Rai kwa vyama vya upinzani Tanzania: Daini Tume Huru ya Uchaguzi kabla ya 2020!

Rai kwa vyama vya upinzani Tanzania: Daini Tume Huru ya Uchaguzi kabla ya 2020!

Naunga mkono hoja. Wapinzani wetu wako bize na mambo mengine mpaka kampeni za uchaguzi wa mwaka 2020 zitakapo tangazwa.
Pasco
Kwamba unsuccessfully fsnya hujui? Kwani watu kama Lipumba wanaibuliwa kwaalengo gani?

Lengo ni moja tu kuwahamisha wapinzani kwenye hoja za msingi na watumie muda mwingi kupambana na maadui wa ndani kwanza.

Na nyinyi wazee wa bahasha mkishashikishwa bahasha zenu mnageuka popo.

Sasa hivi sidhani kama mkesha wa mwaka mpya kama tutaenda pamoja kuchoma nyama Monduli.
 
Mkuu Matola, nakubaliana na wewe big money changes hands during elections na mimi nakiri my first 6 figure niliishia for the first time ile 1995, ila issue sio kuwa popo bali it's very hard to stand on the fence hivyo objectivity na impartiality vinakuwa compromised.

Kwa upande wangu sijawahi kuwa na chama chochote mimi kama mimi ila kampuni yangu inafanya kazi ya chama chochote kama alivyo dereva taxi.

Huwezi amini nikikuambia sijawahi kufika Monduli!, ila best wangu ndio right-hand man wake, mimi ananijua tuu kama Mkapa, Kikwete na Magufuli wanavyonijua, na naendelea kusimama on the fence.
Pasco
 
ACT wazalendo wameanza kazi hii kwa kutaka kufufuliwa kwa mchakato wa katiba mpya...ambayo ina kipengele cha tume huru ya uchaguzi.

Kwa kuwa chama chenyewe ni kidogo basi hata hoja zao hazina nguvu.
Shida upinzani wanaungana mambo yasiyo kichwa ila ya maaana Kama hilo hawataki
 
Kwa akili za viongozi wa chadema ikifika 2019 ndio wataanza kudai

wakati huo CCM itakua ishapanga safu yao ya ushindi kwenye tume hawawezi kubadili au kuunda hio tume huru

Huu ndio muda sahihi wa UKAWA kupigania tume huru badala ya huo ujinga wa UKUTA
 
Upo sahihi, ila kwenye nchi changa kama Tz ambayo elimu ya uraia, demokrasia na uzalendo vipo chini ya asilimia zero nadhani hilo tusubiri kwanza kwa sababu:
1. Tz kuna mtu/kikundi kinaweza kununua chama fulani cha upinzani
2. Tz kuna watu/chama/kikundi kinaweza kuwanunulia watu viroba na kuwaambia wadeki barabara
3. Tz kuna mtu mwenye hela anaweza kununua ajenda za wapinzani kwa bil 10 na kuwabadilisha ajenda yao

Hapana, hoja ya nchi kuwa changa na kwa sababu hiyo tusubri siikubali.

Upuuzi hauna cha uchanga na hauna haja ya kusubiri ili kuondokana nao.
 
Haya wasisusie...ila ndo hivo daima wataendelea kuwa wasindikizaji wa CCM huko ikulu na bungeni.
Mkuu halafu kitu kimoja ambacho wanasiasa wetu, hata wa CCM wanajitoa ufahamu! Tume huru ya uchaguzi si kwa manufaa ya wapinzani tu ni kwa afya ya Taifa letu. Hivi Lowassa alipokuwa CCM tena akiwa waziri mkuu angepigania tume huru ya uchaguzi (katiba mpya) ungekuta analilia lia sasa? Sumaye? Kingunge je? Na wengine wengi waliotoka CCM je? Nadhani wanasiasa wetu wanaangamizwa kwa ubinafsi. Lakini kwa hakika kama mchangiaji mmoja alivyosema hapo juu: upinzani unaposhindwa, wanaoathirika ni sisi raia wa kawaida (wapinzani + wana CCM). Mbowe hapotezi chochote kwani ubunge unamtosha.
 
..kususia uchaguzi ni sawa na kumuachia mkeo mgoni wako.

