Nimekupata mkuu, ndio nimemaliza kuyasoma. Nakajua haka kajamaa kwa mbali kalipokuwa na gazeti la Tanzania Daima, lakini sikuwahi kufikiri kuwa kalikuwa na ushawishi wowote (wa maana) katika mambo ya kitaifa. Halafu akawa "mtetezi" wa Lowassa "kiaina" wakati wa Richmond. Sikumbuki walikosana vipi na Mbowe au walishindana tu kimaslahi, ndipo nikasikia yuko kwenye Rai. Ndipo nikadhani kwa habari ya leo, kuondoka (ama kuondolewa) kwake huko kwenye "Rai" ni sawa tu na alivyoondoka (au kuondolewa) kwa Mbowe, au kuna tofauti wakuu? Sijaona tofauti kati yake na yule mwimbaji Waziri Sonyo aliyekuwa anahamahama bendi kila kukicha. Atakaa mtaani kwa muda, utamsikia kesho yuko na gazeti lingine, namwona ni sawa tu na madereva wa daladala za Kiwalani, Manzese au sehemu kama hizo.