Raia Mwema: Mbowe na Lissu watofautiana kauli

Raia Mwema: Mbowe na Lissu watofautiana kauli

Kuna Watu wa Ajabu sana Nchi hii Wakati wa KESI ya KIJINGA ya UGAIDI kuna KUNDI la Watu WALIKUWA Wakipita MITAANI na KUPAYUKA ETI MBOWE ni GAIDI.

Baada ya MUNGU kuwaumbua Waneanza Tena ETI MBOWE na LISSU Hawaelewani Tunawashauri WAWAPATANISHE mbona ni kazi RAHISI TU.

Ila tunachowaambia kama Yule Aliyetumia na RISASI kutaka kuwaua Viongozi wa Chadema na Magereza kutaka Kuwafungwa ALISHINDWA basi CHADEMA HAIFI TENA

Kwa hiyo kwa mawazo yako cdm iko hai!!!?
😛 😛 😛
 
Polepole na mikopo pia kuna kutofautiana sasa kipya ni kipi kati ya Lissu na Mboye. Timu kujaza sifa imekwisha.
 
Mbowe alisema amechanja Corona woote tukamtukana...ila lile dikteta la chattle likajiua kwa ujinga wake wa kutaka sifa na kupenda kuabudiwa....Samia kaingia kachanja Corona...
Unafuatilia mwenendo wa korona duniani wewe?
-Ni asilimia ngapi ya waliochanja(worldwide) !?
-Matumizi ya barakoa, kunawa mikono na kukaa mbalimbali kukoje??

Baada ya kupata majibu jiulize
Maambukizi yanapanda au yanapungua??

Majibu utakayopata yatakupa picha kamili ya hao pua ndefu unaowaabudu na waliokulisha kinyesi kwamba JPM alikufa kwa korona.
 
Gazeti la Raia mwema toleo la leo limekuja na habari kuwa Mbowe na Lisu wametofautiana baada ya Mbowe kuachana na madai ya katiba mpya na kufuta join the chain ambayo ililenga kumchangia mamilioni ya pesa Lisu ili aendelee kutumbua maisha huko Ubelgiji.
Dah!!

Kama hii ni kweli,
Basi Tanzania hakuna mwanasiasa wa kweli.

Wengi ni wababaishaji.
 
Hawawezi kuwa sawa.

Mbowe ameonja uchungu wa uongozi hadi kasota jela miezi nane.

Lissu anaongea akiwa nje ya nchi, hana uhalisia wa chama.

Hata huo uongozi wa chama Lissu aachane nao
Mtahangaika sana kuokoteza mpaka vya kuota.
 
..wametofautiana wapi.

..Lissu kasema mwenyekiti hajakosea kwenda ikulu kumuona Raisi.

..pia amesema wanabadili mbinu kulingana na jinsi SSH anavyoendesha nchi.

..pia ktk kikao cha Bawacha ambacho Mbowe alihutubia kulifanyika zoezi la michango la join the chain.

..Sasa Mwenyekiti na Makamu wa chama wametofautiana ktk lipi?
 
Haikusaidii chochote kukubali kuendelea kuwa mjinga. Mbowe na Lissu Hakuna mahali popote walipotifautiana kauli.

Akiwa Iringa Mbowe aliwakabidhi BAWACHA jukumu la kuongoza Join The Chain Kwa kuwataka kuwa wa kwanza kuleta 1M contributors. Katika kikao hicho hicho akawataka Kwa Umoja wao kusimamia hamasa ya Katiba mpya na wao tayari kupitia Mwenyekiti wa BAWACHA aanaandaa mpangokazi naye kasema Wazi watapita mikoa yote. Alichoongeza Mbowe ni maridhiano na utayari serikali kuhusu uendeshaji wa siasa zisizo za visasi na uhasama.

Lissu kesho yake akiwa Club House akaja na dhana ya utashi wa Rais kuhusu Katiba mpya na mkamponda humu kuhusu kauli hiyo. Wengine Kwa maslahi yenu maana Tangu niwafahamu hamjawahi kuacha umbea mkasema CHADEMA Sasa imejisalimisha baada ya Mwenyekiti na Makamu wake kumtegemea Samia kuleta Katiba huku wakijua Huyo ni CCM na CCM haitaki Katiba mpya.
Sasa Leo mnapokuja na kutofautiana sijui mnakutoa wapi tena wakati Mwanzo mlisema wamesalender?

