Raila Odinga: Polisi wa Tanzania kama Ulaya. Adai wanaweza kusubiri umalize kazi zako ndio wakukamate

Raila Odinga: Polisi wa Tanzania kama Ulaya. Adai wanaweza kusubiri umalize kazi zako ndio wakukamate

By the way...yuko sahihi kabisa..

Ukitii sheria bila shuruti ...unafika mpaka kituoni pasipo kufungwa hata pingu...

Shida inakuja pale unapokaidi tu...na kuwaonyesha kiburi.

Mbona liko wazi kabisa hili.
 
Anaongelea polisi wa Tanzania upande wa Zanzibar.

Ni waungwana Hasa,

Kama huamini nenda kule, likitokea la Kutokea,

Polisi akija atakuomba ukimaliza KAZI zako uende kwenye we kituo Cha polisi wewe mwenyewe.

Kenya si Tanzania unapishana na police karibu, kule polisi na raia ni ni mbalimbali.
 
Mwanasiasa mkongwe wa Kenya, Raila Odinga anasema kuwa polisi wa Tanzania wanapitia kwenye mafunzo ya kufundishwa utu kwa wananchi hata wakitaka kuja kukukamata lazima waombe Kwanza na wakikuta upo na kazi watakusubiri mpaka umalize ndipo wakuchukue.

Polisi wa Tanzania ni Kama wa YUlaya.

Naomba kuwasilishaa.....

Wanasiasa ni hatari SANA
Unafiki mwingi
 
Mwambie huyo jamaa asituchefue, polisi walienda kusachi kwenye getho la Dereva bajaji kisa anasadikika alikodiwa kubeba mali ya uwizi wakakuta jamaa ana ki akiba chake cha elfu70 washenzi wakapita nacho, Sasa hao polisi au wezi tu
 
Mwamba sijui alifanya nini mpaka akabananishwa hivyo

Ni kama yaliyowakuta kina Adamoo, Ling'wenya au kina Lijenje tu.

Fr_7Zw0WcAAavRN.jpeg


Wenye nchi kuwa walamba asali, wahuni au vijana wa hovyo hayo ndiyo matokeo yake hayo.
 
Wako peace sana ase, ilishawahi kunitokea ishu moja tumegombana na mtu ghafla kama nusu saa hivi naona bajaji ipo nje kwangu wakashuka na walijitambulisha vizuri kwa kuonesha ID zao kila mmoja.

Next wakanambia tunakuhitaji kituo cha polisi kwaajili ya kutoa msaada wa maelezo, nilipochungulia ndani ya bajaji nikamuona mke wangu. Nikamuuliza mke wangu "umeumia sana kiasi utahitaji uchunguzi wa kitabibu?" akanijibu "hapana naweza kwenda hata asubuhi".

Basi bwana nikawaambia wale jamaa naomba nilipe tu nauli ya bajaji ila nitakuja nikishampeleka mke wangu hosptali, wakaniambia nilipe nauli elfu tano wakarudi zao na kesho yake saa nane mchana nikaenda tukayamaliza.
Aise
 
Mwambie huyo jamaa asituchefue, polisi walienda kusachi kwenye getho la Dereva bajaji kisa anasadikika alikodiwa kubeba mali ya uwizi wakakuta jamaa ana ki akiba chake cha elfu70 washenzi wakapita nacho, Sasa hao polisi au wezi tu
Hahahaa njaa tu
 
Japo kuna kaukweli, polisi wa Kenya makatili sana, rushwa kwa kwenda mbele, wa Tanzania hata kama wala rushwa ila utahisi kuna utu wa kiaina.
Weeee, hujaingia kwenye 18 zao, polisi afrika ni KERO kwa raia
 
Nafikiri kwa wale waliozunguka East Africa, Msumbiji, DRC na Zambia watapata picha kweli police wa Tanzania ni waungwana.

Uzuri wao, wanapotaka kukukamata unaweza ukawahoji na wakakupa majibu.

Sio hivyo kwa nchi nyingi, ni uhasama mbele kwa mbele.
 
Back
Top Bottom