Raia wa Zambia: Mwenge wa uhuru ni tunu ya Afrika, vijana tuungane kwa maendeleo

Raia wa Zambia: Mwenge wa uhuru ni tunu ya Afrika, vijana tuungane kwa maendeleo

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
1,194
Reaction score
911
Raia wa Zambia, ABRAHAM TAMBALAA aliyefika katika Manispaa ya Sumbawanga, Mkoa wa Rukwa, kuungana na Watanzania katika kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2026, amewataka Watanzania kuendelea kuulinda na kuuenzi Mwenge wa Uhuru akieleza kuwa ni tunu muhimu kwa Tanzania na bara la Afrika.

Amesema Mwenge wa Uhuru unabeba ujumbe wa umoja, mshikamano na maendeleo, akibainisha kuwa Tanzania ina utamaduni wa kipekee wa kuukimbiza Mwenge wa Uhuru ambao haupo katika nchi nyingi za Afrika, ikiwemo Zambia.

Aidha, amewahimiza vijana wa Tanzania kuungana, kushirikiana na kujikita katika shughuli za maendeleo, huku akiwataka kuepuka vitendo vya vurugu vinavyoweza kuhatarisha maendeleo yao binafsi na ustawi wa Taifa.
 
Rais wa Zambia Ibrahim Tambala??
 
Rais wa Zambia Ibrahim Tambala??
 
Back
Top Bottom