Kila mwaka wa uchaguzi mnashiriki chaguzi za kutafuta viongozi wa ngazi mbalimbali nchini.
Chaguzi mnazoshiriki huendeshwa na kuratibiwa na tume ya taifa ya uchaguzi.
Huku mkiwa mnajua kabisa jinsi ambavyo hiyo tume huundwa, huwa mnashiriki na si ajabu kujipa matumaini hewa kuwa mwaweza kushinda, hususan nafasi ya urais.
Kwa jinsi ilivyo sasa mtaendelea kuishia kujipa matumaini hewa tu kwa sababu mshindi wa hiyo nafasi ya urais ni 'a foregone conclusion'.
Kama ilivyo ada, matokeo yakishatangazwa huwa mnayakataa na kuanza kudai kuwa tume haipo huru.
Kama mnaona tume haipo huru [jambo ambalo nakubaliana nalo], kwa nini huwa mnaamua kushiriki chaguzi zinazoendeshwa na hiyo tume?
Leo Raila Odinga na muungano wao wa NASA wameamua kujitoa ushiriki wao kwenye marudio ya uchaguzi uliokuwa umepangwa kufanyika baadaye mwezi huu kwa sababu hawajaridhishwa na utendaji wa hiyo tume.
Muda umefika sasa na nyie muache kushiriki chaguzi ziendeshwazo na tume ambayo hamna imani nayo. La sivyo, mtaendelea kuwa wasindikizaji wa CCM ikulu maana msitegemee tume ya uchaguzi iliyoundwa na mwenyekiti wa CCM ije kuwatangaza washindi.
Fuateni nyayo za Raila hata kama mnampenda Uhuru.
Ni kwa sababu hawana
influence yoyote ile nje na ndani ya Tanzania, hata wakisusia CCM watafanya uchaguzi,
kuapisha Raisi na maisha kuendelea, lkn Kenya ni tofauti Raila Odinga ana
wafuasi milioni 10 ambao wanamsikiliza na kutii chochote asemacho, ni Mfalme kwa kifupi, hivyo ana uwezo mkubwa wa kushinikiza chochote, lkn Upinzani wa Tanzania, kwa mfano chadema Tanzania nzima wana
Wabunge 30 tu, sasa watamshinikiza nani?
Mfano mdogo tu Tundu Lisu kashambuliwa lkn hakuna hata
Mwanasingida ukiondoa Nyarandu, labda Wema Sepetu na Mama yake kidogo aliyekosa usingizi kwa maana ya kwamba kujitokeza kutaka kumtetea kwa njia yoyote ile, lkn Kenya Raisi Uhuru Kenya alivyomshambulia JM Maraga huko anakotoka sijui Kisi palisimama kwamba mtu wao kashambuliwa na hivyo Uhuru Kenya ilibidi aende kujielezea, hivyo Kenya na Tanzania ni mazingira mawili tofauti, hakuna Mtanzania utakaye mwambia asitii Dola aingie barabarani kwa ajili ya
Mbowe, hata Wachaga wenyewe KLM hawatomtii ije kuwa TZ nzima?
Hivyo ni ngumu maadamu Tanzania hakuna Siasa za Kikabila au Kidini ni ngumu kushawishi kukubali kuumia kwa ajili ya Mwanasiasa, hiyo ndiyo tofauti na Kenya, kwani Raila Odinga ni Mfalme wa
Wajaluo, ...