Raila Odinga issues a statement on the Supreme Court's decision.


Ahaa, nakuelewa ndugu. Lakini unafaa uelewe hivi, watu wengi walimpigia Kura Uhuru si kwa sababu wanampenda saana, ni kwa vile walikua hawamtaki Raila kamwe.

Raila ndiye andui yake mwenyewe number one, kama hangeitisha maandamano alivyofanya 2007 na watu wengi wakauawa, imagine huyu mtu alingojea watu 1300 wauawe huku yeye anangangania 'nusu mkate'. Alipopewe kipande chake basi, akaambia wafuasi wake watulie. Tena akakosea heshima wale wenzake waliomsaidia 2007 akina Ruto,Balala na wengine, nao wakamhepa.

Kama si siasa zake za chuki na mapropaganda, huyu Raila angepata Kura mingi sana katika ngome yake Uhuru huko Mt Kenya . Kama hangekosea Ruto na watu wa Riftvalley kwa matusi mingi, ange pate kura huko, lakini sasa........
 
Nchi za Afrika badio tuna safari ndefu sana katika safari yetu kuelekea kuwa nchi za Ki Demokrasia. Mahakama katika nchi zetu zimebaki kuwa 'mahakama za Kangaroo'. Mahakama zetu ni zenye kujali maslahi ya mtawala hususani pale panapohusiana na kesi za Ki Katiba kama vile Uchaguzi Mkuu wa Nchi wa Rais. Na ndio maana tumekuwa tukishuhudia watu wakisaka haki kwa njia za mitulinga badala ya kukaa pamoja mezani kutafuta suluhu kwa njia za kimahakama au ki diplomasia. Tumeshuhudia watu wakiingia barabarani/mtaani kutafuta haki zao mpaka ile waswahili wanasema 'kieleweke'.

Pamoja na madiliko makubwa ya mahakama ya Kenya kuwezeshwa bado imeonekana kuwa haijakuwa huru wala kuwa na ujasiri wa kudhubutu kama yenyewe ilivyo kuwa ikijinadi tena kwa kuhimiza kuwa shauri lipelekwe huko ili haki ipate kutendeka. Kwa wale mliokuwa mnafutilia shauri hili pale lilipoanza tu Rais wa Mahakama alitoa kauli kuwa anaomba wale walioleta shauri wawe tayari kwa uamuzi wowote hata ule ambao hautawafurahisha. Kauli ile peke yake ilikuwa na utata mkubwa. Wengi walitolea maoni kuwa na kubashiri kuwa uamuzi utakuwa na nguvu ya kisiasa zaidi kuliko kutimiza haki hata kama Majaji wanaiona haki hiyo. Hivyo kwa kifupi mahakama imeamua kesi hii kwa maslahi ya kisiasa zaidi. Kwa maneno mengine ni kuwa Mahakama imetishika baada ya 'kutishiwa nyau' kupitia ile slogan ya kuwa 'nchi itatumbukia kwenye dibwi la vurugu na umwagaji wa damu endapo uamuzi ungekuwa kutengua ushindi wa kinya ama kuarisha marudio ya duru ya pili kwa kuwa kura za UK hazikutosha katika duru ya kwanza. Mahakama imefanya exactly yule lawyer (msomali) wa IEBC alivyodai wakati akifunga hoja zake (kwa kutisha majaji) kuwa nchi itaingia katika vurugu, uchumi utayumba na thamani ya shilingi kuzidi kudolora na sabu kedekede za vitisho. Na akahitimisha kuwa mahakama na majaji wake wawe tayari kubeba mzigo wa lawama.

Kwa Mahakama kufanya maamuzi ya kisiasa badala ya Ki katiba kuna hatari kubwa. Kwa huko mbele ya safari napata mashaka kama vyama vitadhubutu kupeleka kesi nyingine kama hii. Kenya inaweza kurudi tena nyuma kwani mambo yatakuwa kama yale yale ya 2007. Kesi za uchaguzi wa Rais zitaishia kuamuliwa kimabavu mitaani. Kwani mahakamani imewaangusha wale wanaoamua kudai haki zao kwa taratibu za Ki Katiba. Kwa jinsi zoezi zima lilivyokwenda inaonyesha kuwa bado ni rahisi kushinda uchaguzi kwa njia za mkato na bado ukaweza kushinda kwa hoja za kutishia "kuvunjika kwa amani" na mwisho wa siku ushindi wako wa mashaka (mkato) kutakaswa (barikiwa) na msimamzi mkuu wa haki ambayo ni mahakama.

Hivyo kwa Afrika safari ya kuelekea nchi ya demokrasia kamili bado ni ndefu na ina kitambo kirefu.
 
mi simpendi uhuru kiukweli !
Ukiniuliza sababu sina!
Simpendi tu!
Kama ambavyo sina sababu ya kuichukia barcelona.
pole ww utakuwa cdm mrudie mungu wako kwani kumchukia mtu bila sababu ni kwamba unamchukia aliyemuumba
 
