Rais akikosea aambiwe ukweli hadi aelewe

Rais akikosea aambiwe ukweli hadi aelewe

Tunakoelekea ni kubaya zaidi jamani. Viongozi waliotangulia wangekuwa wanapambana kuuza kila kitu yeye angekuta nini? Hizo hela wanazopokea baada ya mauzo zinafanya nini zaidi ya kuliwa na wajanja wachache?

Kwani ni lazima rasilimali zote ziuzwe in her regime? Yani napata ile feeling ya mzazi kutaka kuuza mali zake sababu amezeeka ili atumbue kabla hajafa bila kujali kizazi cha wajukuu zake kitakuja kuanza kuhangaika upya
Kwanza hongereni kwa kupokea ruzuku kila mwezi nyie chadema, nasikia mmeomba na Ruzuku za miaka ya nyuma hebu achen ulafi,
 
Kwani Hadi sasa watakaokuja kuchimba madini ushawajua?..
Why unahisi watakuwa waarabu?

Informed decisions ni Jambo moja
Na execution ni Jambo lingine
Mkuu, mbona siyo ngumu kabisa kuwafahamu.

Hifadhi na Mbuga za wanyama ni WORLD NATURAL HERITAGE hivyo zinalindwa na miongozo na matamko ya UMOJA WA MATAIFA. Hivyo uhakika ni asilimia 100% kwamba makampuni ya Ulaya na Marekani hayawezi kuchimba kwasababu ya kuogopa kelele na vikwazo (Sanctions and Boycotts) kutoka kwa mataifa na mashirika makubwa yanapigia chapuo suala zila la mazingira na mabadiliko ya hali ya hewa (Global Warming).

Hivyo kama ambavyo Raisi Magufuli aliwafuata waarabu, ARAB CONTRACTORS, ili wajenge STIEGLER'S GORGE, sehemu ambayo ni WORLD HERITAGE, vivyo hivyo Raisi Samia ashawapa waarabu haki hiyohiyo kwasababu mashirika yao hayawezi kuguswa kabisa na vikwazo vya mashirika na nchi za Magharibi. Ndiyo maana mpaka sasa, wanyama wanauzwa kwa UAE siyo America or United Kingdom ambako ingezua tahariki.

Haya sasa, hebu mtuache tufanye kazi na waarabu ambao haki za binadamu kwao ni jambo la kufuru. Hawa mabeberu watatupigia kelele.

Msimkwamishe MAMA.​
 
..shida yetu ni mapato.

..tukiihifadhi Serengeti na kuitangaza zaidi tunaweza kuongeza mapato serikalini.

..hatupaswi kukata tamaa ktk utalii wetu na kuanza kuvuruga na kuharibu hifadhi zetu.

..vilevile yako maeneo mengi ya Tanganyika ambayo yana madini na hayako ktk hifadhi, ni vizuri serikali ikachimba huko, badala ya kulazimisha kuchimba Serengeti.
Hata kwenye Bandari mlisema hivihivi, kwamba tujiamini sisi wenyewe ili mapato yongezeke. Mzee George Mkuchika akawajibu na kusema ni lazima tuwape wageni bandari ili tupate mapato zaidi. Hata Zembwela na Kitenge nao walitoa hoja nzito kuhusu hili baada ya kwenda Dubei kufanya utafiti mkubwa na kuacha kujificha nyuma ya Keyboard kama wewe.

Pia, nikutoe hofu kwamba hizo sehemu nyingine zenye madini nako MAMA atafika kabla hajaondoka. Ila imeamuliwa kwanza tuanzie kwenye mbuga ambako ndiko kuna ugumu na upinzani mkubwa. Huko kwingine hakutasumbua wala hakutakuwa na makelele na majungu ya wakristo na watanganyika kutaka kukwambisha juhudi za mama.​
 
Mkuu, mbona siyo ngumu kabisa kuwafahamu.

