Raia wa Marekani wapiga kura kumchagua Rais mpya kati ya Donald Trump anayewania muhula wa pili au mpinzani wake Joe Biden

Trump kama Magufuli tu, ngwe ya pili is loading.
 
Sio marekani, ni wale watu 270 ndo wanateua raisi majority vote wala hazihesabiki! Hakuna uchaguzi maigizo kama wa marekani!
Inavyoonekana hata hauna uelewa mzuri kuhusu hizo electoral college votes. Hao hawateui tafuta vyanzo vya habari usome na kuelewa.
 
Jisemee nafsi yako wewe pamoja na wazazi wako na ukoo wako.
 
Kwa hiyo Marekani kuna vyama viwili tu vya siasa?
Marekani kuna vyama vingi vya siasa mbali na Democrat na Republicans.
Uchaguzi wa marekani mwaka 2020 una wagombea zaidi ya kumi toka vyama tofauti na hivyo viwili lakini pia marekani inaruhusu mgombea binafsi.

Hawa baadhi wagombea wa USA mwaka huu ukitoa Trump na Biden.
  1. Howie Hawkins wa chama cha Green Socialist
  2. Jo Jorgensen wa chama cha Libertarian
  3. Don Blankenship wa chama cha Constitution
  4. Brian T. Carroll wa chama cha American Solidarity.
  5. Roque De La Fuente wa chama cha American Delta Party
Kuhitimisha kuna wgombea 21 kwenye nafasi ya uraisi wa marekani, lakini sio majimbo yote hao wagombea watatokea kwenye ballots. Majimbo yatakayokuwa na wagombea wote ni Vermont na Colorado. Pitia hii linki Presidential candidates, 2020 - Ballotpedia kuelewa jinsi uchaguzi wa US unavyofanyika na pia kuwafahamu wagombea wengine.

Tunawajuwa Trump na Biden kwa sababu wanatoka kwenye vyama vikubwa na vikongwe nchini Marekani ila vyama vya siasa vipo vingi.
 
Ni sawa na ilivyo Zanzibar.

Vyama vikubwa ni viwili ila vyama vipo vingi ti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…