Raila Odinga: Nilikwenda Zanzibar kuondoa mshtuko wa kupoteza Uchaguzi

Raila Odinga: Nilikwenda Zanzibar kuondoa mshtuko wa kupoteza Uchaguzi

Mwenzako kashindwa uchaguzi kaenda Zanzibar kucheza na Kobe wewe mwananchi wa kawaida unaingia barabarani kuandamana unachezea Rungu za kutosha😁
 
View attachment 2357892

Aliyekuwa Mgombea Urais wa Azimio la Umoja Raila Odinga alieleza kwamba alisafiri kwenda Zanzibar pamoja na familia yake yote ili kupata nafuu baada ya kushindwa Uchaguzi wa Agosti 9, 2022.

Waziri Mkuu huyo wa zamani alibainisha kuwa safari ya nje ya nchi ilikuwa muhimu kuwezesha familia yake kupata nafuu kutokana na mshtuko wa kupoteza uchaguzi.

Raila amezungumza wakati wa hafla ya kuapishwa kwa Gavana wa Mombasa Abdulswamad Nassir mnamo Alhamisi, Septemba 15.

"Nilienda kufanya mazoezi Zanzibar. Nilimtoa mke wangu, watoto na wajukuu wangu kutokana na mshtuko walioupata. Nimerudi asubuhi ya leo kutoka Zanzibar, sikuweza kuwa nanyi wakati wa kuapishwa (kwa Abdulswamad), lakini niko hapa," Raila alisema.

Kabla ya kuapishwa kwa William Ruto kuwa Rais, Raila alitoa taarifa iliyoashiria kuwa atakosa hafla hiyo kwa vile alikuwa amesafiri nje ya nchi.
Kuunga mkono udikteta wa jiwe kumekuponza , Mungu hataniwi
 
Back
Top Bottom