..Tanzania hatuna wapinzani,,,,,,nani Lowassa?Sumaye?Kingunge?mmh

...Kushinda kwa CCM kunachangiwa na "Ujinga" wetu pamoja tume isiyo huru,na pia wapinzani waliokosa misimamo................................
Ukweli mchungu, UJINGA WA MTANZANIA NDIO NGAO YA CCM na UPINZANI USIOJIELEWA!
 
Upo sahihi, ila kwenye nchi changa kama Tz ambayo elimu ya uraia, demokrasia na uzalendo vipo chini ya asilimia zero nadhani hilo tusubiri kwanza kwa sababu:
1. Tz kuna mtu/kikundi kinaweza kununua chama fulani cha upinzani
2. Tz kuna watu/chama/kikundi kinaweza kuwanunulia watu viroba na kuwaambia wadeki barabara
3. Tz kuna mtu mwenye hela anaweza kununua ajenda za wapinzani kwa bil 10 na kuwabadilisha ajenda yao
CCM inatumia ngao ya "UJINGA" kutawala nchi hii. Upinzani nao unaongoza bila mwelekeo kabisa, ndio maana wengi wa wanaojielewa hawaoni umuhimu wa hao wapinzani. Wengi hawana hata uwezo wa kupambana na ccm hata kidogo.
 
Ni vigumu mabadiliko ya katiba au hata ya tume ya uchaguzi yaanzishwe na upinzani kwa sababu kimsingi hiyo siyo agenda yao kuu. Ikumbukwe kuwa siasa za nchi hii hazichagizwi na mapambano ya kitabaka na kwa hivyo hazina misingi ya kiitikadi. At individual level, wanasiasa, wawe wa upinzani au wa CCM, wanapogombea nafasi za kuchaguliwa lao ni moja tu: kuendeleza maslahi binafsi na kusaka fursa za kiuchumi. Kwa vile uwezekano wa kushinda uchaguzi wa ubunge na udiwani upo kwa wapinzani; na kwa vile kura za urais zitawaongezea ruzuku hata kama uwezekano wa kushinda hiyo nafasi haupo; kwa kupitia tume iliyopo, kamwe hawatasusia uchaguzi. Hivyo, kwao suala la kudai tume huru ya uchaguzi halina umuhimu mkubwa.
 
Sio lazima kubadili katiba, ni kupigania mabadiliko ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwepo kwa Tume huru yenye wajumbe wenye divedified compositions.

Wanatakiwa kupigania the level playing field,
Wenzetu Bunge likiishavunjwa mali zote za umma zinarudishwa na wagombea wote wanakiwa na equal status. Huku kwetu magari yanabadilishwa tuu number na kuwekwa za kiraia, rais anaendelea kugombea na presidential status, 2015 timu yote ya Ikulu including the press unit ilikuwa nyuma ya Magufuli na fedha za kampeni ni fedha za serikali! .

Mnagombea kisu cha makali kuwili, mwenzako ameshika mpini wewe unapewa kushika kwenye makali ukitegemea kushinda! .

Ni kweli Pasco.
Playing ground iliyokuwa sawa ni jambo ambalo limezungumzwa sana.
Watawala wanajua faida ya kuwa na uwanja usiokuwa sawa na wapinzani wanajua hasara yake.ila wananchi inaelekea hawajui faida wala hasara ya kuwa na uwanja usio sawa.
mambo yatabadilika wakati wananchi watakapogundua.
 
Naunga mkono hoja. Wapinzani wetu wako bize na mambo mengine mpaka kampeni za uchaguzi wa mwaka 2020 zitakapo tangazwa.
Pasco
hivi kwa akili zenu ccm watakubali kuleta tume huru ya uchaguzi hizo ni ndoto labda kwa vurugu watu wauliwe ndio wanaweza kufahamu
 
Kutoshiriki uchaguzi ni suicide kwa vyama vya upinzan. Huna wabunge, maana yake huna ruzuku. Utaendesha vipi chama? Tume huru ya uchaguzi itapatikana wananchi wakiamua na kuchoshwa kuibiwa kura. Seif kule kasusa na watu wanakulaga tu.
 
Kwa hiyo wapinzani waendelee tu kushiriki chaguzi zinazoendeshwa na tume ya uchaguzi inayoteuliwa na mwenyekiti wa CCM?
 
Back
Top Bottom