Raia Mwema: Mbowe na Lissu watofautiana kauli

Raia Mwema: Mbowe na Lissu watofautiana kauli

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2016
Posts
17,506
Reaction score
16,003
Waungwana,

Hadi sasa kuna fukuto, tangu Mbowe asamehewe na Rais Samia kutoka jela hawana maelewano na Lissu. Kuna watu ndani ya Chadema mioyoni mwao walitamani Mbowe asitoke jela.

Muda unatuambia sasa.

Awali, hapa JF kulikuwa na hii thread - Kiongozi wa chama haelewani na yule kiongozi mwenzake, ugomvi ni mkubwa

IMG-20220312-WA0011.jpg
 
Hajatokea mtu wakuweza to handle issues Kama MBOWE, sijui ana moyo wa aina gani....

Kwa ubora wa moyo na akili ya mbowe hata tukitofaitiana naye wote kauli yake huja kudhihirika kuwa ni sahihi

Sio mbaya lissu akawa na msimamo tofauti ila watakutana katikati vizuri tu.

Mbowe alisema amechanja Corona woote tukamtukana...ila lile dikteta la chattle likajiua kwa ujinga wake wa kutaka sifa na kupenda kuabudiwa....Samia kaingia kachanja Corona...
 
Mbowe ameoverstay kwenye cheo chake. Wengine wapate/wanataka nafasi ya uenyekiti.
 
Upuuzi na ulafi wa madaraka, Tanzania ni sumu ya upinzani,

Wekeni tofauti pembeni, Tunataka upinzani imara enyi mbowe na Lisu, acheni uduwanzi!

Tumechoka na migogoro yenu ya kijinga
 
Tatizo chawa hawajazoea watu kuwa wamoja hapo watatumia kila aina ya hila ili viongozi wakuu wasikae pamoja MATAGA vs NYUKI WA MAMA vimeumana
 
Mkweli wa Mungu, Mimi sio CHADEMA Wala CCM ila niwaeleze tu ndugu zangu usije ukawaamini wanasiasa, kwasababu wao pia ni binadamu Wana madhaifu Yao hivyo mengi wao ni chumia tumbo tu hakuna lolote na mtaji wao ni wananchi wapuuzi, wajinga na maskiniaani Mimi nashangaa sana wewe mwenyewe mwanaCHADEMA huna maisha mazuri unaishi kwa tabu ,shida na madeni lakini unafanya kila uwezalo eti Mbowe au Lissu wachangiwe pesa sijui kwaajiri ya shughuri za chama sijui nini yaani ni upumbavu wa kiwaongo Cha juu sana.

Nilishasema na narudia tena sio Mbowe, Lissu, Samia au Zitto ndio wanaweza kukuletea maendeleo iyo ni big no maendeleo ya nchi hii yanahitaji wanachi wenye akili ambao hawataweza kumvumilia kiongozi wa namna yeyote Ile fisadi, mbazilifu, mng'ang'ania madaraka kwa muda mrefu bili matokea chanya yeyote ,Mpenda fedha na mwenye kujijali yeye mwenyewe na familia yake. Hapo ndipo viongozi watajiset na kuwa watu wakuwatumikia wananchi basi lakini sio hizi ngonjera za kipuuzi na kijinga za wao viongozi kugombania maslai Yao binafsi
 
Haikusaidii chochote kukubali kuendelea kuwa mjinga. Mbowe na Lissu Hakuna mahali popote walipotifautiana kauli.

Akiwa Iringa Mbowe aliwakabidhi BAWACHA jukumu la kuongoza Join The Chain Kwa kuwataka kuwa wa kwanza kuleta 1M contributors. Katika kikao hicho hicho akawataka Kwa Umoja wao kusimamia hamasa ya Katiba mpya na wao tayari kupitia Mwenyekiti wa BAWACHA aanaandaa mpangokazi naye kasema Wazi watapita mikoa yote. Alichoongeza Mbowe ni maridhiano na utayari serikali kuhusu uendeshaji wa siasa zisizo za visasi na uhasama.

