linapokuja suala la usimamizi wa uchaguzi...

Nikitafakari suala na tume huru ya uchaguzi na suala la wakurugenzi wa halmashauri kuwa wasimamizi wa uchaguzi, hadi huwa nahisi hivi vyama ni mawakala wa chama kile ila wanakuja kwetu kubalance equation Tu. In actual fact kwa muundo wa tume na usimamizi wa uchaguzi hawa jamaa wameshindwa kabla hata uchaguzi haujaitishwa
Hivi jamani nyie mnasikilizaga vyombo gani vya habari? Upinzani hawa kila siku wanalalamikia haya mambo hamsikii.hakuna kususia uchaguzi CCM itajimaliza yenyewe hasa awamu hii tunayoenda nayo.
 
Ndugu yangu Nyani Ngabu kwa akili yako kuna Chama gani cha kukikabidhi Nchi hii zaidi ya CCM? Hatuwezi kuiweka Nchi hii rehani kwa kuwapa watu walioachwa na CCM kwa rekodi mbaya ya ama utendaji au Ufisadi!

Hapo ndipo CHADEMA ilipo bugi step.

Haina tena credibility wala moral authority ya kuikemea CCM.

Ufisadi ndo ulikuwa ni centerpiece ya ajenda ya CHADEMA.

Lakini ndo hivyo tena...baada ya gia kubadilishwa angani na tables nazo zikawa turned.

CHADEMA badala ya kuwa kwenye offensive wakawa defensive na CCM ndo wakawa kwenye offensive.
 
Sabalkheri na masalkheri mabibi na mabwana popote pale mlipo kwenye pembe ya dunia hii.

Natumai nyote mna na mmekuwa na Jumapili njema kabisa kama ilivyo kwangu.

Baada ya salamu ngoja nizame sasa kwenye hoja ya mada husika.

Tayari kuna minong'ono ya hapa na pale iliyoanza kusikika kuhusu nani labda atagombea urais kupitia kile chama kikubwa cha upinzani au kupitia mwamvuli wa UKAWA.

Jambo ambalo linanishangaza ni ukimya wa vyama vya upinzani kuhusu chombo kinachoendesha na kusimamia chaguzi zetu, tume ya taifa ya uchaguzi.

Wengi tunajua jinsi ambavyo uongozi wa hicho chombo unavyoundwa. Na naamini tupo kadhaa ambao hatuna imani kivile na hicho chombo kutokana na ukweli kuwa huwa kinaundwa na rais aliyeko madarakani na ambaye mpaka sasa amekuwa ndiyo mwenyekiti wa chama tawala cha CCM.

Kwa mtaji huo, baadhi yetu huona dosari iliyopo katika muundo mzima wa hicho chombo. Binafsi naamini rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania/ mwenyekiti wa CCM huwa anaweka makada wa chama chake pale ili kulinda na kuhifadhi maslahi ya chama chake endapo ikibidi kufanya hivyo.

Tayari tumeshaona aliyekuwa makamu mwenyekiti wa tume hiyo hapo zamani, Jaji Agustino Ramadhani, alipotangaza nia ya kugombea urais kupitia CCM. Huyu mtu mimi naamini hata alipokuwa makamu mwenyekiti wa hiyo tume ya uchaguzi, pia alikuwa kada wa chama chake kwa wakati huo huo.

Sasa sijui hivi vyama vyetu vya upinzani vimejipangaje kuhusu hilo suala la tume ya uchaguzi. Tume ya uchaguzi inayoundwa na mtu mmoja, tena mtu mwenyewe ndiye mwenyekiti wa chama tawala na mgombea mtarajiwa wa urais kupitia chama chake, haiwezi kuwa huru hata kidogo.

Haiwezi kuwa huru kwa sababu ina wiwa [beholden] na shukurani kwake yeye huyo aliyeiunda.

Mimi ningependa kuona vyama vya upinzani vikisusia kabisa chaguzi kuu zote zijazo hadi hapo tutapokuja na njia ya kuunda chombo kilicho huru cha kuendesha na kusimamia chaguzi zetu.

Kinyume na hapo, wapinzani daima watakuwa wanainsindikiza CCM ikulu halafu baadaye watajifanya kuyasusia matokeo, kutokumtambua rais, na mwisho wao wenyewe kuachia msimamo wao na kumkubali rais aliyepo ikulu.

Sioni kabisa sababu ya kushiriki chaguzi ambazo zinasimamiwa na chombo kisicho huru. Kwa jinsi ilivyo sasa hivi, wapinzani kamwe hawatoiona ikulu. Hata uwingi wa wabunge watauona kwa CCM tu.

Tume ya taifa ya uchaguzi iliyopo sasa hivi haipo kwa ajili manufaa ya Watanzania wote. Ipo kwa ajili ya manufaa ya CCM. Hivyo ndivyo niaminivyo.

*Angalizo*

[Kuwa na tume huru ya uchaguzi haimaanishi moja kwa moja kuwa CCM itashindwa na wapinzani watashinda kwenye chaguzi kuu. Tunachotaka baadhi yetu ni kuwa na tume huru inayoaminika.]
Tume huru haiwezi kuja kwa katiba hii iliyopo kwanza nishauri wapinzani wapiganie katiba mpya yenye tume huru ndani yake..

Bila hivyo ni mpuuzi pekee atakayekwenda kujipanga kwenye mstari kupigia kura upinzani mwaka 2020
 
Wanashiriki chaguzi, wanaimba, wanazungusha mikono, halafu wakija kushindwa eti wanaanza kulalamika 'ooh tume ya uchaguzi si huru'.

Hivi huwa wanazinduka baada ya kushindwa kuwa tume haiko huru?

Mimi siwezi kushiriki jambo ambalo sina imani na mwendeshaji wake.
 
Unachosema uko sahihi ila tusifike kususia uchaguzi maana hawa jamaa malengo yao ni kuua upinzani kama nguvu kubwa inayotumika kwa sasa kumtimia Propesa pumba n.k.
La msingi upinzani by hook crook ni kutafuta namna ya kupata tume huru ya uchaguzi maoena sana japo vikwazo vingi sana kutokana na woga wa ccm
 
..kususia uchaguzi ni sawa na kumuachia mkeo mgoni wako.

..Tanzania hatuna wapinzani,,,,,,nani Lowassa?Sumaye?Kingunge?mmh

...Kushinda kwa CCM kunachangiwa na "Ujinga" wetu pamoja tume isiyo huru,na pia wapinzani waliokosa misimamo................................
 
Back
Top Bottom