Nimepitia makala yako sioni umuhimu wa kusema kuwa wafanyakazi wa wizara ya mambo ya nje wanahitaji kusoma kozi ya conflict Resolution ili waweze kutatua migogoro.
Jee DR.Salim Ahmed Salim ambaye amekubaliwa na mataifa yote atuwakilishe ana hiyo qualification? au duniani hakuna watu wenye hiyo digrii?ndio maana akapewa Salim Ahmed?
Mwalimu Nyerere nae alikuwa akipewa kazi hizo jeee nae ana digrii hiyo?
kusema kuwa wizarani hakuna watendaji si kweli labda una chuki nao tu, na kitendo chako cha kuwa Ulaya huko HULL haina maana kuwa wewe ndio mjuaji kuliko watu walioko wizarani.
WaTanzania hao hao ndio waliopewa dhamana huko mahakama ya Arusha mtu kama jaji Chande hana CONFLICT RESOLUTION.
BALILE hatuwezi kuwekeza kwenye fani ya migogoro kwa kiasi unachotaka wewe ( miaka 19-30) mtu ukisomea migogoro unakuwa umejibana sana.
kuna rafiki yangu alipata division one point saba ECA badala ya kwenda UDSM kufanya B.COM au kozi nyingine akaenda kufanya Material management Mzumbe kisa alimuona jirani yake anamiliki gari na alikuwa akifanya kazi kampuni ya chakula cha kuku.
huyo jamaa yangu alitafuta sana kazi hakupata, kwani kozi aliyoisoma ilikuwa ina nguvu kipindi cha ukiritimba wa Mwalimu.
kifupi kuna kozi ambazo ni short term na hazina future in long term.
BALILE uliza wangapi wamemaliza INTERNATIONAL RELATIONS na wanatembea na vyeti vyao mikononi?itakuwa na hiyo kozi yako?sababu International Relation eneo lake ni finyu sana ukikosa kazi wizara ya mambo ya nje inakuwa taabu maeneo mengine.
hiyo migogoro iko mingapi ambayo tutapewa?
imagine wewe umesoma B.A CONFLICT RESOLUTION na unafanya kazi wizara ya nje unashughulikia mgogoro wa Zimbambwe jee unapoisha mgogoro wa Zimbambwe unafanya nini? ukifukuzwa kazi wizara ya mambo ya nje utafanya kazi wapi?
Najua inawezekana ndungu yangu unababaika na kila cha ulaya kuna vingine si vyetu.ukitizama westminster university wana masters ya LONDON STUDIES jee kozi hii inatusaidia nini sisi kama watanzania? au na sisi tuanzishe DSM STUDIES?
Wizara kama wizara itakuwa na mtaalam wa mambo hayo lakini si kuidharau wizara na kutulazimisha tusomeshe kwa wingi conflict Resolution. tena usiwadanyanye watu wafanye undergraduate. mtu anaweza kuwa na Law halafu masters akafanya hiyo kozi yako ili awe na pa kushikia.
Makala ya Balile.
Makala -Membe; fursa hii tusiipoteze