Raila Odinga: Polisi wa Tanzania kama Ulaya. Adai wanaweza kusubiri umalize kazi zako ndio wakukamate

Raila Odinga: Polisi wa Tanzania kama Ulaya. Adai wanaweza kusubiri umalize kazi zako ndio wakukamate

Mwanasiasa mkongwe wa Kenya, Raila Odinga anasema kuwa polisi wa Tanzania wanapitia kwenye mafunzo ya kufundishwa utu kwa wananchi hata wakitaka kuja kukukamata lazima waombe Kwanza na wakikuta upo na kazi watakusubiri mpaka umalize ndipo wakuchukue...
Angejua
 
Mwanasiasa mkongwe wa Kenya, Raila Odinga anasema kuwa polisi wa Tanzania wanapitia kwenye mafunzo ya kufundishwa utu kwa wananchi...
Hahahaha 😅😂🤣😭
Aiseee!

Aje kuishi hapa kama sisi. Awe wa kawaida. Aandamane, akutwe na kesi za kubambikwa. Hapo tutamuelewa. Au akutwe na madini yenye thamani. Atajuta..
 
Wako peace sana ase, ilishawahi kunitokea ishu moja tumegombana na mtu ghafla kama nusu saa hivi naona bajaji ipo nje kwangu wakashuka na walijitambulisha vizuri kwa kuonesha ID zao kila mmoja...
.
Screenshot_20230224-102948.jpg
 
Kama mtu alishaishi Kenya haswa na kufahamu vizuri nafikiri atakubali kuwa polisi wa Kenya daaah sijui niseme Nini, actually ukiingia anga zao utajuta kwanini ulizaliwa, wengi siyo friendly kabisa...huku Hadi unatukanana na polisi kabisa.
 
Mwanasiasa mkongwe wa Kenya, Raila Odinga anasema kuwa polisi wa Tanzania wanapitia kwenye mafunzo ya kufundishwa utu kwa wananchi hata wakitaka kuja kukukamata lazima waombe Kwanza na wakikuta upo na kazi watakusubiri mpaka umalize ndipo wakuchukue...
Siku akiwakuta wamepewa oda wa CCM!!
 
Sawa ni sawa na wa ulaya. Je wanaweza kulinda mashabiki wa mpira uwanjani bila kugeuza shingo kuangalia mtanange kwenye pichi?

Ukute polisi wenyewe ni mashabiki wa simba na yanga au timu zao za polisi. Hawa polisi wetu huwa wanaangalia mpira badala ya kuangalia mashabiki
 
Ni kweli, niliwahi ibiwa nyumbani upangajini nika msearch askari ambae tulipanga mpaka mfukoni ananiangalia tu.
 
Msimshangae Odinga, inawezekana kuna ukweli fulani. Kwenye kesi ndogo ndogo wanaweza kukuvumilia tu.

Kwani tumesahau udhaifu wa polisi wetu? Matatizo yao hayapo katika kukamata watuhumiwa hasa wenye kesi ndogondogo. Matatizo yao ni rushwa, wizi, ujambazi na kubambikiana kesi.
 
Katika kuwaponda Polisi wa Kenya kuelekea siku ya Maandamano Makubwa yanayoendelea, Mh Raila Odinga amedai kwamba Polisi wa Tanzania ni waungwana na werevu kama Polisi wa Ulaya na kwamba wakitaka kukukamata wanasema "NDUGU TUNAOMBA TUKUKAMATE"

Hivi kweli jamani hiki alichokisema Odinga ndicho wanachofanya Polisi wa Tanzania?

Toa maoni yako.
 
Back
Top Bottom