Raila visits Mombasa and claims he won the election!!!

Raila visits Mombasa and claims he won the election!!!

Du dingi sasa huko anakoendelea siko. Naona litakuja kuwa zari la kufa mtu hapa, Odinga akimwangwa mahakamani. Mimi ningeshauri wakiitisha kuandamana mwacheni aandamane kwa amani. Mkituma polisi tu hapo wazungu lazima watakuja kuweka no-fly zone.

Sio watakuja, Waingereza wana Military base kubwa tu Kenya tangu siku nyingi, na tayari kuna wanajeshi kibao washamwagwa, hivyo huyo Bw. Odinga anajua anchokifanya, wewe utasikia tu!
 
Sio watakuja, Waingereza wana Military base kubwa tu Kenya tangu siku nyingi, na tayari kuna wanajeshi kibao washamwagwa, hivyo huyo Bw. Odinga anajua anchokifanya, wewe utasikia tu!

Tena ingekuwa vyema akiitisha maandamano, polisi wasionekane kabisa kwenye maandamano, kitu kizuri ni kuyaonyesha maandamano hayo live kwenye TV. Ili waone fujo zitaanzishwa na akina nani. Lakini wakipeleka polisi tu hapo kwisha kazi, Uhuru na Ruto watajikuta wanakamatwa kama panya kama walivyomkamata Gbabo ama Gadaffi.
 
Odinga hajashindwa kwenye uchaguzi.wewe unayejidanganya kashindwa ujue unamwandalia njia ya kwenda ikulu.huyu bwana ni so bright>wakenya wamekariri kuwa waongozwe na wakikuyu na wakalenjini na ndo sababu kura huwa zinaibwa.
 
Kama wakenya wamekariri hivyo ni uthibitisho tosha kua RAO alishindwa kihalali maana hao hao waliokariri ndo wapiga kura, labda kama kuna wapiga kura ambao siyo wakenya ndo atashinda RAO.
 
Odinga ni mleta fujo kivipi haswa?

Mijizi ya kura kama Kibaki na Kikuyu allies wake ndo waleta fujo.

Jitu limeiba kura na bila hata simile linaenda kuapishwa uani.

How low can one get than that?

Huyo aliyeapishwa uwani Raila alimkubali ndio maana akawa Waziri Mkuu wake, ww ni nani kupinga? Na isitoshe hiyo ni historia tuzungumzie kilchopo mbele yetu.

Mlikuwa mnapiga kelele ana haki ya kwenda mahakamani sawa amekwenda sasa hizi chokochoko za mitaani za nini? kwa nini asisubiri uamuzi wa mahakama? Hichi anachokitafuta ni kuleta fujo ndani ya nchi!! kilichobaki sasa ni kutandikwa tu! na safari hii atatandikwa kwelikweli ili mpate ya kusema vizuri kwani ndicho mnachokitafuta!!!!!!!!!!!
 
Acheni uzushi. Raila hajaanzisha wala kuhamasisha vurugu mitaani.

Hata kama hamumpendi kutokana na biases zenu si vyema kumzulia mambo mtu ambayo hajayafanya.

From the jump kwenye hii election cycle amekuwa akihubiri amani.
 
Mkuu with all due respect, mtu anasimama jukwaani anatangaza kushinda uchaguzi wakati vyombo vilivyopewa jukumu hilo vinasema tofauti hiyo ni nini kama sio kuitisha vurugu?

Wote walikubaliana tokea mwanzo kama hujaridhika nenda mahakamani- sasa kwa nini mahakama isiachiwe itoe maamuzi yake kwanza?

Kwa hali ya siasa za kenya zilivyo kutoa kauli anazotoa Raila hivi sasa ni sawa na kuchezea kibiriti kwenye petroli, moto ukilipuka hakutakuwa na mwingine wa kulaumiwa zaidi yake!!
 
Freedom to air one's opinion is a civil liberty. Raila was doing just that.

And, in keeping with his promise, he has gone to court to fight the declared results.

