Rai kwa vyama vya upinzani Tanzania: Daini Tume Huru ya Uchaguzi kabla ya 2020!

Sasa badala ya kujadili hoja wewe unaanza kunishambulia mimi.

Typical kamanda behavior[emoji23] [emoji23] [emoji23]
Wapinzani wanafahamu fika kwamba kwao kushika dola ni ndoto na kama ni halisia basi siyo karne hii.

Wao huingia kwenye chaguzi kwa lengo la kuongeza wabunge ili wapate ruzuku lakini huwapotosha vipofu wao kwamba ikulu ni saa nne asubuhi.
Natamani 2020 ifike ili nione Mbowe atawaagiza kuzungusha nini.
 
upinzani wa tz ni mgumu sana, kuanzia mapungufu ya katiba mpaka watu wenyewe wakenya wapo commited sana na sio waoga na wanafiki kama hapa tz. odinga leo kutangaza kujitoa kwenye uchaguzi subiri uone reaction yake kuanzia kwa wakenya mpaka kwenye mifumo ya kikatiba, na hiyo ninawasiwasi ni janja ya odinga either kuepuka 6th straight defeat au kutaka fresh call up for election ili ajipange.
 
Odinga ana hoja nzuri tu hapa.

Hao IEBC walivuruga uchaguzi wa awali. Halafu hao hao tena ndo wasimamie marudio ya huo uchaguzi katika mazingira yaleyale?

Hahahaaa.
 
Hahahaaa.

Wewe, huijui dhamira yangu. Hivyo acha kuandika kama vile unaijua.

Mambo ya wapinzani kususia chaguzi zinazoendeshwa na NEC sijaanza kuyazungumzia leo.

Nimeanza kuyazungumzia tokea 2005 kule bcstimes.com, jamboforums.com, na mpaka leo hii JF.

Nimeshawakejeli CCM na nimeshawakejeli vyama vya upinzani.

Acha kuandika usivyovijua.

Dhamira yangu huna uwezo wa kuijua.
Hawa makamanda tuko nao huku mitaani. Wanachotamani ni zamu yao tu hamna jipya.
 
Odinga ana hoja nzuri tu hapa.

Hao IEBC walivuruga uchaguzi wa awali. Halafu hao hao tena ndo wasimamie marudio ya huo uchaguzi katika mazingira yaleyale?

Hahahaaa.
Kabla ya uchaguzi uliomchagua Magu kuna makamanda huwa naongea nao niliwaambia uchaguzi huu ukiisha mtasema mmeibiwa! Jamaa akasema oh sasa hivi yule mtaalam wa hayo mambo tunae hawana uwezo wa kutuibia. Uchaguzi ulivyoisha kilio kile kile.
 
Kila mwaka wa uchaguzi mnashiriki chaguzi za kutafuta viongozi wa ngazi mbalimbali nchini.

Chaguzi mnazoshiriki huendeshwa na kuratibiwa na tume ya taifa ya uchaguzi.

Huku mkiwa mnajua kabisa jinsi ambavyo hiyo tume huundwa, huwa mnashiriki na si ajabu kujipa matumaini hewa kuwa mwaweza kushinda, hususan nafasi ya urais.

Kwa jinsi ilivyo sasa mtaendelea kuishia kujipa matumaini hewa tu kwa sababu mshindi wa hiyo nafasi ya urais ni 'a foregone conclusion'.

Kama ilivyo ada, matokeo yakishatangazwa huwa mnayakataa na kuanza kudai kuwa tume haipo huru.

Kama mnaona tume haipo huru [jambo ambalo nakubaliana nalo], kwa nini huwa mnaamua kushiriki chaguzi zinazoendeshwa na hiyo tume?

Leo Raila Odinga na muungano wao wa NASA wameamua kujitoa ushiriki wao kwenye marudio ya uchaguzi uliokuwa umepangwa kufanyika baadaye mwezi huu kwa sababu hawajaridhishwa na utendaji wa hiyo tume.

Muda umefika sasa na nyie muache kushiriki chaguzi ziendeshwazo na tume ambayo hamna imani nayo. La sivyo, mtaendelea kuwa wasindikizaji wa CCM ikulu maana msitegemee tume ya uchaguzi iliyoundwa na mwenyekiti wa CCM ije kuwatangaza washindi.

Fuateni nyayo za Raila hata kama mnampenda Uhuru.

Watu wengi hamjajua kwanini raila kafanya alichokifanya na hamjuhi hata katiba yao inasemaje pale mgombea anapojitoa.

Kifupi tu:-
1. Mgombea akijitoa huko kenya uchaguzi unasimmishwa na tume inatangaza upya wagombea.
2. raila alikuwa anamadai anataka yatekelezwe na Uhuru nadhani walikuwa wansingizia muda hautoshi na haupo.
3. So kitendo cha kujitoa ni msg kwa tume na serekali kuwa jipangeni sasa mfanye marekebisho na uchaguzi uitishwe upya.

