Mlokua mnasubiri bei za umeme zishuke poleni...
Mnaosubiri eti hiyo siku ya uzinduzi atatangaza bei ya umeme kushuka kuanzia September mosi poleni
Hii habari nina uhakika nayo asilimia 100%
Niliwaambia hatupendi sisi watu wa Upande huu mkabisha ingekua ni kule kwao angetangaza gharama ya units ishuke
Kuelekea uzinduzi wa bwawa la Nyerere miongoni mwa ajenda na sababu za ujenzi ni gharama za umeme kushuka zaidi gharama ya units
Namheshimu Engineer mramba ni mtendaji nzuri hapo Tanesco lakini hili la kumshawishi Rais umeme usishuke bei sidhani kama umewatendea haki Watanzania.
Anatumia kigezo cha bei za nchi jirani akisema eti sisi bado ni nafuu zaidi na pia akisema eti lazima gharama za mradi zirudi..
Na rais naye amekubali kuwa hakuna tena gharama ya umeme kushuka baada ya bwawa kukamilika, hapo ndo mtajua tulivyo na viongozi wabinafsi nchi hii....
Mramba anadai umeme hauwezi kushuka chini ya sasa kwani eti kitakwimu kwa East africa sisi bado bei ipo chini anasahau lengo la kujengwa kwa bwawa hili ni ili wananchi wote wapate umeme kwa bei ndogo watu wapikie umeme waachane na mikaa na kukata viwanda vifunguliwe nk lakini hii nchi watu ni wabinafsi sana...
Kwahiyo mnaosubiri Tangazo la bei za umeme kushuka hiyo siku ya uzinduzi msahau kabisa!!