Rais achaguliwe kwa 'merits' zake sio kwa upande anaotoka, wala dini yake au jinsia yake

Quinine

Platinum Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
25,848
Reaction score
63,306
Katiba inasema Rais akitoka bara basi makamu wake lazima atoke visiwani hata kama upande huo hatuoni mtu mwenye sifa. Hii sio sahihi.

Kuna tendency au tabia ambayo haijandikwa popote kuwa kama Rais anayemaliza muda wake ni mkristo basi atakayefuata lazima awe mwislamu lengo kubalance dini hata kama hakuna mwislamu anayefaa, tabia hii haifai na imepitwa na wakati.

Kuna ubaya gani tukiwa na rais mkristo na makamu wake mkristo kama wana sifa au rais mwislamu na makamu mwislamu.

Jambo jingine la kuangalia ni nafasi ya makamu, kanuni zinasema mgombea Urais atapendekeza mgombea mwenza, nafikiri hili nalo si sahihi, chama husika kishiriki kumpata mgombea mwenza ili kuepuka kupata weak candidate ambaye kikatiba ni president in waiting.

Tujifunze kwa makosa tunayopitia kwa sasa, ni imbalancement kwa nchi.
 
Eti tujifunze kwa yanayotokea kwa sasa..we ni nyumbu tu
Kwa hyo ili mmuone ni kuwa ni bora anatakiwa awe mpole aruhusu kila ujinga?
Na mkileta nyoko nyoko tena mnanyooshwa!
 
Myopic, wewe huwezi kuona consequences yeyote kwa yaliyotokea Ila nafikiri kwa sasa aliko mama yako ana cha kujifunza.
 
Pole pole alifafanua vizuri sana kuhusu kundi la wanamtandao na wahuni. Hizi sasa ndio athari zake.. Na hili kundi bado lina nguvu Sana
 
Tatizo la watu wengi kumchukia huyu tuliyenaye ambaye kaupata urais kwa mserereko Hana sifa ya kuwa president.Hutu alifaa kusimamiwa na siyo yeye kuwa msimamizi.99%ya watanganyika hawamtaki
 
Pole pole alifafanua vizuri sana kuhusu kundi la wanamtandao na wahuni. Hizi sasa ndio athari zake.. Na hili kundi bado lina nguvu Sana
Tatizo la kuwa na kiongozi asiye na vision binafsi anayetegemea wanamtandao wampangie cha kufanya.
 
Katiba inasema Rais akitoka bara basi makamu wake lazima atoke visiwani hata kama upande huo hatuoni mtu mwenye sifa. Hii sio sahihi.

Kuna tendency au tabia ambayo haijandikwa popote kuwa kama Rais anayemaliza muda wake ni mkristo basi atakayefuata lazima awe mwislamu lengo kubalance dini hata kama hakuna mwislamu anayefaa, tabia hii haifai na imepitwa na wakati.

Kuna ubaya gani tukiwa na rais mkristo na makamu wake mkristo kama wana sifa au rais mwislamu na makamu mwislamu.

Jambo jingine la kuangalia ni nafasi ya makamu, kanuni zinasema mgombea Urais atapendekeza mgombea mwenza, nafikiri hili nalo si sahihi, chama husika kishiriki kumpata mgombea mwenza ili kuepuka kupata weak candidate ambaye kikatiba ni president in waiting.

Tujifunze kwa makosa tunayopitia kwa sasa, ni imbalancement kwa nchi.

Rais na Makamu kuwa wa dini moja imeshatokea huko nyuma na hakukuwa na tatizo. Wakati wa JK Makamu wake walikuwa ni Ali Shein na Mohamed Bilal.

Ila siku ikitokea Rais na Makamu wakristo ..... wote tunajua kelele zake zitakuwaje.
 
Ikitokea hivyo kelele yake itakuwa si ya karne hii kila siku matamko kila mtu atakuwa shehe.
 
Back
Top Bottom