Wewe ambae sio wa hovyo tuambie umeifanyia nini Nchi hii toka ujitambue!! Mmeshindwa kufanya harakati zenu kwasababu ya uroho wenu,sasa mnataka watu wasifurahie maisha yao kisa harakati!! Nonsense kabisa. Hata uko Kenya kipindi wanauana kabla ya kupata katiba mpya, wapo watu walikuwa wanakula maisha yao bila stress wala shinikizo la mtu.
Hao wanaharakati wenu na wanasiasa,watoto wao wanasoma hapa nchini?uyo Lissu,Mbowe watoto wao wanasoma hapa nchini,sasa tofauti yao na maccm ni nini? Tanzania hakuna wanaharakati ni njaa tu na kujiuza kama malaya wa riverside! Mtu anatafuta umaarufu ili anunuliwe na watawala kwa bei juu! Wengine wamepata tu ubunge kwa nguvu ya Umma kupitia vyama vya upinzani,wanaanza kutambia wananchi, maisha mazuri wanayoishi wakiwaonyesha mahoteli wanayomiliki na kujisifu kwa safari za daraja la kwanza kwenye ndege!
Mimi binafsi yangu siwezi kujishughulisha na siasa za kitanzania zilizojaa ghiriba na tamaa,nafanya shughuli zangu naenjoy maisha yangu,nikijisikia kununua jezi hata millioni kama ninazo nitanunua! Kama kuna starehe ya kuangalia hata milioni kumi nitaenda,siwezi kujitesa kuwaunga mkono wanasiasa malaya wasio na msimamo.