Raila kawekwa na Uhuru kuvuruga biashara za Ruto, kasema Wakenya wagomee vifuatavyo

Raila kawekwa na Uhuru kuvuruga biashara za Ruto, kasema Wakenya wagomee vifuatavyo

mockers

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2013
Posts
12,843
Reaction score
35,442
Wakuu,

Sasa anaemsukuma huyu Odinga kufanya vurugu zote hizo ni Uhuru kenyatta na ndio mfadhili mkuu wa hiyo migogoro.

Kwanza lengo kubwa baadae serikali ya Ruto itumie nguvu ili hata asipotoka japo ndio lengo, mauaji yatakayosababishwa na polisi wapate upenyo wa kwenda Mahakama ya Makosa ya Kijinai ili Ruto asichomoke.

Raila kashauri Wakenya wagomee:
1. SAFARICOM
2. KCB
3. Star Newspaper

Kwenye hayo Wakenya wanayotakiwa kugomea huko Ruto na Gachagua wanamiliki hisa za kutosha. Kamwe hutosikia Raila anataja biashara za Kenyatta family kama;

1. CBA Bank
2. Brookside maziwa na bidhaa zake
3. Kameme FM
4. K24 TV

Hizo ni baadhi ya biashara za Kenyatta ukiacha mahoteli ya kitalii huko Mombasa, Lamu na Naivasha, wala shule ya hadhi ya watu wa juu Kenya peponi school wanakosoma matajiri, wala hutosikia kagusa kampuni za tours za Kenyatta, wala hatogusa majumba na maghorofa ya biashara ya Kenyatta family yeye lengo kila Ruto alipo na hisa wahakikishe biashara inakufa.

Msukumo wa hayo yote ni kuguswa kwa biashara za gesi zake Raila na Uhuru moja kwa moja kwa kuruhusu watu kama Taifa Gas kuingia Kenya hao macartels hawakupenda kabisa.

Hayo maandamano ya kila Jumatatu na Alhamisi ambayo hayana kikomo ni kuvuruga amani ya Kenya na biashara kwa ujumla, wale wanaoandamana wanaamini wanapiganiwa maskini kumbe watu wanapigania maslahi yao binafsi tu.

Hakuna mwanasiasa aliempigania maskini hiyo kwa Afrika hii sahau.
 
Huyo mzee kaona liwalo na liwe, kapoteza matumaini ya kuwa rais wa kenya kwa kipindi kijacho umri utakuwa umemtupa mkono
 
Mkuu nadhani wewe unaandika pasipo kufatilia,sababu kuu za hayo maandamano ni ingezeko la gharama za maisha hasa bei ya unga vilevile na ongezeko la bajeti ya ununuzi wa magari ya viongozi 4 Raid,Makamu,Ofisi ya Msalia Mdavadi na bajeti ya ununuzi wa magari ya Rais Mstaafu -Uhuru.
 
Mkuu nadhani wewe unaandika pasipo kufatilia,sababu kuu za hayo maandamano ni ingezeko la gharama za maisha hasa bei ya unga vilevile na ongezeko la bajeti ya ununuzi wa magari ya viongozi 4 Raid,Makamu,Ofisi ya Msalia Mdavadi na bajeti ya ununuzi wa magari ya Rais Mstaafu -Uhuru.

Motive ya maandamano sio gharama ya maisha, dunia nzima gharama zimepanda ni mfumo wa kidunia hakuna muujiza watafanya zishuke ndio maana Ruto anajikita kwenye production wazalishe chakula kwanza cha kutosha ili kukabiliana na hali, mfadhili mkubwa wa yanayoendelea ni uhuru kenyatta ndio mtoa pesa
 
Imekua Vita kubwa sana baada ya Rostam kuruhusiwa kufanya biashara ya gesi Kenya hizo mambo za kupanda gharama za maisha Mzee Odinga anazunguka tuu amechukizwa na kitendo cha Ruto kumruhusu Rostam ambae hawezi kushindana nae...ngoja tuendelee kuangalia boli likitambaa juu ya bahari..
 
Imekua Vita kubwa sana baada ya Rostam kuruhusiwa kufanya biashara ya gesi Kenya hizo mambo za kupanda gharama za maisha Mzee Odinga anazunguka tuu amechukizwa na kitendo cha Ruto kumruhusu Rostam ambae hawezi kushindana nae...ngoja tuendelee kuangalia boli likitambaa juu ya bahari..