Mbali ya hayo haiwezekani Mbowe na Lissu wakawa na mawazo yanayofanana Kwa Kila kitu Kila siku. Ukiona hivyo ujue aidha kuna mmoja hafikirii au mmoja anafikiria Kwa niaba ya mwenzake.
Unajua huyo Wakudadavuwa kila jambo la Chadema huwa analichukulia negatively. Hivi kutofautiana mawazo ni jambo baya kwa chama chenye watu wanaotumia akili?
Chadema sio CCM ambako eti hata spika wa bunge anatoa mawazo yake kwa vile yako tofauti na mwenyekiti basi hata barua ya kujiuzulu wanamwandikia ili tuu afukuzwe hawamtaki.
Chadema iko imara sana kwa sasa kuliko wakati mwingine wowote
 
Sasa ni rasmi tunaelekea siasa za Ulaya na Marekani.

Siasa za maendeleo. Siasa za kistaarabu. Zile siasa za kitafutana kuuana, kutekana, kufungana na kufilisiana mali Mh Rais Samia ameona hazina tija kwa taifa.

Akiongea na Wasikilizaaji ktk Mtandao wa maongezi wa Club House Mh Makamu Mwenyekiti Chadema Tundu Antiphas Lissu ameungi mkono jambo zuri alilofanya Mh Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Chama hicho kuwa ni jambo jema.

Ni jambo jema kwa kuwa Rais ameachana na siasa za mitulinga. Tumefikia hatua hii kwa jasho na damu, tumelipa gharama hapa tulipofika " alisema kiongozi huyo.

Aliongeza kuwa Mbinu na mikakati iliyotumika kuishi wakati za awamu ya tano haiwezi kuzaa matunda wakati wa awamu ya sita kwani wakati huo tuliamua kubadilika kwa ajili ya Individual survival.

Jambo hili limeungwa mkono na wadau mbali mbali wa siasa na watanzania woote wakidai kuwa sasa tunaelekea Tanzania Mpya.

Wito kwa vyombo vingine vya serikali viige mfano mwema wa Rais Samia.

Wikendi njema

NB: Baada ya haya mliyoandika wenyewe bado mna mengine mmeficha au tuwapuuze?
Kuna maneno watu wanawawekea viongozi wa Chadema sijui wanayatoa wapi. Lissu huyu hapa.
 
Kule jela kawakuta na kuwaacha wangapi walikuwa na haki ya kutoka kama Mbowe ila hawajatoka?
Ayo ujibu mwenyewe ,jibu ni MOJA Mbowe hajatotoka KWa hisani ya mtu bali ulikua lazima kufanya hivyo binadam wote ni sawa ila sio sawasawa
 
Ayo ujibu mwenyewe ,jibu ni MOJA Mbowe hajatotoka KWa hisani ya mtu bali ulikua lazima kufanya hivyo binadam wote ni sawa ila sio sawasawa
Ndio ujue kwamba katoka kwa hisani kwa sababu kama sio hisani basi angendelea kusota kama wengine ambao hawajapata hisani.
 
Mkweli wa Mungu, Mimi sio CHADEMA Wala CCM ila niwaeleze tu ndugu zangu usije ukawaamini wanasiasa, kwasababu wao pia ni binadamu Wana madhaifu Yao hivyo mengi wao ni chumia tumbo tu hakuna lolote na mtaji wao ni wananchi wapuuzi, wajinga na maskiniaani Mimi nashangaa sana wewe mwenyewe mwanaCHADEMA huna maisha mazuri unaishi kwa tabu ,shida na madeni lakini unafanya kila uwezalo eti Mbowe au Lissu wachangiwe pesa sijui kwaajiri ya shughuri za chama sijui nini yaani ni upumbavu wa kiwaongo Cha juu sana.

Nilishasema na narudia tena sio Mbowe, Lissu, Samia au Zitto ndio wanaweza kukuletea maendeleo iyo ni big no maendeleo ya nchi hii yanahitaji wanachi wenye akili ambao hawataweza kumvumilia kiongozi wa namna yeyote Ile fisadi, mbazilifu, mng'ang'ania madaraka kwa muda mrefu bili matokea chanya yeyote ,Mpenda fedha na mwenye kujijali yeye mwenyewe na familia yake. Hapo ndipo viongozi watajiset na kuwa watu wakuwatumikia wananchi basi lakini sio hizi ngonjera za kipuuzi na kijinga za wao viongozi kugombania maslai Yao binafsi
debbug hiki ulichokiandika kilitakiwa kinapaswa kifunguliwe uzi wake umeongea point kubwa Sana Mwamba unatakiwa ujengewe sanamu pale Posta
 
Unajua huyo Wakudadavuwa kila jambo la Chadema huwa analichukulia negatively. Hivi kutofautiana mawazo ni jambo baya kwa chama chenye watu wanaotumia akili?
Chadema sio CCM ambako eti hata spika wa bunge anatoa mawazo yake kwa vile yako tofauti na mwenyekiti basi hata barua ya kujiuzulu wanamwandikia ili tuu afukuzwe hawamtaki.
Chadema iko imara sana kwa sasa kuliko wakati mwingine wowote
Kamanda jikite kwenye hoja.
 
