Hawajui vizuri
Afu ifike mahali tuache kujilanganisha na nchi za wazungu, ni mbingu na ardhi, juzi Kuna mtu nilikua naongea nae yaani police service ya kwetu kuja kufanana na nchi kama USA itachukua miaka 200 Mungu akitusaidia aisee
Kule police wote wana body cameras Kila uwapo kazini unachofanya kinaenda kwenye server! Ole wako uzingue sasa, Kila kitu kinarekodiwa, hii inasababisha wawe waadilifu, ishu ya kumpiga mtu bila sababu za lazima usijaribu utanyea ndoo
Kama haupo kazini huruhusiwi kufanya arrest na shughuli zingine za kiofisi(labda iwe emergency) kiufupi policy Yao inataka ufanye kazi ukiwa na body camera inayorekodi matukio yote
Kuna polisi walienda kufanya eviction mahali walivyo wajinga wakawa wanaiba sijui saa,sijui Nini aisee washafukuzwa kazi na sa ivi kesi ipo mahakamani ni mwendo wa kula mvua tu, huku bongo polisi wakikupiga ambush wakikusachi kama una Mali ni halali Yao, watu wanapekuliwa bila search warrant huku, wenzetu ukimpekua mtu bila warrant hata ukimkuta na Nini ushajichanganya huwezi kumshinda
Niliona clip Moja jamaa kamsimamisha mtu anahisi anaendesha huku kalewa, kufungua mlango anakuta ni bosi wake, jamaa akamkomalia kibishi bosi akawa anamuomba let it go am your captain jamaa akakomaa nafanya kazi yangu, mwisho wa siku yule captain alifukuzwa kwa madai alitaka kutumia madaraka yake vibaya
Sasa huku kwetu unaweza mkomalia mkubwa wako, never!! Bado tuna safari ndefu kwenye kupata haki, bongo ukiingia polisi hata kama Huna kosa huwezi kutoka mikono mitupu