Kiambu mafia
Member
- Mar 26, 2013
- 43
- 10
Kenya - Kenyata nami sikupenda sana lakini Wakenya wameamua. sikupenda hasa kwa mawazo yangu kuwa ule ukoo ulishatawala na kujikusanyia mali kemkem hivyo usiendelee na kufamya mfano wa ufalme. Kuna uwezekano Uhuru kabebwa na historia ya anakotokea na si kwa sababu yeye kazidi wenzake kwa ubora. kwa msingi huo ukigombea na mtu wa aina hiyo inakuwavigumu kupita hilo tu! sina chuki na Uhuru
Ahaa, nakuelewa ndugu. Lakini unafaa uelewe hivi, watu wengi walimpigia Kura Uhuru si kwa sababu wanampenda saana, ni kwa vile walikua hawamtaki Raila kamwe.
Raila ndiye andui yake mwenyewe number one, kama hangeitisha maandamano alivyofanya 2007 na watu wengi wakauawa, imagine huyu mtu alingojea watu 1300 wauawe huku yeye anangangania 'nusu mkate'. Alipopewe kipande chake basi, akaambia wafuasi wake watulie. Tena akakosea heshima wale wenzake waliomsaidia 2007 akina Ruto,Balala na wengine, nao wakamhepa.
Kama si siasa zake za chuki na mapropaganda, huyu Raila angepata Kura mingi sana katika ngome yake Uhuru huko Mt Kenya . Kama hangekosea Ruto na watu wa Riftvalley kwa matusi mingi, ange pate kura huko, lakini sasa........