Every petitioner who goes to court thinks he is right. Otherwise why would anyone go to court thinking that he is not right?

That would be silly and stupid.

Raila is well within his rights by holding and expressing his opinion that he thinks he won.
 
KWANIA NJEMA TUU, AISUBIRI MAHAKAMA ANAYOITEGEMEA IAMUE.
ni lini wagombea uraisi wa KIafrika watapata ufahamu kila uchaguzi una "SHINDA au SHINDWA"
 
Siasa bana we acha tu. Tusubiri maamuzi ya Mahakama. Lakini kama kulikuwa na irregularities Jaji Mutunga mtamsikia maamuzi atakayotoa.
 
Mbona katika kesi hajasema kuwa alishinda.

Raila ana mapungufu.
 
[h=2]Wednesday, March 20, 2013[/h][h=3][/h]

Waziri Mkuu Raila Odinga

Mombasa.
Waziri Mkuu Raila Odinga Jumatatu alidai kwamba muungano wake wa Cord ulishinda uchaguzi wa Machi 4 kwa kupata kura 5.7 milioni dhidi ya zile za muungano wa Jubilee ulioongozwa na Uhuru Kenyatta 4.5 milioni.

Alidai kwamba uchaguzi huo ulikuwa na udanganyifu mkubwa kuliko ule wa mwaka wa 2007 ambao pia alidai alishinda kwa kura 60,000 mbele ya zile za Rais Mwai Kibaki.

Akiwahutubia wafuasi wa Cord waliokuwa na furaha maeneo ya Hola Changamwe mjini Mombasa Odinga alisema Wakenya wameamua kwamba haki yao watailinda. Akitoa mfano wa busara ya mfalme Solomon kwenye Biblia ambaye alitoa hukumu kwamba, mtoto mchanga atakwe na kila mmoja wa wanawake wawili waliokuwa wakizozana juu yake atwae nusu ya mwili, Odinga alisema wakati huu haiwezekani kuendeleza dhuluma.

“Mfalme Solomon aliamua kwamba mtoto akatwe katikati na akina mama wawili waliokuwa wakizozana kila mmoja achukue nusu. Lakini yule mama wa kweli akasema afadhali mtoto apewe yule mama mlaghai kuliko kumuona mwanawe akiuawa. Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwangu mwaka wa 2007”, alisema.

Odinga aliuongoza umma kwa kuimba, “rejesha mtoto wetu, rejesha mtoto wetu, rejesha mtoto wetu” na kuwataka Uhuru na makamu wa rais-mteule William Ruto kung’atuka uongozini mara moja.

“Namwaambia ndugu yangu Uhuru kwamba yeye bado ni mdogo na kwamba baba yake alikuwa Rais wa nchi hii kwa miaka 15. Ajue Wakenya hawawezi kuongozwa kwa nguvu. Uhuru huwezi kujilazimisha juu ya Wakenya”.

Alisema Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ilifanya dhambi kubwa kuliko ile ya ECK ya marehemu Samuel Kivuitu mwaka wa 2007.

“Nawaahidi Wakenya kwamba mtaona maajabu kutoka mahakamani. Wizi na ulaghai na ufisadi na ujanja vilikithiri mno wakati wa uchaguzi huo ulioibiwa”, alisema.

Alisema endapo kutakuwa na uchaguzi awamu ya pili, Cord itapinga usimamizi wa IEBC na kutaka kamati huru kusimamia uchaguzi huo.

Alisema alitembelea Mkoa wa Pwani kuwashukuru wapigakura “kwa kupigia kura Cord na mimi kwa fujo”. Aliwaambia wabaki watulivu huku Mahakama Kuu ikiendelea na kesi hiyo ambayo alisema anaamini Cord itashinda.

Mwananchi

Safi sanaaaa big up!!! Haki ichukue mkondo wakeee ndio mpangoo mzima!!

Sent from my BlackBerry 9810 using JamiiForums
 
images

429615_161224080700534_734338026_n.png
 
Back
Top Bottom