kwa wale wenye uelewa wa mambo ya kisiasa kidogo,na kuweka ukabila na ushabiki pembeni,watakubaliana na mimi kwamba odinga ameitendea haki kenya kupigania mabadiliko mengi ya kisiasa. harakati zake hazijaanza leo wala jana,yeye pamoja na wanaharakati wengine wa mabadiliko wamepigania katiba mpya ambayo leo wakenya wanajivunia,katiba iliyotoa mwanya wa kuundwa kwa vyama kama TAN,ODM,URP nk leo hii kenya ina mfumo wa maseneta,gavana kutokana na katiba hii hii waliokuwa wanaipinga wakina uhuruto,leo hii wameungana makabila mawili na kupinga chochote asemacho odinga,kisa eti sio kabilal lao.ukisoma magazeti ya yao( bahati nzuri majina yao yanaonyesha wazi watanoka kabila gani) hakuna hata mmoja anaye japo kwa mbali kumpa kudos odinga kwa yote aliyoyafanya. ukisoma different blogs za kwao,coments zinaonyesha wazi wazi uchaguzi huu umewagawa kitabaka sana wakenya,wakikuyu wanaona wao ndio the choosen tribe,wakalenjin wanaona baada ya uhuru, Ruto ndie next prezo.nadiriki kusema kwamba serikali ya jubilee inaitaji nguvu kubwa ku heal na kuwaunganisha wakenya tena.ebu angalia bunge,maspika wote wawili.kulikuwa na haja gani ya kumtoa marende,ila wamemuondoa kwa sababu alikuwa anatokea ODM bunge lililopita,japo alifanya kazi nzuri sana. ukabila utawatafuna sana wakenya ngoja tusubiri baraza a mawaziri tuone itakuwaje.
 
Ni kweli mkuu,wametikishika na kudorora kwa uchumi na vurugu,kwa upande mwingine wa shilingi lazima tujiulize ,kwa nini vurugu zitokee kwani ni lazima awe uhutu tu?
kusema kweli hii kesi mahakama imewalet down wakenya,hii kesi ingeamuliwa uchaguzi urudiwe,ingekuwa ni fundisho kwa viongozi wanaoingia madarakani kwa njia za udanganyifu.
 
Raila is a failed politician aende zake akapumzike aleee wajukuu kama anao..uraisi ndo basi tena ..labda awe rais wa bendi kama akudo au nanyuki jazz band
 
kumbuka raila alikubali nusu mkate baada ya jopo la wasuluhishi kumuomba aiokoe kenya kwa kukubali yaishe,coment yako imejaa ukabila na kutokuona mbali.kosa la raila kwa ruto ni lipi?
Ruto alitaka apewe dpm docket, raila akampa Mdv,hapo ruto kwa kushirikiana na wakikuyu wakaanza kumsaliti odinga.
angalia ishu ya MAU forest ilivyogeuzwa kisiasa na kuiweka eti odinga hawapendi kalenjins,wakati lile lilikuwa for the benefit of the country at large
 
...hapa umenishangaza sana, ulitegemea vipi eti Wabunge ambao majority ni wa Jubilee eti wamchague Spika toka chama pinzani cha CORD?kumbuka kwenye uchaguzi huu Jubilee ina Serikali na ina majority kwenye mabunge yote mawili, kama hii sio ishara ya imani kuwa majority ya Wakenya wameichagua Jubilee sijui mpate ishara gani zaidi...
 
kwako anaweza kuwa amefeli kisiasa,lakini kwa wale wanao ona mbali na kukumbuka ya jana wanamuona HERO.coment kama hii haiwezi kutolewa na mtu mzima hata kama anamchukia odinga,maneno yetu yana reflect umri na the type of people we are.naona wewe ni moja kati wale wa vijana wanao ongozwa na mihemko ya kisiasa.
hold on your horses waweza kujikut unaongea pumba mbele ya watu.kwani kutochaguliwa ndio inamaana uwezi kuongoza? kwani kiongozi wa akudo an mapungufu gani? kijana nakushauri uchague forum kam vipi unaweza enda fb,kule kuna watu kama wewe wengi tu.
 
Hao kwa kifupi isha kula kwao, na huyo Kalonzo ndo kabisa, anapotea kwenye Dunia ya Siasa, Ila siasa ndo zilivyo nazania Joseph Stalini wa Iliyo kuwa USSR aliongelea vizuri sana kwenye hili,

Naunga mkono hoja hapo kwenye red!!! Hii ndivyo hali ya demokrasia iko katika nchi nyingi za kidikiteta au zenye ukoloni mamboleo (nyingi zikiwa katika bara la Afrika)!!!

View attachment 88687
 
Kenya itabidi warudie uchaguziwa Rais in a year's time kwani Uhuru na Ruto watakuwa wameisha hukumiwa kifungo huko Hague!!! Kukataliwa kwao kusikiliza kesi yao kwa mtandao ni ishara tosha kuwa wanatakiwa waende Hague in person ili hukumu ikitolewa waende lupango!!
 

Ulichosema na mimi ndiyo nimekuwa nakisema. Ila kuna wapumbavu humu waliolewa kool-aid ya Uhuru ambao hawawezi kuelewa.

Wana-heap praise kwa Kenya kutuzidi Tanzania hususan kwenye haya mambo ya kisiasa ila wanasahau wanaharakati waliojitoa mhanga kuhakikisha hiyo nchi inafika hapo ilipo na kwenda mbele zaidi.

Unazi bila akili mbaya kuliko UKIMWI!
 

Afadhali mumesema nyie mazee!
 
Inabidi tu tuuseme ukweli bana.

Mchango wa Raila kwenye mageuzi ya Kenya ni mkubwa sana kuliko mchango wa Uhuru.

Au naongopa mzee mwenzangu?

Raila amechangia hadi mafanikio madogo ya Uhuru na Ruto....
hata hiyo Supreme court kaichangia uwepo wake...
Bila Raila hata TNA maybe isingekuwepo labda leo Rais angekuwa Gideon Moi
 
We can outsource Raila to Tz if u guys feel for him that much. Aliyesema mambo ya mau forest ajaribu kutafuta clip za siasa za hiyo ishu pre 2
007 na atapata jibu. We are wise enough to see beyond veiled threats and propaganda. I challenge any of you atafute kanda za kampeni 2013 za cord atwambie healing aina gani ingetoka kwa hiyo group.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…