Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Baadhi ya watu wamekimbia nchi ili kuepuka chanjo ya corona
Baadhi ya watu wamekimbia nchi ili kuepuka chanjo ya coronaImage caption: Baadhi ya watu wamekimbia nchi ili kuepuka chanjo ya corona
Raia wa Rwanda na wakazi lazima wawe wamepewa chanjo kamili dhidi ya Covid ili kuruhusiwa kufika maeneo ya umma, taarifa iliyotolewa na Waziri Mkuu inasema. Amri ya kutotoka nje usiku itaanza saa sita usiku, na vilabu vya usiku na matamasha ya muziki yamepangwa kufunguliwa tena.
Takriban watu milioni saba kati ya milioni 13 wamechanjwa kikamilifu nchini Rwanda, wakati zaidi ya watu milioni nane wamepata chanjo ya kwanza.
Rwanda ni mojawapo nchi za Afrika zilizo na viwango vya juu vya watu waliochanjwa ikilinganishwa na idadi ya watu wake, na ya kwanza katika Afrika Mashariki.
Lakini uamuzi wa Jumatano usiku unamaanisha kuwa mamilioni ya watu bado wanahitaji kupata chanjoya pili ili kufikia maeneo ya umma.
Ingawa chanjo ni ya hiari, kumekuwa na ripoti za watu kupewa chanjo kwa lazima, na wengine wamekimbilia nchi jirani za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Burundi ili kuepuka chanjo.
Msemaji wa serikali alikiri kwa shirika la utangazaji la Ufaransa, RFI, kwamba baadhi ya mamlaka "zinaweza kuwa na bidii sana" katika kampeni zao lakini haikuwa sera ya serikali.
BBC swahili