Bwana Kaka, wizi wa fedha za serikali si wa mtu mmoja mmoja bali ni mfumo. Ni ngumu sana mtu mmoja kuiba fedha za serikali, labda aibe vifaa. Sasa mfumo mzima wa serikali kuanzia Waziri hadi muhudumu unaweza kuhamisha mabilioni ya pesa, kila mmoja napata mgao wake na mradi haufanyiki na fedha zinaonekana kimaandishi zimetoka. Tukubali ukweli kwamba malezi yetu kuanzia ngazi ya familia, mashuleni, nk...yanazalisha tabia za watu walafi na wabinafsi. Hivi unakumbuka shule za boarding, chakula kizuri eti wanakula viongozi, au mchuzi wenye mafuta mengi (top layer) unachotwa na kugawia viongozi tu. Sasa hao wakija kuwa viongozi serikalini wataachaje kujipendelea? Rais akitaka kuonesha mfano, siku moja ang'oe mfumo mzima, haijalishi watakuwa watu wangapi. Mwaka 1982 kuna mahabusu wahaini walitoroka Gereza Keko, na katika kuwajibika aliondoka Waziri (Mambo ya Ndani), Kamishna Mkuu wa Magereza, Mkuu wa Magereza Dsm, Mkuu wa Gereza Keko, Afisa wa zamu wa wiki, Afisa wa zamu wa siku hiyo na askari walinzi wote waliokuwa zamu. Utaratibu huu wa uwajibikaji ukifanyika, naamini nidhamu itarudi serikalini..!