Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 98,439
- 145,410
Ni kwel kabisa ulichosema ila kususia uchaguzi itakuwa ni moja ya njia ya kujiua kisiasa, hii tume ya uchaguzi ni kweli inasimamishwa na mtu mmoja na ni ngumu sana wakamsaliti yule aliyewapa madaraka.
Nikirudi Tz nitaongea mengi sana (samaki mwenye maji mdomoni ana mengi ya kuongea)
Sidhani kama kususia itakuwa ni kujiua kisiasa.
Kwa sababu, kwa nini mtu ushiriki uchaguzi huku ukijua kuwa tume ya uchaguzi haiko huru, halafu ukishindwa ndo uanze kulalamika eti tume yenyewe haiko huru?
Kwa nini ushiriki uchaguzi ambao unajua unaendeshwa na tume isiyo huru?
Sioni kabisa sababu aisee.
Ukishaamua kushiriki kwenye uchaguzi unaoendeshwa na hiyo tume maana yake ni umeikubali hata tume yenyewe na hivyo kuja kulalamika kuwa haiko huru baada ya kushindwa unakuwa huna mamlaka ya kimaadili na unaonekana mzushi tu.
Naunga mkono hoja. Wapinzani wetu wako bize na mambo mengine mpaka kampeni za uchaguzi wa mwaka 2020 zitakapo tangazwa.
Pasco
Kwani ukirudi utaongelea wapi majukwaani au kwenye vipindi vya TV, kama ni humu humu JF kwani inashindikana nini kuongeza saa hizi.Nikirudi Tz nitaongea mengi sana (samaki mwenye maji mdomoni ana mengi ya kuongea)
Hawawezi kususia uchaguzi ni sawa sawa kumuachia nguruwe akuchomee mishikaki.
Kingine hawa viongozi wa kudumu wa vyama vya upinzani wameishayazoea hayo maisha ya kuwa wapinzani wa kudumu.
Hata wakishindwa kwao uwa siyo tatizo wafuasi wao ndiyo wanaoumia.
Ndugu yangu Nyani Ngabu kwa akili yako kuna Chama gani cha kukikabidhi Nchi hii zaidi ya CCM? Hatuwezi kuiweka Nchi hii rehani kwa kuwapa watu walioachwa na CCM kwa rekodi mbaya ya ama utendaji au Ufisadi!Sabalkheri na masalkheri mabibi na mabwana popote pale mlipo kwenye pembe ya dunia hii.
Natumai nyote mna na mmekuwa na Jumapili njema kabisa kama ilivyo kwangu.
Baada ya salamu ngoja nizame sasa kwenye hoja ya mada husika.
Tayari kuna minong'ono ya hapa na pale iliyoanza kusikika kuhusu nani labda atagombea urais kupitia kile chama kikubwa cha upinzani au kupitia mwamvuli wa UKAWA.
Jambo ambalo linanishangaza ni ukimya wa vyama vya upinzani kuhusu chombo kinachoendesha na kusimamia chaguzi zetu, tume ya taifa ya uchaguzi.
Wengi tunajua jinsi ambavyo uongozi wa hicho chombo unavyoundwa. Na naamini tupo kadhaa ambao hatuna imani kivile na hicho chombo kutokana na ukweli kuwa huwa kinaundwa na rais aliyeko madarakani na ambaye mpaka sasa amekuwa ndiyo mwenyekiti wa chama tawala cha CCM.
Kwa mtaji huo, baadhi yetu huona dosari iliyopo katika muundo mzima wa hicho chombo. Binafsi naamini rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania/ mwenyekiti wa CCM huwa anaweka makada wa chama chake pale ili kulinda na kuhifadhi maslahi ya chama chake endapo ikibidi kufanya hivyo.
Tayari tumeshaona aliyekuwa makamu mwenyekiti wa tume hiyo hapo zamani, Jaji Agustino Ramadhani, alipotangaza nia ya kugombea urais kupitia CCM. Huyu mtu mimi naamini hata alipokuwa makamu mwenyekiti wa hiyo tume ya uchaguzi, pia alikuwa kada wa chama chake kwa wakati huo huo.
Sasa sijui hivi vyama vyetu vya upinzani vimejipangaje kuhusu hilo suala la tume ya uchaguzi. Tume ya uchaguzi inayoundwa na mtu mmoja, tena mtu mwenyewe ndiye mwenyekiti wa chama tawala na mgombea mtarajiwa wa urais kupitia chama chake, haiwezi kuwa huru hata kidogo.
Haiwezi kuwa huru kwa sababu ina wiwa [beholden] na shukurani kwake yeye huyo aliyeiunda.
Mimi ningependa kuona vyama vya upinzani vikisusia kabisa chaguzi kuu zote zijazo hadi hapo tutapokuja na njia ya kuunda chombo kilicho huru cha kuendesha na kusimamia chaguzi zetu.
Kinyume na hapo, wapinzani daima watakuwa wanainsindikiza CCM ikulu halafu baadaye watajifanya kuyasusia matokeo, kutokumtambua rais, na mwisho wao wenyewe kuachia msimamo wao na kumkubali rais aliyepo ikulu.
Sioni kabisa sababu ya kushiriki chaguzi ambazo zinasimamiwa na chombo kisicho huru. Kwa jinsi ilivyo sasa hivi, wapinzani kamwe hawatoiona ikulu. Hata uwingi wa wabunge watauona kwa CCM tu.
