Mwanamume mwenye umri wa miaka 56 kutoka Kenya amekamatwa nchini Zambia baada ya mamlaka kumhusisha na operesheni inayodaiwa kuhusisha uhalifu wa mtandaoni dhidi ya mifumo ya Serikali kuelekea Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo.
Wizara ya Mambo ya Ndani na Usalama wa Taifa ya Zambia ilitangaza Agosti 12, 2026 kuwa Mkenya huyo alikamatwa katika operesheni ya kiintelijensia iliyofanywa na kikosi cha pamoja cha vyombo vya ulinzi na usalama.
Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara hiyo, Mkenya huyo anayetajwa kwa jina la Michael Njuka, alikamatwa baada ya uchunguzi kubaini kuwa alidaiwa kupewa mkataba wa kufanya shughuli za kimtandao zilizolenga kuingilia mifumo muhimu ya Serikali wakati Zambia ikijiandaa kupiga kura Jumatano, Agosti 13, 2026.
Akizungumza katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari mjini Lusaka, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dickson Matembo, alisema Njuka alihusishwa na shughuli hizo za kimtandao, bila kutoa maelezo zaidi.
Kwa upande mwingine, vyombo vya usalama vilipata zaidi ya kwacha milioni 7.3 za Zambia, sawa na takribani Sh milioni 50.1 za Kenya, kutoka kwa watu wengine watatu; Japhen Mwakalombe, Mwila Kakana na Sensho Banda.
Watu hao wameitwa kutoa maelezo kuhusu chanzo na matumizi yaliyokusudiwa ya fedha hizo, lakini mawakili wao wamesema watajitokeza kwa ajili ya mahojiano baada ya Ijumaa, Agosti 14, 2026
Aidha, uchunguzi umebaini taarifa nyeti za kijasusi za kijeshi kwenye baadhi ya vifaa vya kielektroniki vilivyokamatwa kutoka kwa watu hao watatu, jambo lililozua wasiwasi zaidi kuhusu upatikanaji usioidhinishwa wa taarifa za siri.
Chanzo: Citizen Kenya
Soma pia Ni Hichilema vs. Mundubile uchaguzi mkuu Zambia
---------
My take
Huu mchezo mbona kama wameiga kutoka Tanzania, "Waliofanya vurugu ni kutoka nje", Wamelipwa kuvuruga uchaguzi!