Well said mkuu, sijui kwa nini baadhi ya members wanambeza Raila? Ukichunguza Waswahili wengi wanao msema vibaya Odinga utakuta ni wale wenye chuki binafsi dhidi ya JPJM!!!
Kila mtu mwenye akili timamu anajua Odinga alichezewa rafu katika uchaguzi huu, uthibitisho ni kuuwawa kwa Mkurugenzi Mkuu aliye kuwa ana simamia mission critical ICT system, mtambo huo ndiyo kila kitu, mtu akifanikiwa kuhu-hack ndio basi tena - Uhuru na kundi lake walijua sana ukweli huo, hivyo kuuwawa kwa msimamizi mkuu wa tehama hasa baada ya yeye kusema hakuna Mkenya yeyote anayeweza kuingilia system hiyo na kufanikiwa kuiba kura, aliongezea kwamba awezi kumwambia yoyote jinsi system hhiyo inavyo fanya kazi labda wamkate mkono ndio anaweza kutoa siri, sasa nini kilifuatia baada ya kutoa kauli hiyo kwenye Luninga - jamaa walituma mwanamke ambaye alikuwa rafiki yake wakawawekea mtego na kuwauua wote, hawakuishia hapo walimtesa na baadae kukata mkono wake - what does that tell you about matokeo ya uchaguzi tunao ushuhudia huko Kenya - kuna tatizo si bure.
Mimi nashangazwa sana kwa maoni ya waangalizi wa upigaji kura kutoka nje, kwa nini kuuwawa kwa mtu anaye simamamia roho/brain ya kutoa takwimu kamili ya upigaji kura naona waangalizi awakuchukulia tukio hilo ovu seriously - mimi nilitegemea wangesema kura zirudiwe kwa kutumia Sytem mpya yenye wasimamizi kutoka nje - hilo alikufanyika badala yake wanalazimisha Raila eti akubali kushindwa - hii inaleta picha gani kuhusu chaguzi barani Africa? Ni aibu tupu.