Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ungechukua fomu mkuuNinavyojua Rais Magufuli anatembea kwenye viatu vya Nyerere.
Sawa mkuuHao walikuwa wanatumiwa na Mabeberu sasa Mabeberu yamewaingiza king baada ya kukubali uzalendo wa Rais Magufuli.
Kujinasibu ama kupewa sifa na watu wengine vyote vinaangukia katika kipengele cha MISTAKEN IDENTITY ambacho ndio dhima kuu ya mada hii.kwenye andiko lako sijaona mahali huyo marehemu akijinasibu kuwa yeye ni usalama wa taifa mpaka ikapelekea kifo chake.
Ignorance/ujinga/kutokujua kwao...Cha msingi, tambua ni kipi haswa kilichowavuta kukuhisi hivyo
Kama ndicho basi waelimishe. Hiyo ndiyo suluhu.Ignorance/ujinga/kutokujua kwao...
Watu wa usalama hawana muonekano wowote wa kipekee...Kama ni kwa sababu ya muonekano wako badilika.
Kwani hapa tunaongelea watu wa usalama ama kufananishwa na watu wa usalama? Nimekuambia uchambue ni nini haswa kinawafanya watu wakuhisi hivyo. Then, change.Watu wa usalama hawana muonekano wowote wa kipekee...
Hapa sawa plus katazo la Polisi.Kama ndicho basi waelimishe. Hiyo ndiyo suluhu.
Comment yako #172 hapo juu umesema kwambaKwani hapa tunaongelea watu wa usalama ama kufananishwa na watu wa usalama? Nimekuambia uchambue ni nini haswa kinawafanya watu wakuhisi hivyo. Then, change.
Hayawani!!Mbowe atimuliwa jukwaani na wanachadema huko hai! Hawamtaki.
Tena ni hayawani yule wa kiwango cha SGRHayawani!!
Hii Nchi imetoka mbali yale mawazo na ndoto za Nyerere yanaanza kutekelezwa na Rais Magufuli.Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums.
Ndugu yangu;
Mtanzania Raia Mpenda Misifa: Ukiambiwa umefanana na mtu wa usalama usifurahie. Hiyo sio sifa nzuri. Unaweza ukadhurika kwa bahati mbaya (Mistaken Identity);
Huko mtaani mnapoishi kuna watu ambao ni hatari sana kwa ustawi wa Tanzania yetu. Huko mnaishi na majambazi, magaidi (kama wale wa Mkuranga, Kibiti na Rufiji), wezi, vibaka, wauza mihadarati (bangi, gongo) ambao wote hao hawawapendi watu wa usalama wa nchi hata kidogo.
Nimeamua kuliongelea hili suala leo kwa maana kwamba, kwa siku za hivi karibuni kumeibuka na wimbi kubwa sana la vijana wenzangu wanaopenda kujitambulisha kuwa wao ni watu wa kwenye system kwa lengo/minadi ya kujitafutia umaarufu pamoja na sifa huko mitaani, mbele ya kadamnasi na wanawake warembo. Wengine wameenda mbali zaidi wakijitambulisha kuwa wao ni watumishi wa usalama wa taifa kwa lengo la kutaka kufanya utapeli jambo ambalo sio sahihi kabisa.
Soma thread hii hapa: Watu wanahisi mimi ni usalama wa taifa, naombeni ushauri
KISA KIDOGO CHA WATU WA USALAMA WA MOSSAD WALIVYOMUUA MTU KWA KUMFANANISHA (MISTAKEN IDENTITY)
===========
Miezi tisa baada ya tukio la Munich, July 1973 majasusi wa Mossad walipewa taarifa na mashushu wao wa Ulaya kuhusu uwepo wa Ali Hassan Salameh huko mjini Lillehammer, kaskazini mwa Norway. Michael Harari, aliyekuwa msaidizi wa Zvi Zamir alichukua vijana wake wa kazi na kwenda nchini Norway.
Siku chache baadaye, mkurugenzi wa Mossad Zvi Zamir alijiunga na timu hiyo. Ilikuwa ni utamaduni wa wakuu wa vyombo vya dola wa Israel kuwepo mstari wa mbele wakati wa kazi maalum.