All in all anacholingia Raila ni Katiba mpya ya kenya ambayo hakika imetoa uhuru mkubwa sana wa kidemokrasia kwa wapinzani. na nachofanya raila ni kuabuse huo uhuru, na hapa usifikiri NASA watakaa kimya kw avyovyote wana majority Bungeni so vipengele kama hivi hakika wataenda kuvibadilisha vyote, maana kwa sasa vinatumika vibaya.
 
Unawashauri watu gani hasa!
Tanzania hakuna upinzani kamwe
Tanzania ina Vibendera na wasaka Tonge tu.
Waache watanzania wapige kazi
muda wakuwajadili hawa wapuuzi haupo
 
Ni kwa sababu hawana influence yoyote ile nje na ndani ya Tanzania, hata wakisusia CCM watafanya uchaguzi, kuapisha Raisi na maisha kuendelea, lkn Kenya ni tofauti Raila Odinga ana wafuasi milioni 10 ambao wanamsikiliza na kutii chochote asemacho, ni Mfalme kwa kifupi, hivyo ana uwezo mkubwa wa kushinikiza chochote, lkn Upinzani wa Tanzania, kwa mfano chadema Tanzania nzima wana Wabunge 30 tu, sasa watamshinikiza nani?

Mfano mdogo tu Tundu Lisu kashambuliwa lkn hakuna hata Mwanasingida ukiondoa Nyarandu, labda Wema Sepetu na Mama yake kidogo aliyekosa usingizi kwa maana ya kwamba kujitokeza kutaka kumtetea kwa njia yoyote ile, lkn Kenya Raisi Uhuru Kenya alivyomshambulia JM Maraga huko anakotoka sijui Kisi palisimama kwamba mtu wao kashambuliwa na hivyo Uhuru Kenya ilibidi aende kujielezea, hivyo Kenya na Tanzania ni mazingira mawili tofauti, hakuna Mtanzania utakaye mwambia asitii Dola aingie barabarani kwa ajili ya Mbowe, hata Wachaga wenyewe KLM hawatomtii ije kuwa TZ nzima?
Hivyo ni ngumu maadamu Tanzania hakuna Siasa za Kikabila au Kidini ni ngumu kushawishi kukubali kuumia kwa ajili ya Mwanasiasa, hiyo ndiyo tofauti na Kenya, kwani Raila Odinga ni Mfalme wa Wajaluo, ...
Haahaaa wapinzani hawana ufuasi ssa mlizuia UKUTA ya nini ?? Kivp mzuie mikutano ya hadhara kma upinzani hawana wafuasi hivi bila wafuasi wangefikisha kura million 6 au million 5 Za ubunge?? Btw waliachiana majimbo hivyo upinzani majimboni wanamajimbo almost 80 so usipotoshe umma
 
Unafikiri Kenya Uhuru Kenya ana uwezo wa kuzuia ukuta kama Tanzania?
 
Huu si ushauri mpya, wala si kwamba haijatokea Tanzania. CUF ni chama cha upinzani hapa Tanzania. Maalim Seif alijitoa kwenye uchaguzi Zanzibar baada ya kuona tume ile ile iliyokataa kumtangaza yeye kuwa mshindi, inaratibu uchaguzi mwingine wa marudio. Kwa ufupi hakukuwa na haja ya kuanzisha thread hii kwani ulichoshauri kilishafanyika miaka miwili iliyopita. Sana sana ungeanzisha thread ya kumpongeza Raila kwa kuwaiga wapinzani wa Tanzania. Mods futeni huu uzi jamaa amepitiwa

Huyo kibabu Mpenda Misifa Gucci Mane aka Nyani kaacha ku-analyze video za Chris Brown na Rihanna leo kaibukia kwenye midahalo isiyo level yake. Aibuuuu!!
 
Unafikiri Kenya Uhuru Kenya ana uwezo wa kuzuia ukuta kama Tanzania?
Sababu kule walichinjana hilo tu basi ndio Maana Wanamhanya Odinga ila naye kma 2007 asingemtuma ruto kuchinja wakikuyu makanisani basi upinzani kenya ungeshakufa cku nyingi

Hata hapa Tanzania mfano 2015 lowasa angekinukisha bara alafu seif akinukishe visiwani yaani watu waingie barabarani kwa mafuriko kma ya kwenye kampeni wachome ofisi za NEC nchi nzima mbona tungeheshimiana tu ila Tanzania kinachowapa ccm kiburi ni upole wa wapinzani ndio maana mna jeuri ya kuwaita vilaza
 
Watu wengi hamjajua kwanini raila kafanya alichokifanya na hamjuhi hata katiba yao inasemaje pale mgombea anapojitoa.