Lissu kesho yake akiwa Club House akaja na dhana ya utashi wa Rais kuhusu Katiba mpya na mkamponda humu kuhusu kauli hiyo. Wengine Kwa maslahi yenu maana Tangu niwafahamu hamjawahi kuacha umbea mkasema CHADEMA Sasa imejisalimisha baada ya Mwenyekiti na Makamu wake kumtegemea Samia kuleta Katiba huku wakijua Huyo ni CCM na CCM haitaki Katiba mpya.
Sasa Leo mnapokuja na kutofautiana sijui mnakutoa wapi tena wakati Mwanzo mlisema wamesalender?

Mbali ya hayo haiwezekani Mbowe na Lissu wakawa na mawazo yanayofanana Kwa Kila kitu Kila siku. Ukiona hivyo ujue aidha kuna mmoja hafikirii au mmoja anafikiria Kwa niaba ya mwenzake.
 
Kwangu mimi sioni tatizo viongozi kutofautiana katika mitazamo yao, kwani hiyo ni afya kwa taasisi. Nakumbuka kosa la kumpokea Lowassa lilifanyika na viongozi wengi waliunga mkono. Ni vyema viongozi wakatofautiana ili maamuzi sahihi ndio yachukuliwe.
 
Gazeti la Raia mwema toleo la leo limekuja na habari kuwa Mbowe na Lisu wametofautiana baada ya Mbowe kuachana na madai ya katiba mpya na kufuta join the chain ambayo ililenga kumchangia mamilioni ya pesa Lisu ili aendelee kutumbua maisha huko Ubelgiji.
Hebu thibitisha kwamba join the chain zilikuwa hela binafsi za matumizi ya Tundu Lissu.

Huwa haipendezi mtu mzima kuwa mwongo
 
Sasa ni rasmi tunaelekea siasa za Ulaya na Marekani.

Siasa za maendeleo. Siasa za kistaarabu. Zile siasa za kitafutana kuuana, kutekana, kufungana na kufilisiana mali Mh Rais Samia ameona hazina tija kwa taifa.

Akiongea na Wasikilizaaji ktk Mtandao wa maongezi wa Club House Mh Makamu Mwenyekiti Chadema Tundu Antiphas Lissu ameungi mkono jambo zuri alilofanya Mh Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Chama hicho kuwa ni jambo jema.

Ni jambo jema kwa kuwa Rais ameachana na siasa za mitulinga. Tumefikia hatua hii kwa jasho na damu, tumelipa gharama hapa tulipofika " alisema kiongozi huyo.

Aliongeza kuwa Mbinu na mikakati iliyotumika kuishi wakati za awamu ya tano haiwezi kuzaa matunda wakati wa awamu ya sita kwani wakati huo tuliamua kubadilika kwa ajili ya Individual survival.

Jambo hili limeungwa mkono na wadau mbali mbali wa siasa na watanzania woote wakidai kuwa sasa tunaelekea Tanzania Mpya.

Wito kwa vyombo vingine vya serikali viige mfano mwema wa Rais Samia.

Wikendi njema

NB: Baada ya haya mliyoandika wenyewe bado mna mengine mmeficha au tuwapuuze?
 
Laana ya kushangilia kifo cha Magufuli itawatafuna milele Mbowe na Lisu.

Hata mwaka haujaisha saccos yao inakiona cha moto
Hahaha huwa nacheka sana hizo laana hewa mnazoziandika huku. Kwanza zinasishia hapa jf halaf haziend kwingine
 
Hawawezi kuwa sawa.

Mbowe ameonja uchungu wa uongozi hadi kasota jela miezi nane.

Lissu anaongea akiwa nje ya nchi, hana uhalisia wa chama.

Hata huo uongozi wa chama Lissu aachane nao
 
Kwa hiyo watu wakiwa na maoni tofauti ni ugomvi?!

Wacha ramli chonganishi
 
Back
Top Bottom