PakaJimmy
JF-Expert Member
- Apr 29, 2009
- 16,199
- 8,761
Bila ya kusitasita ,Nyerere alikuwa Mkristo alifanikiwa kuiweka nchi kwenye mstari heshima kwa watu wa dini zote zilikuwepo japo kulikuwa na manunguniko ya hapa na pale.
Akaingia Mwinyi ,yeye ni Muislamu halikadhalika Nchi ilikuwa imetulia hakuna mvutano ,na wengi waliweza kuona uongozaji wake ulikuwa ule wa fanya na nenda uwezako lakini usivunje sheria ,ilitokea watu wakamsifu kuwa mifuko ya wananchi ilikuwa inajaa vijisenti ,japo senenesenene hazikukosa.
Akaingia Mkapa yeye ni Mkristo .uongozaji wake ulikumbwa na ubabe na walevi wengi walikuwa wakipatiliza na ndipo matabaka yalipoanza kujitokeza na nchi kuuzwa kwa bei poa na kusababisha hata uhuru wa dini kuvurugika na kila mmoja kuona anagandamizwa.
Hapa tulipo tunae Kikwete yeye ni Muislamu ,uongozi wake unaonekana kuwa dhaifu na unaolegalega ,baada ya nchi kuchafuliwa na Mkapa ,Kikwete anaonekana kushindwa kuiridisha kwenye mstari ,malalamiko yameongezeka kila sehemu mauaji ya ovyoovyo yamezagaa .
Nakusifu sana wewe Mwiba kwa uchambuzi wako.
Mbona wadau wengine mnakuwa waoga? Kutoongelea jambo kutalifanya lijisolve?
Kwanini mnashindwa kujibu hoja ya msingi ya mtoa mada, mnaanza kumlaumu unnecessarily? Elezeni mnachoficha na si kukimbia NA KULAUMU..
Kwani hamuwajui wapenda kucheza Ngoma wanatoka maeneo gani, na kwani hamtazami runinga mkamwona ZUMA na ngoma? Mnataka kusema hamjui kuwa MWIBA NI mtu wa wapi , wakati anaongelea SENENE? Nani hajui kwamba tabia za watu zinaathiriwa au kuwa framed na mazingira? Ni nani aliyelikana ziwa la mamaye? Na tangu lini mwenda kwao akawa mtoro? Au nianze tena somo la Saikolojia?
Management ni fani inayojitegemea, na ni matter ya personality, lakini tusisahau kwamba kuna styles za management ambapo ndipo hapo watu huingizia u`majimbo wao. Si dhambi kuongelea jambo hilo wadau, mnakumbuka kuwa hata kwenye kampeni za ubunge kulikuwa na tabia wa kuongea kilugha, hadi tume ya uchaguzi ilipostukia?
Mimi ninasema kwamba kuna direct relationship kati ya mtu na kule atokako. These two have always been a clone of one-another.