Kamanda jikite kwenye hoja.
Acha kuwa mtu wa njozi na utabiri mangungu, subiri leo saa 3.30 usiku utazame StarTv pengine utapata akili kidogo kujua nini kinaendelea ndani ya Chadema
yerickonyerere-___CbALiOOr9IQ___-.jpg
 
Ndio ujue kwamba katoka kwa hisani kwa sababu kama sio hisani basi angendelea kusota kama wengine ambao hawajapata hisani.
Nimekwambia mkuu binadam wote ni sawa ila sio sawa sawa ,tumeshudia misamaha mbali mbali ya wafungwa kupitia marais tz ,lin umewaona wanatoka na kwenda Ikulu, ukiachana na babu sea,jiongeze mkuu Kesi ya Mbowe lilisha kuwa zigo kwao , vinginevyo siku zote wasingekua wanaangaika Kama kuku atakae kutaga, Nguvu ya Dunia, nguvu ya umma,nguvu ya Mawakili upande wa utetezi, nguvu ya Mungu imewanyoosha, na wamekoma kweli kweli
 
Nimekwambia mkuu binadam wote ni sawa ila sio sawa sawa ,tumeshudia misamaha mbali mbali ya wafungwa kupitia marais tz ,lin umewaona wanatoka na kwenda Ikulu, ukiachana na babu sea,jiongeze mkuu Kesi ya Mbowe lilisha kuwa zigo kwao , vinginevyo siku zote wasingekua wanaangaika Kama kuku atakae kutaga, Nguvu ya Dunia, nguvu ya umma,nguvu ya Mawakili upande wa utetezi, nguvu ya Mungu imewanyoosha, na wamekoma kweli kweli
Siwezi kukuzuia kuamini utakavyo mkuu, huo umma unaouzunguzia hatukuona nguvu yao yeyote wakati Lissu alipomiminiwa risasi mchana kweupe na hadi leo hakuna aliyekamatwa labda tuseme Lissu hakuwa mtu mzito wa kuamsha hiyo nguvu ya uuma.
 
Waungwana,

Hadi sasa kuna fukuto, tangu Mbowe asamehewe na Rais Samia kutoka jela hawana maelewano na Lissu. Kuna watu ndani ya Chadema mioyoni mwao walitamani Mbowe asitoke jela.

Muda unatuambia sasa.

Awali, hapa JF kulikuwa na hii thread - Kiongozi wa chama haelewani na yule kiongozi mwenzake, ugomvi ni mkubwa

View attachment 2147558
Huu ni mkakati maalum wa kumuandama mbowe kwa lengo la kudhoofisha nguvu ya chadema. Baada ya ile tamthilia ya ugaidi kugonga mwamba sasa wamekuja na mkakati mwingine. Kama kweli Rais na mwenyekiti wa chama tawala ana nia nzuri yakushirikiana na vyama vingine kujenga nchi angeanzia kwa kukemea vyombo vya dola na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa. Baada ya hapo aitishe kikao cha maridhiano kwa kushirikisha vyama vyote na viongozi wao na yeye ashiriki kama mwenyekiti wa chama badala ya kushiriki kama Rais. Lakini kitendo cha kuzungumza kwa nyakati tofauti na viongozi mmoja mmoja kutoka chama kimoja kuna kila dalili ya hujuma dhidi ya chama husikka.
Lakini kwa ukubwa wa akili ya mbowe hili nalo atalitatua na nguvu ya chama chake itaendelea kuwanyima usingizi chama tawala.
Kuna mifano mingi tu yakumdhoofisha mbowe binafsi na kukidhoofisha chama anacho kiongoza, lakini ukiangalia kwa jicho ambalo si la ushabiki utaona mbowe bado adi sasa hivi ni mshindi wa mikakati yote yakumdhoofisha yeye na chama chake.
 
Waungwana,

Hadi sasa kuna fukuto, tangu Mbowe asamehewe na Rais Samia kutoka jela hawana maelewano na Lissu. Kuna watu ndani ya Chadema mioyoni mwao walitamani Mbowe asitoke jela.

Muda unatuambia sasa.

Awali, hapa JF kulikuwa na hii thread - Kiongozi wa chama haelewani na yule kiongozi mwenzake, ugomvi ni mkubwa

View attachment 2147558
Nilifikiri kwa kukaa kwako bungeni kipindi cha kutosha basi ungeweza kuwa na ufahamu kuwa Rais hana mamlaka ya kumsamehe mtuhumiwa wa kesi yeyote bali anaweza kumsamehe mhalifu aliyehukumiwa tayari.
Kilichomtoa Mbowe ni DPP kuona hana misingi katika kesi yake hivyo kuiondoa mahakamani. Kaiondoa DPP au kaagizwa na Rais yote sawa maana sio msamaha.
 
Back
Top Bottom