Kifupi tu:-
1. Mgombea akijitoa huko kenya uchaguzi unasimmishwa na tume inatangaza upya wagombea.
2. raila alikuwa anamadai anataka yatekelezwe na Uhuru nadhani walikuwa wansingizia muda hautoshi na haupo.
3. So kitendo cha kujitoa ni msg kwa tume na serekali kuwa jipangeni sasa mfanye marekebisho na uchaguzi uitishwe upya.

All in all anacholingia Raila ni Katiba mpya ya kenya ambayo hakika imetoa uhuru mkubwa sana wa kidemokrasia kwa wapinzani. na nachofanya raila ni kuabuse huo uhuru, na hapa usifikiri NASA watakaa kimya kw avyovyote wana majority Bungeni so vipengele kama hivi hakika wataenda kuvibadilisha vyote, maana kwa sasa vinatumika vibaya.
Raila Ana abuse uhuru wa kikatiba? Yaani ulitaka Angie kwenye uchaguzi ambao unaendeshwa na tume mbovu? Kma hya ndio maoni ya watanzania wote basi tuna safari ndefu sana ya kufikia demokrasia ya kweli
 
Kila mwaka wa uchaguzi mnashiriki chaguzi za kutafuta viongozi wa ngazi mbalimbali nchini.

Chaguzi mnazoshiriki huendeshwa na kuratibiwa na tume ya taifa ya uchaguzi.

Huku mkiwa mnajua kabisa jinsi ambavyo hiyo tume huundwa, huwa mnashiriki na si ajabu kujipa matumaini hewa kuwa mwaweza kushinda, hususan nafasi ya urais.

Kwa jinsi ilivyo sasa mtaendelea kuishia kujipa matumaini hewa tu kwa sababu mshindi wa hiyo nafasi ya urais ni 'a foregone conclusion'.

Kama ilivyo ada, matokeo yakishatangazwa huwa mnayakataa na kuanza kudai kuwa tume haipo huru.

Kama mnaona tume haipo huru [jambo ambalo nakubaliana nalo], kwa nini huwa mnaamua kushiriki chaguzi zinazoendeshwa na hiyo tume?

Leo Raila Odinga na muungano wao wa NASA wameamua kujitoa ushiriki wao kwenye marudio ya uchaguzi uliokuwa umepangwa kufanyika baadaye mwezi huu kwa sababu hawajaridhishwa na utendaji wa hiyo tume.

Muda umefika sasa na nyie muache kushiriki chaguzi ziendeshwazo na tume ambayo hamna imani nayo. La sivyo, mtaendelea kuwa wasindikizaji wa CCM ikulu maana msitegemee tume ya uchaguzi iliyoundwa na mwenyekiti wa CCM ije kuwatangaza washindi.

Fuateni nyayo za Raila hata kama mnampenda Uhuru.
nonsense
 
Sababu kule walichinjana hilo tu basi ndio Maana Wanamhanya Odinga ila naye kma 2007 asingemtuma ruto kuchinja wakikuyu makanisani basi upinzani kenya ungeshakufa cku nyingi

Hata hapa Tanzania mfano 2015 lowasa angekinukisha bara alafu seif akinukishe visiwani yaani watu waingie barabarani kwa mafuriko kma ya kwenye kampeni wachome ofisi za NEC nchi nzima mbona tungeheshimiana tu ila Tanzania kinachowapa ccm kiburi ni upole wa wapinzani ndio maana mna jeuri ya kuwaita vilaza

Mnadanganywa sana si Fisadi Lowasa wala yoyote mwenye uwezo wa kukinukisha Tanzania, wangekuwa na huwo uwezo wangeshautumia kuishinikiza Serikali, Lowasa hawezi kumuingiza mtu barabarani Tanzania nakuhakikishia hilo, angeshautumia!
 
Ipo siku hata tume yenyewe itachoka.Cha msingi ni wananchi kuamua wanataka nini!Bado hawajaamua kuongozwa na upinzan ila siku wakiamua, Hata Rais awe mwenyekiti wa tume atatangaza upinzani.Mi nasubiri Sizonje achokwe na wasukuma wenzake maana kwa sasa huko Dsm,Arusha,Kilimanjaro,Mbeya nk washamchoka.Siku Mwanza wakiweka ukabila wao pembeni ndio ccm kwisha!Maana kwa sasa mkoa wenu wa kujidia ni Dodoma tuu.
Tatizo LA upinzani Tanzanian wanadhani kuongoza nchi mpaka ushinde urais. Kuna wsnasheria lukuki huko upinzsni lakini wanasahau kuisoma hiyo hiyo katiba y'all chama kimoja inawapa uwexo wa kuunda serikali kwa sharti moja wawe name wabunge wengi zaidi bungeni. Lakini wao wapo busy kuazima wagombea kutoka ccm. Hivi hawajuil Kama lowasa angekua rais mbowe name wenzake wasingepata uwaziri wangeishia ukuu wa mikoa. Someni vizuri katiba ina mwanya mzuri sana wa kutumia kuirekebisha lakini ndo hivyo tena
 
Kila mwaka wa uchaguzi mnashiriki chaguzi za kutafuta viongozi wa ngazi mbalimbali nchini.

