Rais ambaye hajawahi kugombea, ilitokea Marekani, itatokea tena huku

Rais ambaye hajawahi kugombea, ilitokea Marekani, itatokea tena huku

Kama nimekusoma unamaanisha atakaeteuliwa umakamu wa Rais kumsaidia mama atakuwa Rais kabla ya mama kukamilisha hii miaka 4 na ushee?

Kama ndio hivyo nitamuomba Mungu abatilishe hii kitu ila tu kwa mapenzi yake basi angalau mama amalizie miaka 5 japo binafsi napenda aende hadi 2030

Sitaki kabisa tuingie kwenye historia ya Zambia
 
Wakuu,

Mwaka 1973 Spiro Agnew alijiuzulu nafasi ya makamu wa Rais wa Marekani kufuatia skendo ya rushwa na matumizi mabaya ya ofisi ikiwemo kukwepa kodi alikofanya wakati ni governor wa Maryland. Rais Richard Nixon akamteua Gerald Ford kuchukua nafasi yake.

August ya mwaka 1974, Rais Richard Nixon alijiuzulu kufuatia skendo ya Watergate. Hapo ikabidi makamu wa Rais, bwana Gerald Ford aapishwe kuwa Rais wa Marekani.

Unaweza kuona jinsi Ford alivyokuwa na bahati. Hakuwahi kugombea umakamu wa Rais au Urais wenyewe lakini alishika vyeo vyote hivyo kwa nyakati tofauti zinazofuatana.

Nimeandika hii habari kuonyesha yanayokuja soon.

Endelea kusubiri!
😳😳😳😳😳
 
Back
Top Bottom