Raia wa Kenya ni masikini kuliko Watanzania

Raia wa Kenya ni masikini kuliko Watanzania

Sasa waTz wangapi wana 30M? 😂
Mkuu watu wanahela ohooo hio 30m watu wanaingiza daily unaandika mataputapu hapa tena sio moja au wawili wengi tu


Yaani daah comment ya ki pumbavu sana hii 🤣🤣🤣
 
Mkuu unajua kwa nini iko hivi? Hii ni sababu ya ARDHI TU. Kenya ardhi ni ya mtu, mali yake, lakini TZ ardhi ni ya umaa. Hivyo lazima ujue ukiwa na ardhi hata kama ni ya umiliki wa hati, umiliki ya miaka 33, 66 au hata 99 inaonekana ardhi hiyo ni yako. Hivyo utaitumia kwa kilimo na kukuwezesha kupata kipato cha kutosheleza familia. Kenya ardhi walishauziana siku nyingi, hivyo kama babu ya babu yako hakuwa na ardhi yake mwenyewe basi wewe hautakuwa na ardhi asilani abadani na utaishia kuwa kibarua tuu. Ndio maana namheshimu Mwl. JKN kwa kuweka ardhi iwe ya Wananchi, kwa maana ARDHI NI MALI YA UMMA, maana hata BABU yangu hajasoma anamiliki ardhi kwa niaba ya Serikali. JKN hana wa kulinganisha naye.
Jkn hapa alicheza kama pele. Mimi babu yangu mzaa babu alikuwa anamiliki almost vijiji viwili na wote waliokuwa wanaishi mle wafanyakazi wake.
Ila ndio hvyo baada ya huo utaratibu ikabido waichukue hiyo ardhi na ndio wakapata ardhi ambao mpaka leo wanaimiliki.
Hili suala kuna wanaosema alifanya vibaya ila mimi naona ni suala zuri kabisa
 
Watanzania tunalalamika ufisadi

Kule Kenya ndo Kumejaa mafisadi plus

Hasa wanasiasa, sio upinzani au utawala

Kule Watu wanafisadi Hadi maji ya kunywa,

Familia moja inaweza zuia maji yote yanayotiririlka bondeni kwa ajili ya swimming pool au bustani ya maua yake

Afu familia bondeni zikafa kwa ukame na serikali isimfanye chochote maana katiba inamlinda.

SERA ZA KENYA ZA UMASKINI NI HOVYO KABISA
Kama
Kenyatta family
Moi family
Odinga family
Ruto family

Hao ndo wanalamba asali ya nchi kama sijui nn

Sema hamna self made billionaire sijui kwann asee
 
Kwenye kuagiza magari watanzania umetuonea Sana

Bado serikali yetu inaamini kumiliki Gari Ni anasa, Tunabambikwa Kodi zaidi ya 100% Bei halisi ya Gari

Kwa wakenya Gari Ni hitaji la msingi,
Kodi zao Ni rafiki Sana kwny magari

Ni Kama ilivyo kwa msumbiji au Zambia.

Msumbiji Wana uchumi mdogo
Ila Rolls Royce na Mercedes Utazikuata zimepaki uswahilini mazingira hata hayaeleweki
Acha basi msumbiji rolls royce zimepaki sehemu haxieleweki wakati Arusha hamna da aa hii noma asee
 
Kuna jamaa mkenya alikuwa anashangaa sana restaurants za huku zilivyo na mionekano mizuri, alikuwa anawashangaa hata mama ntilie wa huku pia kwani alikuwa akisema kwamba kule kenya restaurant tunazolia huku kule huwezi kuzipata na ukizipata basi gharama zipo juu sana imagine hawa wamama ntilie tunaowaona huku kwetu wanaouza vyakula 2000tsh kule kwao ukimpata kama huyo na ukupikie fresh food kama anachopika mmama wa hapa kule atauziwa bei ghali sana kwahiyo mara nyingi kule kwao watu wa hali hizi ambazo kwetu tunaita ni hali za kawaida kwao ni high levels.
 
Mkuu watu wanahela ohooo hio 30m watu wanaingiza daily unaandika mataputapu hapa tena sio moja au wawili wengi tu


Yaani daah comment ya ki pumbavu sana hii 🤣🤣🤣
Mtu akishaanza kutukana huwa nawaza nijibu comment au niache, sikia mi sina tatizo na mabishano yenu ya ukenya na UTz, swali langu kama waTz wapo wengi wenye 30M nini kinafanya wakenya wasiwepo wenye 1.7M? Kwamba huku kuna biashara nyingi na kubwa kuliko kenya! and why?

