Kwanza hongereni kwa kupokea ruzuku kila mwezi nyie chadema, nasikia mmeomba na Ruzuku za miaka ya nyuma hebu achen ulafi,Tunakoelekea ni kubaya zaidi jamani. Viongozi waliotangulia wangekuwa wanapambana kuuza kila kitu yeye angekuta nini? Hizo hela wanazopokea baada ya mauzo zinafanya nini zaidi ya kuliwa na wajanja wachache?
Kwani ni lazima rasilimali zote ziuzwe in her regime? Yani napata ile feeling ya mzazi kutaka kuuza mali zake sababu amezeeka ili atumbue kabla hajafa bila kujali kizazi cha wajukuu zake kitakuja kuanza kuhangaika upya
Haijui dunia huyu. Hajui impact ya anachofanya.Halafu atachafuka vibaya Sana especially hizo kampuni za madini zikitoka huko Asia... western media zitamchafua kupita maelezo....
Hii habari inaweza kumchafua milele kuliko anavyofikiria
Kwani Hadi sasa watakaokuja kuchimba madini ushawajua?..
Why unahisi watakuwa waarabu?
Informed decisions ni Jambo moja
Na execution ni Jambo lingine
..shida yetu ni mapato.
..tukiihifadhi Serengeti na kuitangaza zaidi tunaweza kuongeza mapato serikalini.
..hatupaswi kukata tamaa ktk utalii wetu na kuanza kuvuruga na kuharibu hifadhi zetu.
..vilevile yako maeneo mengi ya Tanganyika ambayo yana madini na hayako ktk hifadhi, ni vizuri serikali ikachimba huko, badala ya kulazimisha kuchimba Serengeti.
Mkuu, mbona siyo ngumu kabisa kuwafahamu.
Hifadhi na Mbuga za wanyama ni WORLD NATURAL HERITAGE hivyo zinalindwa na miongozo na matamko ya UMOJA WA MATAIFA. Hivyo uhakika ni asilimia 100% kwamba makampuni ya Ulaya na Marekani hayawezi kuchimba kwasababu ya kuogopa kelele na vikwazo (Sanctions and Boycotts) kutoka kwa mataifa na mashirika makubwa yanapigia chapuo suala zila la mazingira na mabadiliko ya hali ya hewa (Global Warming).
Hivyo kama ambavyo Raisi Magufuli aliwafuata waarabu, ARAB CONTRACTORS, ili wajenge STIEGLER'S GORGE, sehemu ambayo ni WORLD HERITAGE, vivyo hivyo Raisi Samia ashawapa waarabu haki hiyohiyo kwasababu mashirika yao hayawezi kuguswa kabisa na vikwazo vya mashirika na nchi za Magharibi. Ndiyo maana mpaka sasa, wanyama wanauzwa kwa UAE siyo America or United Kingdom ambako ingezua tahariki.
Haya sasa, hebu mtuache tufanye kazi na waarabu ambao haki za binadamu kwao ni jambo la kufuru. Hawa mabeberu watatupigia kelele.
Msimkwamishe MAMA.
Mama ameingia madarakani watu wakawa wanamuangalia atafabya nini.28% ya ardhi Tanzania imehifadhiwa, mbona kama nyingi?
utalii na madini havitofautiani kivile, mwaka jana utalii uliingiza $3.52b, madini $3.06b
na hapo ni baada ya utalii kuweka rekodi ambayo haijawahi tokea tangu uhuru
shida ninayoona labda ni kwamba serikali ikifanya kitu haiwaambii wananchi kwanini, haishawishi....
lakini nyie wananchi wengi mna 'siasa za hisia' mmeamua kumchukia mama basi kila anachofanya mnachukia
Mkuu, unatia aibu wewe!Mkuu una hoja dhaifuu, nadhani hadi The Boss anaona aibu kukusapoti pamoja na kujifungamanisha naye kwamba ni ndg yako ktk imani.
Hakika unatia aibu!.
Nimeshakusoma GT🤣
Umerudi kwenye track ...
Hukuwahi kuona tatizo kwenye utawala huu...
Nini kimekupata?
Rais ni taasisiWakati wa Magufuli niliwahi andika hapa kama Magufuli anao watu wa kumwambia ukweli na akawasikiliza, nilitoa mfano wa Fidel Castro alivyokuwa anaogopwa na watu wengi sana lakini walikuwepo watu wawili walikuwa wana uwezo wa kumwambia ukweli Raul Castro mdogo wake na Comrade Che Guevara. Hawa wawili walikuwa na uwezo wa kumwambia ukweli na makosa yake bila kupepesa macho na akawasikiliza.
Juzi Rais Samia kasema madini yachimbwe kwenye mbuga, cha muhimu hela. Hii kauli si sahihi kabisa tena sio sahihi kutoka kwa Rais wa nchi.
Rais alipaswa kwanza kupata elimu ya kutosha kuhusu uchimbaji wa madini na athari za mazingira, lakini la muhimu zaidi alipaswa kuniuliza kwanini Viongozi kabla yake wote walisita au kukataa kutoa vibali vya kuchimba Mbugani?
Je hata kama tukikubaliana na Rais cha muhimu hela, kwani Rais hajui utalii ndo unaingiza hela Tanzania kupita madini?