Tume ya taifa ya uchaguzi iliyopo sasa hivi haipo kwa ajili manufaa ya Watanzania wote. Ipo kwa ajili ya manufaa ya CCM. Hivyo ndivyo niaminivyo.
Hivi jamani nyie mnasikilizaga vyombo gani vya habari? Upinzani hawa kila siku wanalalamikia haya mambo hamsikii.hakuna kususia uchaguzi CCM itajimaliza yenyewe hasa awamu hii tunayoenda nayo.Cha kushangaza hawa jamaa hawajawahi kuitisha maandamano au kususia bunge linapokuja suala la usimamizi wa uchaguzi...
Nikitafakari suala na tume huru ya uchaguzi na suala la wakurugenzi wa halmashauri kuwa wasimamizi wa uchaguzi, hadi huwa nahisi hivi vyama ni mawakala wa chama kile ila wanakuja kwetu kubalance equation Tu. In actual fact kwa muundo wa tume na usimamizi wa uchaguzi hawa jamaa wameshindwa kabla hata uchaguzi haujaitishwa
Ndugu yangu Nyani Ngabu kwa akili yako kuna Chama gani cha kukikabidhi Nchi hii zaidi ya CCM? Hatuwezi kuiweka Nchi hii rehani kwa kuwapa watu walioachwa na CCM kwa rekodi mbaya ya ama utendaji au Ufisadi!
Tume huru haiwezi kuja kwa katiba hii iliyopo kwanza nishauri wapinzani wapiganie katiba mpya yenye tume huru ndani yake..Sabalkheri na masalkheri mabibi na mabwana popote pale mlipo kwenye pembe ya dunia hii.
Natumai nyote mna na mmekuwa na Jumapili njema kabisa kama ilivyo kwangu.
Baada ya salamu ngoja nizame sasa kwenye hoja ya mada husika.
Tayari kuna minong'ono ya hapa na pale iliyoanza kusikika kuhusu nani labda atagombea urais kupitia kile chama kikubwa cha upinzani au kupitia mwamvuli wa UKAWA.
Jambo ambalo linanishangaza ni ukimya wa vyama vya upinzani kuhusu chombo kinachoendesha na kusimamia chaguzi zetu, tume ya taifa ya uchaguzi.
Wengi tunajua jinsi ambavyo uongozi wa hicho chombo unavyoundwa. Na naamini tupo kadhaa ambao hatuna imani kivile na hicho chombo kutokana na ukweli kuwa huwa kinaundwa na rais aliyeko madarakani na ambaye mpaka sasa amekuwa ndiyo mwenyekiti wa chama tawala cha CCM.
Kwa mtaji huo, baadhi yetu huona dosari iliyopo katika muundo mzima wa hicho chombo. Binafsi naamini rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania/ mwenyekiti wa CCM huwa anaweka makada wa chama chake pale ili kulinda na kuhifadhi maslahi ya chama chake endapo ikibidi kufanya hivyo.
Tayari tumeshaona aliyekuwa makamu mwenyekiti wa tume hiyo hapo zamani, Jaji Agustino Ramadhani, alipotangaza nia ya kugombea urais kupitia CCM. Huyu mtu mimi naamini hata alipokuwa makamu mwenyekiti wa hiyo tume ya uchaguzi, pia alikuwa kada wa chama chake kwa wakati huo huo.
Sasa sijui hivi vyama vyetu vya upinzani vimejipangaje kuhusu hilo suala la tume ya uchaguzi. Tume ya uchaguzi inayoundwa na mtu mmoja, tena mtu mwenyewe ndiye mwenyekiti wa chama tawala na mgombea mtarajiwa wa urais kupitia chama chake, haiwezi kuwa huru hata kidogo.
Haiwezi kuwa huru kwa sababu ina wiwa [beholden] na shukurani kwake yeye huyo aliyeiunda.
Mimi ningependa kuona vyama vya upinzani vikisusia kabisa chaguzi kuu zote zijazo hadi hapo tutapokuja na njia ya kuunda chombo kilicho huru cha kuendesha na kusimamia chaguzi zetu.
Kinyume na hapo, wapinzani daima watakuwa wanainsindikiza CCM ikulu halafu baadaye watajifanya kuyasusia matokeo, kutokumtambua rais, na mwisho wao wenyewe kuachia msimamo wao na kumkubali rais aliyepo ikulu.
Sioni kabisa sababu ya kushiriki chaguzi ambazo zinasimamiwa na chombo kisicho huru. Kwa jinsi ilivyo sasa hivi, wapinzani kamwe hawatoiona ikulu. Hata uwingi wa wabunge watauona kwa CCM tu.
Tume ya taifa ya uchaguzi iliyopo sasa hivi haipo kwa ajili manufaa ya Watanzania wote. Ipo kwa ajili ya manufaa ya CCM. Hivyo ndivyo niaminivyo.
*Angalizo*
[Kuwa na tume huru ya uchaguzi haimaanishi moja kwa moja kuwa CCM itashindwa na wapinzani watashinda kwenye chaguzi kuu. Tunachotaka baadhi yetu ni kuwa na tume huru inayoaminika.]
Tume huru haiwezi kuja kwa katiba hii iliyopo kwanza nishauri wapinzani wapiganie katiba mpya yenye tume huru ndani yake..
Bila hivyo ni mpuuzi pekee atakayekwenda kujipanga kwenye mstari kupigia kura upinzani mwaka 2020