Na ni WaTz wangapi wanamiliki hizo 30M hata kwa asilimia ili tuone ni kwa jinsi gani tuko ahead of Kenya, speaking of kuiingiza kwa siku mbona wapo wanaingia zaidi ya hiyo na wala sio jibu la swali nililouliza.
 
Ndo mana
Ni ngumu sn kumkuta mtanzania anazamia Kenya kutafta maisha
Uzuri ni kwamba mimi naishi Karibu na mpaka. Tangu utotoni nimeona na kukutana na watanzania wengi waliokuja kutafuta maisha huku Kenya. Nikiwa mtoto, wazazi wangu waliwaajiri watanzania wengi sana kutuchungia ng'ombe enzi hizo. Hata hivi leo, watanzania wako wengi sana Kenya kikazi na kibiashara pia, wengine wanazungusha hadi bakuli kwenye mitaa na barabara zetu. Enda Nairobi, utakutana na wachaga wengi sana wakiuza viatu Gikomba. Sema tu hujui unachosema
 
Kwa wakenya,
Ni rahisi Sana kijana unapambana Hadi unazeeka, unakufa bila kumiliki ardhi

Na usipoweka mifumo thabiti,
Hadi kizazi chako Cha 10 mtafia nyumba za kupanga
DeepPond acha kupotosha jamani, sisi wakenya Ni wapambanaji Sana
 
Ni upuuuzi uliotukuka kujilinganisha n Kenya muda wooooooote.

Kenya wana pesa n mzunguko wao wa pesa ni mkubwa kuliko kwetu. Kenya walishajenga miundombinu n mazingira rafiki kuvutia wawekezaji wa kubwa wa kubwa kutoka pande zote za dunia, sisi ndio kwanzaa tunaanza. Kwa ufupi wa Kenya wapo mbali sana kiuchumi.

Ni aibu kujilinganisha n Kenya ukizingatia wa tanzania tuliiona fly over ya kwanza kwenye ardhi yetu nadhani 2017, mfugale fly over ilhali Kenya iliviona vyote tangu 2008-11. Ndio kwanzaa tumeanza kujenga kibaha highway yetu ilhali Kenya sasa walijenga yao enzi za kibaki.

Kwa ufupi Kenya wapo mbali sana kujilinganisha nao. Ila hili halimaanishi sisi pia tupo nyuma kwenye kila idara. Sifa n moja ya Tanzania ni wananchi wake wenye mioyo ya dhahabu. Wakenya ni makatili sana. Mtu akionekana anaiba kariakoo, 70% ukiskia 'mwizii basi kafa.

Kenya kila mtu ajitegemee. Kuibiwa mchanaaa mbele ya watu ni kawaida. Ukikutana n mtu sehemu yenye kiza Kenya basi ni lazima ujiandae kwa lolote maana watu usiku hawaaminiki.

Pia, pongezi kwa viongozi wetu kwa kutujengea kutujengea infrastructure za kisasa*barabara nadhifu ijapokuwa chache, stendi za mabasi zenye hadhi ya kimataifa kama gerezani, mbezi, mawasiliano nk vitu ambavyo Kenya hawana bus stands, zilizopo kipindi cha masika hazitofautiani na soko la mabibo, matope hatari~ country bus opposite *muthura Market, ile stand yenye iko besides TUK, penye magari za ongata n kite hukuwa.

Classic electric SGR. Tanzania tuna serekali ya kidikteta ambayo inatujali wananchi wake ukilinganisha na wakenya wanaoongozwa na magaidi ambao ukikaa mbele yao, kufa ni pap tu tofauti n sisi serikali yetu inawauwa mahasimu wake kwa ustaarabu kidogo, wachache sana.

Tanzania tuna mapolisi wakarimu, akiuwa wananchi anafungwa, Kenya polisi akinyooshea bunduki lala chini, ukikimbia marehemu. Kenya ugaidi umekithiri, sio kiivyo ila afadhali Tanzania majambazi tu wanajitafutia riziki.

Kwa ufupi Kenya ipo mbali sana kiuchumi. Sisi kimaisha tupo mbaali sana maana ijapokuwa tunapolekeshwa zoblezoble, ina wananchi wake tuna raha n unaishi kwa amani.