Rais hajui au hana ushauri wa kumwambia kuwa athari za kimazingira huko Mbugani zinaweza moja Kwa moja kuathiri utalii na kupunguza mapato kuliko hata kuongeza hayo mapato?
Rais hajui kuwa hayo makampuni ya madini huwa yanaahidi sana mambo mengi mazuri lakini mwisho hushindwa kutekeleza kuanzia Kodi hadi taratibu za kulinda hayo mazingira? Kampuni ya madini inaweza sababisha sumu kwenye vyanzo vya maji ya wanyama hadi binadamu, na hili sio nadharia imewahi tokea na ushahidi upo.
Madini yanaweza chimbwa yakaisha na mapato ya maana yasipatikane, imeshatokea..na haitakuwa la ajabu ikitokea tena.
Mbuga za Wanyama zilzopo Tanzania haipatikani tena kwingine duniani, ni urithi wa dunia. Mbuga kama Serengeti ina Wanyama Wengi kupitia Mbuga yeyote duniani, hii Peke yake ni dhahabu kuliko dhahabu yenyewe.
Mbuga kama Selous ukubwa wa Ardhi tu ni zaidi ya nchi ya Belgium, halafu leo tunaanza tena kuruhusu uharibifu wa mazingira Mbugani mradi ipatikane hela? tuharibu kuku anaetotoa mayai ya dhahabu ili tukatafute mayai mengine tumboni?
Rais akikosea aambiwe hadi aelewe.
Tuthibitishie hiyo kauli ndugu...Baada ya kusema tu kwamba "Wachagga wasubiri sehemu nyingine ziendelee kwanza" nikajua hapa tushapigwa vibaya.
Kiuhalisia, hii kauli hainaga maana yoyote..katiba yetu haina nguvu hivyo mambo kibao yanaamuliwa kwa utashi wa Rais aliyepo wakati huo.Rais ni taasisi
Kwa hili nipo na wewe. Madam President alifikirie tena hili.Wakati wa Magufuli niliwahi andika hapa kama Magufuli anao watu wa kumwambia ukweli na akawasikiliza, nilitoa mfano wa Fidel Castro alivyokuwa anaogopwa na watu wengi sana lakini walikuwepo watu wawili walikuwa wana uwezo wa kumwambia ukweli Raul Castro mdogo wake na Comrade Che Guevara. Hawa wawili walikuwa na uwezo wa kumwambia ukweli na makosa yake bila kupepesa macho na akawasikiliza.
Juzi Rais Samia kasema madini yachimbwe kwenye mbuga, cha muhimu hela. Hii kauli si sahihi kabisa tena sio sahihi kutoka kwa Rais wa nchi.
Rais alipaswa kwanza kupata elimu ya kutosha kuhusu uchimbaji wa madini na athari za mazingira, lakini la muhimu zaidi alipaswa kuniuliza kwanini Viongozi kabla yake wote walisita au kukataa kutoa vibali vya kuchimba Mbugani?
Je hata kama tukikubaliana na Rais cha muhimu hela, kwani Rais hajui utalii ndo unaingiza hela Tanzania kupita madini?
Rais hajui au hana ushauri wa kumwambia kuwa athari za kimazingira huko Mbugani zinaweza moja Kwa moja kuathiri utalii na kupunguza mapato kuliko hata kuongeza hayo mapato?
Rais hajui kuwa hayo makampuni ya madini huwa yanaahidi sana mambo mengi mazuri lakini mwisho hushindwa kutekeleza kuanzia Kodi hadi taratibu za kulinda hayo mazingira? Kampuni ya madini inaweza sababisha sumu kwenye vyanzo vya maji ya wanyama hadi binadamu, na hili sio nadharia imewahi tokea na ushahidi upo.
Madini yanaweza chimbwa yakaisha na mapato ya maana yasipatikane, imeshatokea..na haitakuwa la ajabu ikitokea tena.
Mbuga za Wanyama zilzopo Tanzania haipatikani tena kwingine duniani, ni urithi wa dunia. Mbuga kama Serengeti ina Wanyama Wengi kupitia Mbuga yeyote duniani, hii Peke yake ni dhahabu kuliko dhahabu yenyewe.
Mbuga kama Selous ukubwa wa Ardhi tu ni zaidi ya nchi ya Belgium, halafu leo tunaanza tena kuruhusu uharibifu wa mazingira Mbugani mradi ipatikane hela? tuharibu kuku anaetotoa mayai ya dhahabu ili tukatafute mayai mengine tumboni?
Rais akikosea aambiwe hadi aelewe.
Tuthibitishie hiyo kauli ndugu...
Watu wengi wanakuheshimu humu.
Ukileta hiyo taarifa tamdharau sana Magufuli.Kama alisema Msiwabomolee nyumba Mwanza kwasababu walinipa kura, ambako huku akibomoa kwingine angeshindwa kusema nini BWANA YULE ???
SWADAKTAAA, ntakutafutia lile gazeti, maana naona bado husadiki kama TOMASO.
Tukiwaambia hana uchungu na rasilimali za bara tunasimangwaRais alipaswa kwanza kupata elimu ya kutosha kuhusu uchimbaji wa madini na athari za mazingira, lakini la muhimu zaidi alipaswa kuniuliza kwanini Viongozi kabla yake wote walisita au kukataa kutoa vibali vya kuchimba Mbugani?