Raia muombolezaji apigwa ngumi na mlinzi wa msafara wa Lowassa

Raia muombolezaji apigwa ngumi na mlinzi wa msafara wa Lowassa

Ni mambo ya ajabu sana na huwa yanatokea Africa tu,mtu kashakufa ni maiti mnalinda nini sasa?
Kwamba kuna watu wataiba maiti?
Na hii mijinga linatoka kwake kwenda kuaga mwili wa Lowassa linapigwa ngumi nzito.
Mbona sisi tumemuaga tu kimya kimya.
 
Hivi yule mlinzi hajakamatwa?? Unapigaje mtu asie na silaha yeyoe anaanguka chini kwenye shuguli za msiba??? Hivi ni lini hawa Polisi wataacha huu ukoloni mkongwe??
 
Hivi ngumi ya kushtukizwa unaikwepaje? Imagine tuko jogging halafu ghafla nikuchape left hook unafikiri utakaa uione?😂

Wanaojua mazoezi au boxing anakwepa ngumi muda wowote, sasa huyo kanyenyua mikono juu anajua kabisa ngumi inakuja hajui hata kukwepa
 
Ndio wa kuwa askari, madaraka, wa kulinda raia na viongozi wake!
Traffic barabarani tunaipata fresh, ukienda kituo cha polisi UTAJUTA, ukienda mahakamani balaa, ukikutana na askari wa halmashauri imekula kwako, ukikutana na wale "UNANIJUWA MIMI NI NANI" minyanyaso ya kufa mtu, raia sijuwi ukimbilie wapi?!
Lakini huko masomoni hawafundishwi kutumia nguvu pekee, wanafundishwa na taratibu pia. Hawa watu wana matatizo.
 
Wanaojua mazoezi au boxing anakwepa ngumi muda wowote, sasa huyo kanyenyua mikono juu anajua kabisa ngumi inakuja hajui hata kukwepa
Kaka we unajua ngumi naomba tu weekend moja tuwe wote then katika muda usiojulikana nitakutandika konde boy call me number one baaresaaah. Tuone kama utaliona.
 
Laiti kama angekua mwanamke watu wangesimama dede kupinga ila kwakua ni mwanaume linaonekana ni swala la kwaida tuu
 
Mkuu wakati mwingine hata sisi raia tunakuwa wajinga. Kilichotokea wakati wa kifo cha Magufuli kilinifanya nifikirie mara mbili kuhusu mazishi ya viongozi. Wale waliokufa kwa kukanyagana walikuwa wengi kweli kweli lakini serikali ikadanganya idadi. Kuna jamaa alikwenda kumcheki ndugu yake vyumba vya maiti vya hospital za Muhimbili na Amana akasema kulikuwa na maiti nyingi sana. Na serikali haikujali hata kidogo ilifanya kama ni mbwa wamekufa. Imefika wakati kwa raia kuacha kujipanga au kwenda kwenye mazishi ya hawa viongozi.

Wanakomaga sasa ushamba umewajaa
 
Hawa vijana wetu tunaochukua wa Div 4 ya mwisho wanatupa shida sana. Imagine Taasisi nzima inaonekana hamnazo kisa mtu mmoja kama huyu. Pole sana kwa mwathirika waa tukio hili.
Naamini hataachwa salama mlizn ataadhibiwa tu
 
1708079602854.png
 



Aliyepigwa huyu hapa
 
Kwahiyo marehemu ana thamani kuliko jamaa aliehai watu wanatembea na maradhi utampiga mtu afe alafu uchukuliwe hatua ofisi ikugeuke ilikua haina ulazima wa kutumia nguvu kubwa hivyo hata muongozo wake wa kazi sidhani kama unamtuma hivyo
 
Hakutakiwa kuusogelea misafara kapata posho yake

Kubugia Viroba vya pombe huyo vimemponza pombe sio chai Ona Sasa kilichomkuta angelewa akabaki nyumbani yasingemkuta
Jiulize, kama akifa hakuna kesi ya kujibu hapo, cha kuomba ni Mungu ayapishe mbali, raia anyanyuke apate afueni ajikung'ute mavumbi aende zake.

Lakini kiuhalisia kitendo hicho chaweza kuwa ni chanzo cha kesi ya jinai kubwa na ya kujutia.

Kulikuwa na mazuio yoyote ya raia kuisogelea bara bara?

Na kwa tukio kama hilo je kulikuwa na tangazo kutafsiri umbali gani 'onlookers' wasimame wasisogelee?

Enhe, kulinda, nini kilikuwepo cha kulindwa hapo ili kisiletewe madhara?

Unajua waTz sijui ni laana ama nini, ama ni jamii tuliyomo ndiyo wote tumeoza kifikira namna hii?

Ukimhoji kwa kina huyo mbabe kwa nini kafanya kitendo cha namna hiyo kwa mtu asiyekuwa na dhamira yoyote mbaya ya kuukwaza msafara, wadhani anaweza kuwa na sababu ya maana?

Mwisho wa siku watu kama hao hujuta sana kwa matendo yao ya kinyama wanayowafanyia wenzao wasiokuwa na hatia, hasa sheria zinapowawajibisha kuchukua mkondo na huhisi kuwa wao ni maalumu na wameonelewa.
 
Back
Top Bottom