So nchi zote zima raha zake na shida zake. Kenya kwa starehe wapo next level, clubs zimejaa kubwa kubwa kama nyumba za wageni zilivyojaa Sinza, hadhi kulingana n mfuko wako. Ni vitu vichache ila ni uhalisia mtupu.
Kenya wana maisha magumu sana hasa raia wa kawaida, mkifuatilia maisha ya wakenya msiishie mijini......zama ndani ndani mtajua ukweli ni upi
 
Kenya wana maisha magumu sana hasa raia wa kawaida, mkifuatilia maisha ya wakenya msiishie mijini......zama ndani ndani mtajua ukweli ni upi
Ni kweli wakenya wengi wana maisha magumu na ni masikini lakini umasikini wetu haijafika hii level yenu
 
Nenda Kariakoo, kaulize mitaji ya watu wa pale. Achana na hapo nenda Iringa kwenye mashamba ya nyanya. Huko mbali, rudi Mwanza au kigoma kwa wamiliki Mitumbwi

Hiyo ni mifano michache kati ya Mingi ninayoijua, achana na nisiyoijua. Bongo wanaomiliki 30M ni wengi sana.

Hapo nimeongelea wafanyabiashara, sijaongelea wafanyakazi.
Achana nae huyo mil 30 pesa ndogo sana kwa mtu mwenye biashara hapa bongo. Nakutolea mfano tu nina rafik yangu mdogo tu ana miaka 28 ila saiv kafikisha milion 60 ktk account na nyumba yupo kwenye stage ya kupaua.

Mwezi ulioisha kanionesha salio Lake 61Milion. Anauza viazi t anafata mbeya analeta dar na hajashikwa mkono na mtu yoyote.

Kwahyo mil 30 watu wengi tu wanayo hapa bongo
 
Mkuu unajua kwa nini iko hivi? Hii ni sababu ya ARDHI TU. Kenya ardhi ni ya mtu, mali yake, lakini TZ ardhi ni ya umaa. Hivyo lazima ujue ukiwa na ardhi hata kama ni ya umiliki wa hati, umiliki ya miaka 33, 66 au hata 99 inaonekana ardhi hiyo ni yako. Hivyo utaitumia kwa kilimo na kukuwezesha kupata kipato cha kutosheleza familia. Kenya ardhi walishauziana siku nyingi, hivyo kama babu ya babu yako hakuwa na ardhi yake mwenyewe basi wewe hautakuwa na ardhi asilani abadani na utaishia kuwa kibarua tuu. Ndio maana namheshimu Mwl. JKN kwa kuweka ardhi iwe ya Wananchi, kwa maana ARDHI NI MALI YA UMMA, maana hata BABU yangu hajasoma anamiliki ardhi kwa niaba ya Serikali. JKN hana wa kulinganisha naye.
Kabisa aisee mfano hapa bongo vijana wengi tuna miliki ardhi. Respect kwake JKN
 
Kabisa aisee mfano hapa bongo vijana wengi tuna miliki ardhi. Respect kwake JKN
Kweli kabisa, hivi mlala hoi kama mimi namiliki ardhi Bongo, Mwanza hata kama kwa miaka 33 au 66 si eneo langu naliendeleza, maana shariti kubwa la kunyang'aywa ardhi ni kama HAUENDELEZI.
 
Mbaya zaidi ukiwakuta mtandaoni wanavyojitutumua sasa utachoka....ila kwa Africa Tanzania mwananchi wa kawaida ana maisha mazuri kuliko nchi nyingi.
Umeitembea Afrika wew au unalopoka tu kufurahisha Genge. Kwa Afrika hii nchi zenye quality ya maisha ukiondoa South Africa🇿🇦 Morocco🇲🇦 Botswana🇧🇼 na Egypt🇪🇬. Hizo nchi zingine zilizobaki zote ni chai tuu pamoja na Bongo yako🇹🇿 kuku wewe☹️☹️.
 
Umeitembea Afrika wew au unalopoka tu kufurahisha Genge. Kwa Afrika hii nchi zenye quality ya maisha ukiondoa South Africa🇿🇦 Morocco🇲🇦 Botswana🇧🇼 na Egypt🇪🇬. Hizo nchi zingine zilizobaki zote ni chai tuu pamoja na Bongo yako🇹🇿 kuku wewe☹️☹️.
Koma wewe usirudie kuniquote.
 
Back
Top Bottom