Chaguzi mnazoshiriki huendeshwa na kuratibiwa na tume ya taifa ya uchaguzi.

Huku mkiwa mnajua kabisa jinsi ambavyo hiyo tume huundwa, huwa mnashiriki na si ajabu kujipa matumaini hewa kuwa mwaweza kushinda, hususan nafasi ya urais.

Kwa jinsi ilivyo sasa mtaendelea kuishia kujipa matumaini hewa tu kwa sababu mshindi wa hiyo nafasi ya urais ni 'a foregone conclusion'.

Kama ilivyo ada, matokeo yakishatangazwa huwa mnayakataa na kuanza kudai kuwa tume haipo huru.

Kama mnaona tume haipo huru [jambo ambalo nakubaliana nalo], kwa nini huwa mnaamua kushiriki chaguzi zinazoendeshwa na hiyo tume?

Leo Raila Odinga na muungano wao wa NASA wameamua kujitoa ushiriki wao kwenye marudio ya uchaguzi uliokuwa umepangwa kufanyika baadaye mwezi huu kwa sababu hawajaridhishwa na utendaji wa hiyo tume.

Muda umefika sasa na nyie muache kushiriki chaguzi ziendeshwazo na tume ambayo hamna imani nayo. La sivyo, mtaendelea kuwa wasindikizaji wa CCM ikulu maana msitegemee tume ya uchaguzi iliyoundwa na mwenyekiti wa CCM ije kuwatangaza washindi.

Fuateni nyayo za Raila hata kama mnampenda Uhuru.

Wapinzani wa Tanzania nao aidha ni wajinga wa kiwango cha lami au ni matawi ya mfumo
Wao efforts zao hata hazikupaswa kuwa kwenye kushiriki uchaguzi.kupiga kampeni na kutaka kushinda
efforts zao zilipaswa kuwa katika katiba na kutafuta Tume Huru.
Kuendelea kushiriki kwenye chaguzi kila wakati na mazingira ni yaleyale na ukategemea matokeo tofauti.Huo ni uzwazwa wa kiwango cha lami.
 
Tatizo LA upinzani Tanzanian wanadhani kuongoza nchi mpaka ushinde urais. Kuna wsnasheria lukuki huko upinzsni lakini wanasahau kuisoma hiyo hiyo katiba y'all chama kimoja inawapa uwexo wa kuunda serikali kwa sharti moja wawe name wabunge wengi zaidi bungeni. Lakini wao wapo busy kuazima wagombea kutoka ccm. Hivi hawajuil Kama lowasa angekua rais mbowe name wenzake wasingepata uwaziri wangeishia ukuu wa mikoa. Someni vizuri katiba ina mwanya mzuri sana wa kutumia kuirekebisha lakini ndo hivyo tena
mkuu wewe pia unashindwa kuelewa ugumu uliopo.Kwani hao wabunge wanapitishwa na nani? Si ni tume hio hio?
Hivi unajua majimboni nani ni kiongozi wa Tume? Kwa taarifa yako ni Mkurugenzi wa wilaya husika
unajua kuwa wakurugenzi wote wanateuliwa na Mwenyekiti wa CCM ambaye naye huwa ni mgombea wa Urais?
Tatizo hapo ni Tume ya Uchaguzi na si vinginevyo
Wenje na Kafulila wameporwa live na hakuna kilichoendelea
Kwa taarifa yako tume itaendelea kuhakikisha upinzani unakuwa na minority isiyo na uwezo wa kufanya maamuzi
 
Raila Ana abuse uhuru wa kikatiba? Yaani ulitaka Angie kwenye uchaguzi ambao unaendeshwa na tume mbovu? Kma hya ndio maoni ya watanzania wote basi tuna safari ndefu sana ya kufikia demokrasia ya kweli

Kwanini maoni yangu useme ni ya waTanzania wote?
au unajaribu kujitoa ufahamu?
 
Mnadanganywa sana si Fisadi Lowasa wala yoyote mwenye uwezo wa kukinukisha Tanzania, wangekuwa na huwo uwezo wangeshautumia kuishinikiza Serikali, Lowasa hawezi kumuingiza mtu barabarani Tanzania nakuhakikishia hilo, angeshautumia!
aisee kwa ile hali ya 2015 chochote kingewezekana.Ile hali haikuwa ya kawaida.Shukuruni tu mliwachezea wapinzani kete kali mkampeleka lowasa upinzani ili awasaidie
 
Back
Top Bottom