RAI - Nguvu ya Hoja?

Wacha nimpigie Balile nisikie anasemaje .Sijui kama atakumbuka utabiri wangu .

ukimpata mwambie kuwa alianzisha mjadala hapa JF kisha hakurudi kujibu hoja zangu

Mwambie kuwa I really miss him na michango yake...na tunamhitaji arudi
 
Baada ya wazee wa ufisadi sasa ni wakati wa makuwadi wao.....

Tanzanianjema
 
Habari zinazoingia sasa hivi zinadokeza kuwa Mhariri wa gazeti la RAI Bw. Balile ameondolewa wadhifa wake huo. More to come!

Hivi huyu mtu ni vipi hasa? Wakuu wenye habari zake tupeni vizuri mara ya mwisho niliona akiepwa heshima sana hapa JF kuwa amemamliza shule UK, hivi huyu ni nani ayways?
 
Hivi huyu mtu ni vipi hasa? Wakuu wenye habari zake tupeni vizuri mara ya mwisho niliona akiepwa heshima sana hapa JF kuwa amemamliza shule UK, hivi huyu ni nani ayways?


ES
MBONA mTALII ALISHAMWELEZEA VIZURI TUU HUKO NYUMA? HEBU SOMA HAPA:

Balile Acha Kujipendekeza Kwa Membe

SOURCE BONYEZA HAPA:

https://www.jamiiforums.com/newreply.php?do=newreply&p=58038
 
WANg'oane hata meno,si ni mafisadi na dawa ya msaliti siku zote ni hiyo.sina cha kumsikitikia kwani kajitakia
 
Kithuku kuwa mtulivu na soma kwa makini mabandiko juu ya Balile hapa jamvini .Kwa nini ni habari then uje ujadili vinginevyo tulia mkuu wacha tufuatilie .

Nimekupata mkuu, ndio nimemaliza kuyasoma. Nakajua haka kajamaa kwa mbali kalipokuwa na gazeti la Tanzania Daima, lakini sikuwahi kufikiri kuwa kalikuwa na ushawishi wowote (wa maana) katika mambo ya kitaifa. Halafu akawa "mtetezi" wa Lowassa "kiaina" wakati wa Richmond. Sikumbuki walikosana vipi na Mbowe au walishindana tu kimaslahi, ndipo nikasikia yuko kwenye Rai. Ndipo nikadhani kwa habari ya leo, kuondoka (ama kuondolewa) kwake huko kwenye "Rai" ni sawa tu na alivyoondoka (au kuondolewa) kwa Mbowe, au kuna tofauti wakuu? Sijaona tofauti kati yake na yule mwimbaji Waziri Sonyo aliyekuwa anahamahama bendi kila kukicha. Atakaa mtaani kwa muda, utamsikia kesho yuko na gazeti lingine, namwona ni sawa tu na madereva wa daladala za Kiwalani, Manzese au sehemu kama hizo.
 
...........................hata kama ameacha kazi itakuwa zuga tu..baada ya kugundulika hata ni mtoto kuwa anatumika...haimgekuwa busara kuwa naye....ila watampeleka mahali pengine......
 
...........................hata kama ameacha kazi itakuwa zuga tu..baada ya kugundulika hata ni mtoto kuwa anatumika...haimgekuwa busara kuwa naye....ila watampeleka mahali pengine......


Popote watakapompeleka tutamfuatilia... hatutaweza tu kumfuatilia kuzimu...., acha nicheze mie.., mafisadi, watoto wa mafisadi, makuwadi wao na washenga wao wote tunao tu.

Waberoya
 
Wakuu, naomba msaada kwa mwenye jibu, siku nne zilizopita niliweka tahariri ya Tanzanian Daima ikishutumu ukiukwaji wa Bablile kimaadili, Je, kwa nini haikuliona jua hapa likichwa?
 
Hii ndo dawa safi ya makuwadi, na liwe fundisho kwa wengine wenye kupenda kujikomba komba hata wakadhalilisha utu wao na taaluma zao!
 
kichwa kukubwa akili ndogo. mwache aende na sijui ataajiriwa na nani kwa upeo alionao mdogo
 
Hii ndo dawa safi ya makuwadi, na liwe fundisho kwa wengine wenye kupenda kujikomba komba hata wakadhalilisha utu wao na taaluma zao!

Ni kweli uyasemayo. Huyu jamaa ni miongoni mwa makuwadi wengi wanaotumia vibaya taaluma zao kwa lengo la kushibisha matumbo yao. tena wakiachwa vivi hivi wanaweza kukiharibu kizazi kijacho kikawa cha mafisadi.
 
Habari zinazoingia sasa hivi zinadokeza kuwa Mhariri wa gazeti la RAI Bw. Balile ameondolewa wadhifa wake huo. More to come!

Nadhani hawajakosea na kilichomponza ni kujipendekeza kwake kwa mafisadi kwa sababu ya vyeti vya usuluhisi wa migogoro na dharau kwa wengine. kujipendekeza kwa mafisadi kunamfanya ajione kaimaliza dunia yote. wasahili wanasema, akili ya darasani ni punguani wa mtaani. maisha siku zote yanahitaji busara; kutenda kwa wema kwa maslahi ya walio wengi, siku kwa maslahi yako na wanao. lakini hawa mafisadi si mlisema wana mtandao mkubwa kwa hao mnaowaita waandishi? hewa fuatlieni mtujulishe na 'mapopo'.
 



Maneno yako yana uzito mkubwa mno na yanaweza yakawa yamezima mjadala huu .Asante sana kwa ujumbe huu .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…