Rais akikosea aambiwe ukweli hadi aelewe

Hela zitakazopatikana zitakwenda kwenye miradi itakayowasaidia Watanzania na siyo kwenye mifuko ya mafisadi wanaoficha mpaka sh. Bilioni 7 majumbani mwao? Mimi langu ni hilo tu. Haya tuuze Ngorongoro. Kwa faida ya nani?

Kusingekuwa na ufisadi na upigaji huu wa kijinga na kihayawani, Tanzania iliyobarikiwa hivi ingekuwa mbali sana. Mama mpaka namhurumia yaani!
 
Shida ipo hapa, JE! RAIS ANAAMINI KUWA ANAWEZA KUKOSEA?
 
Africa mtu akipewa ridhaa ya kuongoza anachukulia wote kawazidi upeo na ni hamnazo hvyo hakuna kitu anaweza fanywa.


Kauli ya kikubwa HELA ni kauli ya kipumbafu na upeo mdg sana kiakili unapaswa kupigwa vita.
 
Kuhusu kuzitumia vizuri sijui😅

Ila hela watapata

mimi naona kama hizi hifadhi hazitokaa sana

iligundulika kuna mafuta na uranium selous, UNESCO wakakubali mipaka ipunguzwe. JNPP nayo imejengwa hayo maeneo....

Haya, hii SGR imekatiza mikumi....

Uvumilivu utakuja kutushinda tutakata misitu yoooote.
 
Kama Tanapa hawataki basi wako sahihi kabis
 
Lakini kwani huwezi chimba Madini katika namna ya kudhibiti uharibifu wa mazingira na baadae mbuga kurejesha uoto?
 
Wajomba zake washatengeneza ZOO kule kwao, anataka kuharibu za asili.

Anauza Tanganyika, watanganyika wako busy kutafuta madaraka wasiyoyafikia miaka nenda rudi....ni mwanasiasa gani tunaweza dhani ni Mtanganyika halisi mzalendo kwa sasa?
  • Zito?
  • Mbowe?
  • Msigwa?
  • Lisu?
  • Ndugai?
  • Warioba?

Achana na wale watoto wao wanaopiga kelele mtandaoni wazazi wao wanapobanwa kama Shangazi etc.
 
Kama Tanapa hawataki basi wako sahihi kabis
Kuna siasa nyingi kwenye mambo ya hifadhi

wachimbaji wakubwa waliomba selous ipunguzwe 2012.
TANAPA ikafanikiwa kuwazuia 2017. Unaambiwa kuna migodi 48 ingefunguliwa selous.

Lakini maghufuli alipoamua kujenga JNPP, UNESCO, WWF, na TANAPA wote walimshindwa😅
 
Huko kwenye madini bila shaka wajomba zake wa uarabuni wameshaona eneo kwa hiyo hiyo statement ya kutuandaa kisaikolojia watapopewa eneo ndani ya mbuga.

Kama vipi huo ujinga ukafanyike kwenye mbuga za nyumbani kwao Zanzibar.
 
Au pengine ni wataalam wetu hawambambii ukweli Rais, ukweli ni kwamba ukiwa Rais haimaanishi unajua kila kitu...vitu vingi tu hasa vya kitaalam unakuwa huvijui.
Urais ni cheo tu na sio ujuzi, Sa100 hapa umepuyanga...sio kila kitu kinafaa uwekezaji!.
Migodi inaenda sambamba na hekaheka nyingi ambazo sio rafiki kwa wanyama pori.
Hv Sa100 anzijua blasting za migodini kweli?!.
 
Huyu kiukweli angepumzika ni basi tu madaraka matamu ccm wangeleta mtu mwingine yeye mwenyewe aliwahi kusema katiba sio msahafu kusema hauwezi kubadilishwa wangempumzisha walete mtu mwingine hata Simba chawene ni mtu sana kwenye anaweza kutufaa
 
CHURA KIZiWI HIVI HUKUELEWA???
 
Kuna vitu hamuelewani na huyo
Unaposema mwaka Jana madini yaliingiza $3 billion, unamaanisha nn? Hii ni trllion 8.4
Na hiyo utalii ni trillion 9, jumla trillion 18. Kwa mwaka makusanyo yetu ni trllion 26, hapo si ingekua maji bure, umeme bure, matibabu bure😂😂😂

Huyo anazungumzja government revenues, mapato serikali inayopata kutoka kwenye madini. Mapato ya serikali kwa mwaka kutoka kwenye madini kwa sasa ni around bilioni 700
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…