Raia wamekosa imani na magari ya serikali, ikibidi yasiwe tinted

Raia wamekosa imani na magari ya serikali, ikibidi yasiwe tinted

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
Kulikuwa na kimvua leo huku nilipo, likaja gari la serikali namba STN (lipo kama Hiace), vioo tinted likapaki karibu na tulipojificha mvua isitunyeshee. Aisee mara baada ya gari kupaki watu wote wakaitolea macho ile gari kuangalia nani anashuka.

Na wengine wakawa wanasema ni magari kama hayo yaliyokuwa yanatumika wakati wa rabsha za maandamano. Watu wanaangalia gari na kwa kutokea ikiwa watafanya lolote.

Hii imenionesha watu hawana imani kwa sasa na magari ya serikali. Nadhani ili kurudishe imani gari za serikali zisiwekewe tinted ili watu waone mambo yanayoendelea ndani.
 
Back
Top Bottom