Du dingi sasa huko anakoendelea siko. Naona litakuja kuwa zari la kufa mtu hapa, Odinga akimwangwa mahakamani. Mimi ningeshauri wakiitisha kuandamana mwacheni aandamane kwa amani. Mkituma polisi tu hapo wazungu lazima watakuja kuweka no-fly zone.
Sio watakuja, Waingereza wana Military base kubwa tu Kenya tangu siku nyingi, na tayari kuna wanajeshi kibao washamwagwa, hivyo huyo Bw. Odinga anajua anchokifanya, wewe utasikia tu!
Odinga hajashindwa kwenye uchaguzi.wewe unayejidanganya kashindwa ujue unamwandalia njia ya kwenda ikulu.huyu bwana ni so bright>wakenya wamekariri kuwa waongozwe na wakikuyu na wakalenjini na ndo sababu kura huwa zinaibwa.
kila mtu sasa anaona huyu jamaa ni kichaa,basi kama alishinda si angeweka kesi ya kutetea kuwa alinyanganywa ushindi?alafu hizo hesabu zake kweli yeye ni boya
Odinga ni mleta fujo kivipi haswa?
Mijizi ya kura kama Kibaki na Kikuyu allies wake ndo waleta fujo.
Jitu limeiba kura na bila hata simile linaenda kuapishwa uani.
How low can one get than that?
Huyo aliyeapishwa uwani Raila alimkubali ndio maana akawa Waziri Mkuu wake, ww ni nani kupinga? Na isitoshe hiyo ni historia tuzungumzie kilchopo mbele yetu.
Mlikuwa mnapiga kelele ana haki ya kwenda mahakamani sawa amekwenda sasa hizi chokochoko za mitaani za nini? kwa nini asisubiri uamuzi wa mahakama? Hichi anachokitafuta ni kuleta fujo ndani ya nchi!! kilichobaki sasa ni kutandikwa tu! na safari hii atatandikwa kwelikweli ili mpate ya kusema vizuri kwani ndicho mnachokitafuta!!!!!!!!!!!
Acheni uzushi. Raila hajaanzisha wala kuhamasisha vurugu mitaani.
Hata kama hamumpendi kutokana na biases zenu si vyema kumzulia mambo mtu ambayo hajayafanya.
From the jump kwenye hii election cycle amekuwa akihubiri amani.
Mkuu with all due respect, mtu anasimama jukwaani anatangaza kushinda uchaguzi wakati vyombo vilivyopewa jukumu hilo vinasema tofauti hiyo ni nini kama sio kuitisha vurugu?
Wote walikubaliana tokea mwanzo kama hujaridhika nenda mahakamani- sasa kwa nini mahakama isiachiwe itoe maamuzi yake kwanza?
Kwa hali ya siasa za kenya zilivyo kutoa kauli anazotoa Raila hivi sasa ni sawa na kuchezea kibiriti kwenye petroli, moto ukilipuka hakutakuwa na mwingine wa kulaumiwa zaidi yake!!