Hifadhi na Mbuga za wanyama ni WORLD NATURAL HERITAGE hivyo zinalindwa na miongozo na matamko ya UMOJA WA MATAIFA. Hivyo uhakika ni asilimia 100% kwamba makampuni ya Ulaya na Marekani hayawezi kuchimba kwasababu ya kuogopa kelele na vikwazo (Sanctions and Boycotts) kutoka kwa mataifa na mashirika makubwa yanapigia chapuo suala zila la mazingira na mabadiliko ya hali ya hewa (Global Warming).

Hivyo kama ambavyo Raisi Magufuli aliwafuata waarabu, ARAB CONTRACTORS, ili wajenge STIEGLER'S GORGE, sehemu ambayo ni WORLD HERITAGE, vivyo hivyo Raisi Samia ashawapa waarabu haki hiyohiyo kwasababu mashirika yao hayawezi kuguswa kabisa na vikwazo vya mashirika na nchi za Magharibi. Ndiyo maana mpaka sasa, wanyama wanauzwa kwa UAE siyo America or United Kingdom ambako ingezua tahariki.

Haya sasa, hebu mtuache tufanye kazi na waarabu ambao haki za binadamu kwao ni jambo la kufuru. Hawa mabeberu watatupigia kelele.

Msimkwamishe MAMA.​

Mkuu una hoja dhaifuu, nadhani hadi The Boss anaona aibu kukusapoti pamoja na kujifungamanisha naye kwamba ni ndg yako ktk imani.
Hakika unatia aibu!.
 
Tunao wataalamu wa mazingira na waandishi wa habari za kimazingira {Environmental journalism}kwanini wasifanye costs and benefits analysis na umma uhabarishwe juu ya findings ?

Kama kule Ngorongoro zilitumika claims za kulinda mazingira na ikolojia ya hifadhi kwanini sasa tunataka kuruhusu shughuli za kibinadamu ndani ya Serengeti ?
 
28% ya ardhi Tanzania imehifadhiwa, mbona kama nyingi?

utalii na madini havitofautiani kivile, mwaka jana utalii uliingiza $3.52b, madini $3.06b

na hapo ni baada ya utalii kuweka rekodi ambayo haijawahi tokea tangu uhuru

shida ninayoona labda ni kwamba serikali ikifanya kitu haiwaambii wananchi kwanini, haishawishi....

lakini nyie wananchi wengi mna 'siasa za hisia' mmeamua kumchukia mama basi kila anachofanya mnachukia
Mama ameingia madarakani watu wakawa wanamuangalia atafabya nini.

Shida sio kumchukia mama,shida anafanya nini ndio watu wamchukie.
Huwezi chimba madini mbugani! Hilo sio sawa,

Kama Shida ni hela Akitokea mtu anataka kupangisha ikulu akae atakubali? Hiyo ni kauli ya ajabu kutokea.

Mama **** shida kubwa anapitia nahisi maana maamuzi yake na matamshi yake sio ya kawaida,
 
Sidhani kama huyu mama ana uchungu na hii Bara yetu!
Uharibifu unazidi kutamalaki kama enzi za awamu ya $
 
Nimeshakusoma GT🤣
Naona Braza Mkubwa The Boss, na wengine washaanza kupata somo, kwamba bila Spidi Gavana MAZA wetu atapiga mnada hadi misikiti na makanisa. Nafurahi kwamba sasa watu wameanza kufahamu kwamba, MAZA alitumia dini kufanya Divide and Rule, halafu baadaye akaanza kutusawazisha vizuri.

Hili hata baadhi yetu lilitukuta kipindi cha utawala wa BWANA YULEEE, alivyoanza hata mimi niliamini MASIHI amefika. Baada ya kusema tu kwamba "Wachagga wasubiri sehemu nyingine ziendelee kwanza" nikajua hapa tushapigwa vibaya.​
 
Umerudi kwenye track ...