Ni kwa muktadha huo huo, Yonatan 'Yoni' Netanyahu, kaka wa waziri mkuu wa sasa, Benyamin Netanyahu aliongoza kikosi cha makomandoo cha Sayeret Matkal katika operesheni ya Entebe (Operesheni Thunderbolt) ya kuwakomboa waisrael waliotekwa kwenye ndege, huko Entebe, Uganda. Yonatan alikufa katika misheni hiyo ya mwaka 1976.
Zamir alifuata utamaduni huo huo na kufika nchini Norway ili kumuua Ali Hassan Salameh. Kwa masaa mengi walimfuatilia mtu waliyeamini ni Salameh. Ilikuwa usiku, lakini binti mmoja aliyeitwa Marianne Gladnikoff, aliyeletwa na Michael Hariri kwenye timu hiyo ya Mossad alishtuka akasema mtu yule hakuwa Salameh, wakampuuza.
Walipomfuatilia hadi sehemu muafaka, Vijana wa Mossad waliofunzwa mahususi kwa kuua, walirusha risasi na kumuua mtu yule, bila kumjeruhi mwanamke aliyekua akitembea naye barabarani.
Kisha wauaji walirudi hadi jijini Oslo na kujificha kwenye nyumba salama. Hakukuwahi kufanyika mauaji katika mji wa Lillehammer kwa miaka 40, kwa hiyo ilikuwa tukio la ajabu sana kwa wakazi wa mji huo.
Lakini kesho yake iligundulika kuwa, aliyeuawa sio Ali Hassan Salameh, na mtu mwenye jina hilo hakuwepo nchini Norway. Ilikuwa ni pigo kwa Mossad, lakini pigo kubwa lilikuwa kukamatwa kwa timu yote iliyohusika na mauaji yale, isipokuwa Mkurugenzi Zamir na msaidizi wake Harari ambao walitoroka kwa njia zao binafsi kurudi Israel.
Zamir alitumia boti maalum iliyoandalia na muisrael aishiye Norway ,ambaye ni wakala malum wa Mossad. Karibu kila nchi duniani, wapo wakala wa kutoa msaada kwa waisrael, pamoja na kuwasaidia majasusi wa Mossad wanapohitaji msaada. Mawakala hao huitwa 'Sayan' na mara nyingi ni raia wa nchi wanamoishi, lakini wayahudi.
Jamii ya kimataifa ilishangaa, kwamba Mossad inayosifika kwa ufanisi wake imefanya makosa ya kijinga. Lakini zaidi timu iliyohusika na mauaji hayo ilishindwa kujificha na hivyo kukamatwa kirahisi na polisi wa Norway.
Pamoja na makosa mengime, kosa la kijinga walilofanya ni kutumia usafiri wa kukodi, badala ya kutumia usafiri wa umma.
Serikali ya Israel haikuwahi kukubali hadharani kuhusika na tukio hilo, lakini ilizungumza na serikali ya Norway namna ya kwasaidia raia wake waliokamatwa huko Norway.
Ahmed Bouchiki, raia wa Moroko aliuawa na Mossad kwa kufananishwa na Ali Hassan Salameh........
==========
Hii story niliisoma mwaka 2009 katika moja ya vitabu vyangu vingi nikiwa bado chuoni mwaka wa 2 pale IFM.
Kama raia mwema unaweza ukashiriki katika usalama wa taifa lako kwa kutoa ushirikiano kuanzia ngazi ya mjumbe, serikali ya mtaa wako au ikiwezekana toa taarifa hata kituo kidogo cha polisi kilicho karibu yako.
Usalama na ustawi wa nchi hii ni jukumu la kila mtanzania, mzalendo anayeilipenda taifa lake kwa dhati.
Tupo watanzania takribani milioni 50 sasa, jenga picha kila mmoja akitimiza wajibu wake ipasavyo nchii hii itakuwa mbali kiasi gani?
Unakuta kijana anatamani kufanya kazi TISS lakini wanafunzi wa secondary na primary wanapewa mimba na wahuni mtaa anapoishi anashindwa kwenda kutoa taarifa ofisi ya serikali ya mtaa, kwa mjumbe au hata kituo cha police kilicho karibu yake.
Wahusika watajueaje kama una mapenzi mema na taifa lako bila kuona matendo ya kizalendo?
USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.