Huo ndio ukweli wameona wamenyanganywa tonge mdomoni maana , biashara hiyo walikua wameodominate wao, wakenya wanatumika tu huoni sasa gharama za maisha kupanda ashaingiza na migomo ya biashara za akina Ruto ili kuwakomoa
 
Wakenya sio Watanzania miaka na miaka hata kabla Uhuru na Ruto hajawa Rais huwa wanaandamana vitu vikipanda bei.
Hiyo ndio raha ya kuwa na Wananchi walio elimika na kuelimika na wasio waoga.

Wewe hauwajui wakenya, maamuzi ya mahakama yao wanayapinga wao wenyewe, na mahakama iko kikatiba kabisa na waliihitaji ile mahakama kwenye katiba yao mpya,
 
Loser Raila anataka kufa bure.. Raila bado anaota ndoto, wakati mwenzake Ruto ni Rais wa Kenya, Rais huwezi mtisha
 
Mzee Raila anajaribu kuvuruga utawala wa Rutto kwa kila hali ikiwezekana hata kutumia maandamano kuyumbisha shughuli za uchumi.

bora aliukosa huo Urais, Mzee ni kivuruge kweli kweli anachotaka yeye ni madaraka tu.
 
Wakuu
Sasa anaemsukuma huyu Odinga kufanya vurugu zote hizo ni Uhuru kenyatta na ndio mfadhili mkuu wa hiyo migogoro.
Kwanza lengo kubwa baadae serikali ya Ruto itumie nguvu ili hata asipotoka japo ndio lengo mauaji yatakayosababishwa na polisi wapate upenyo wa kwenda mahakama ya makosa ya kijinai ili Ruto asichomoke.
Raila kashauri wakenya wagomee
1.SAFARICOM
2.KCB
3.Star Newspaper

Kwenye hayo wakenya wanayotakiwa kugomea huko Ruto na Gachagua wanamiliki hisa za kutosha.
Kamwe hutosikia Raila anataja biashara za Kenyatta family kama
1.CBA bank
2.Brookside maziwa na bidhaa zake
3. Kameme FM
4. K24 tv
Hizo ni baadhi ya biashara za kenyatta ukiacha mahoteli ya kitalii huko Mombasa, Lamu na Naivasha, wala shule ya hadhi ya watu wa juu kenya peponi school wanakosoma matajiri, wala hutosikia kagusa kampuni za tours za kenyatta, wala hatogusa majumba na maghorofa ya biashara ya kenyatta family yeye lengo kila Ruto alipo na hisa wahakikishe biashara inakufa.
Msukumo wa hayo yote ni kuguswa kwa biashara za gesi zake Raila na uhuru moja kwa moja kwa kuruhusu watu kama Taifa Gas kuingia kenya hao macartels hawakupenda kabisa,
Hayo maandamano ya kila jumatatu na alhamisi ambayo hayana kikomo ni kuvuruga amani ya Kenya na biashara kwa ujumla, wale wanaoandamana wanaamini wanapiganiwa maskini kumbe watu wanapigania maslahi yao binafsi tu,
Hakuna mwanasiasa aliempigania maskini hiyo kwa afrika hii sahau.
Kwanini ataje bidhaa za Kenyatta wakati naye ni raia tu?
 
Nashangaa wale wanaosema kuwa wakenya wako smart kwenye issue zao, msiishie mtandaoni, nendeni Kenya muone maisha halisi ya wakenya haswa vijijini. Kenya ni miongoni mwa mataifa yenye watu wa hovyo kuliko unavyoweza kudhani iwapo hujabahatika kuishi huko. Mkifika Kenya msiikomee mijini pata wasaa wa kuzama vijijini kwa muda wa kutosha
 
Huo ndio ukweli wameona wamenyanganywa tonge mdomoni maana , biashara hiyo walikua wameodominate wao, wakenya wanatumika tu huoni sasa gharama za maisha kupanda ashaingiza na migomo ya biashara za akina Ruto ili kuwakomoa
Mzee Odinga na Uhuru ndio walikua wanaongoza wameshindwa uchaguzi juzi tuu hapa waliwasaidia nini Wakenya sema Nchi zetu Serikali inapumbaza watu kwa kukosa Elimu bora ndio maana mtu mmoja akianzisha jambo la kijinga asiwepo wa kuhoji hawa Wakenya tunaoaminishwa wana Katiba na Elimu bora wanaingia kwenye mitego ya Wafanyabiashara bila kujijua...
 
Back
Top Bottom