Hukuwahi kuona tatizo kwenye utawala huu...

Nini kimekupata?
Uzuri Braza Mkubwa ni mtu muelewa, anajirudi taratibu. Mimi nakumbuka kipindi cha Jakaya alikuwa upande wa mabadiliko na alizipinga mno sera zake za kifisadi. Lakini kama ufahamuvyo, MAZA alikuja na sura ya MALAIKA, kumbe chini ni YEZEBELI, akahadaa watu wengi kweli, akitumia karata ya DINI. Baadaye sasa watu washaanza kusanua mchezo kwamba MAZA, hayuko kwa ajili wa WAISLAMU wala WAZANZIBAR, she's all about business yaaani.​
 
Wakati wa Magufuli niliwahi andika hapa kama Magufuli anao watu wa kumwambia ukweli na akawasikiliza, nilitoa mfano wa Fidel Castro alivyokuwa anaogopwa na watu wengi sana lakini walikuwepo watu wawili walikuwa wana uwezo wa kumwambia ukweli Raul Castro mdogo wake na Comrade Che Guevara. Hawa wawili walikuwa na uwezo wa kumwambia ukweli na makosa yake bila kupepesa macho na akawasikiliza.

Juzi Rais Samia kasema madini yachimbwe kwenye mbuga, cha muhimu hela. Hii kauli si sahihi kabisa tena sio sahihi kutoka kwa Rais wa nchi.

Rais alipaswa kwanza kupata elimu ya kutosha kuhusu uchimbaji wa madini na athari za mazingira, lakini la muhimu zaidi alipaswa kuniuliza kwanini Viongozi kabla yake wote walisita au kukataa kutoa vibali vya kuchimba Mbugani?

Je hata kama tukikubaliana na Rais cha muhimu hela, kwani Rais hajui utalii ndo unaingiza hela Tanzania kupita madini?

Rais hajui au hana ushauri wa kumwambia kuwa athari za kimazingira huko Mbugani zinaweza moja Kwa moja kuathiri utalii na kupunguza mapato kuliko hata kuongeza hayo mapato?

Rais hajui kuwa hayo makampuni ya madini huwa yanaahidi sana mambo mengi mazuri lakini mwisho hushindwa kutekeleza kuanzia Kodi hadi taratibu za kulinda hayo mazingira? Kampuni ya madini inaweza sababisha sumu kwenye vyanzo vya maji ya wanyama hadi binadamu, na hili sio nadharia imewahi tokea na ushahidi upo.

Madini yanaweza chimbwa yakaisha na mapato ya maana yasipatikane, imeshatokea..na haitakuwa la ajabu ikitokea tena.

Mbuga za Wanyama zilzopo Tanzania haipatikani tena kwingine duniani, ni urithi wa dunia. Mbuga kama Serengeti ina Wanyama Wengi kupitia Mbuga yeyote duniani, hii Peke yake ni dhahabu kuliko dhahabu yenyewe.

Mbuga kama Selous ukubwa wa Ardhi tu ni zaidi ya nchi ya Belgium, halafu leo tunaanza tena kuruhusu uharibifu wa mazingira Mbugani mradi ipatikane hela? tuharibu kuku anaetotoa mayai ya dhahabu ili tukatafute mayai mengine tumboni?

Rais akikosea aambiwe hadi aelewe.
Rais ni taasisi
 
Rais ni taasisi
Kiuhalisia, hii kauli hainaga maana yoyote..katiba yetu haina nguvu hivyo mambo kibao yanaamuliwa kwa utashi wa Rais aliyepo wakati huo.
Kwa mfano...wakati wa Magufuli aliapa kwamba chini ya utawala wake hakuna mwanafunzi mjamzito ambaye ataruhusiwa kuendelea na masomo mara baada ya kujifungua, kaja Sa100 kasema mwanafunzi mjamzito akishajifungua aruhusiwe kuendelea na masomo!!.
Hivyo hata hili la kuruhusu uanzishwaji wa migodi hifadhini ni AKILI ya Rais tu yeye binafsi, si umeona utetezi eti tunataka hela wakati madini yenyewe hayaliwi na Simba wala Tembo🤣🤣
 
Wakati wa Magufuli niliwahi andika hapa kama Magufuli anao watu wa kumwambia ukweli na akawasikiliza, nilitoa mfano wa Fidel Castro alivyokuwa anaogopwa na watu wengi sana lakini walikuwepo watu wawili walikuwa wana uwezo wa kumwambia ukweli Raul Castro mdogo wake na Comrade Che Guevara. Hawa wawili walikuwa na uwezo wa kumwambia ukweli na makosa yake bila kupepesa macho na akawasikiliza.

Juzi Rais Samia kasema madini yachimbwe kwenye mbuga, cha muhimu hela. Hii kauli si sahihi kabisa tena sio sahihi kutoka kwa Rais wa nchi.

Rais alipaswa kwanza kupata elimu ya kutosha kuhusu uchimbaji wa madini na athari za mazingira, lakini la muhimu zaidi alipaswa kuniuliza kwanini Viongozi kabla yake wote walisita au kukataa kutoa vibali vya kuchimba Mbugani?

Je hata kama tukikubaliana na Rais cha muhimu hela, kwani Rais hajui utalii ndo unaingiza hela Tanzania kupita madini?

Rais hajui au hana ushauri wa kumwambia kuwa athari za kimazingira huko Mbugani zinaweza moja Kwa moja kuathiri utalii na kupunguza mapato kuliko hata kuongeza hayo mapato?

Rais hajui kuwa hayo makampuni ya madini huwa yanaahidi sana mambo mengi mazuri lakini mwisho hushindwa kutekeleza kuanzia Kodi hadi taratibu za kulinda hayo mazingira? Kampuni ya madini inaweza sababisha sumu kwenye vyanzo vya maji ya wanyama hadi binadamu, na hili sio nadharia imewahi tokea na ushahidi upo.

Madini yanaweza chimbwa yakaisha na mapato ya maana yasipatikane, imeshatokea..na haitakuwa la ajabu ikitokea tena.

Mbuga za Wanyama zilzopo Tanzania haipatikani tena kwingine duniani, ni urithi wa dunia. Mbuga kama Serengeti ina Wanyama Wengi kupitia Mbuga yeyote duniani, hii Peke yake ni dhahabu kuliko dhahabu yenyewe.

Mbuga kama Selous ukubwa wa Ardhi tu ni zaidi ya nchi ya Belgium, halafu leo tunaanza tena kuruhusu uharibifu wa mazingira Mbugani mradi ipatikane hela? tuharibu kuku anaetotoa mayai ya dhahabu ili tukatafute mayai mengine tumboni?

Rais akikosea aambiwe hadi aelewe.
Kwa hili nipo na wewe. Madam President alifikirie tena hili.
 
Tuthibitishie hiyo kauli ndugu...

Watu wengi wanakuheshimu humu.
Kama alisema Msiwabomolee nyumba Mwanza kwasababu walinipa kura, ambako huku akibomoa kwingine angeshindwa kusema nini BWANA YULE ???

SWADAKTAAA, ntakutafutia lile gazeti, maana naona bado husadiki kama TOMASO.​
 
Ukileta hiyo taarifa tamdharau sana Magufuli.
 
Rais alipaswa kwanza kupata elimu ya kutosha kuhusu uchimbaji wa madini na athari za mazingira, lakini la muhimu zaidi alipaswa kuniuliza kwanini Viongozi kabla yake wote walisita au kukataa kutoa vibali vya kuchimba Mbugani?
Tukiwaambia hana uchungu na rasilimali za bara tunasimangwa
 
Back
Top Bottom