Rais amepotoshwa, si kweli kuwa mkoa wa Dar unachangia 80% ya pato la taifa. Kwa sababu;

Mikael Aweda

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2010
Posts
2,973
Reaction score
3,904
Wakati akijenga hoja ya kuteta usafirishaji wa gesi kuja Dsm, Rais alisema kwamba mkoa wa Dar unachangia 80% ya pato la Taifa. kwa hiyo, alimaanisha kwamba kama kila mkoa utang'ang'ania rasimali zake Dar ndo itafaidika kuliko mikoa yote. Kwa maoni yangu Rais amepotoshwa na washauri wake. Kwa sababu zifuatazo;

Walipa kodi wengi wa nchi hii wana makao makuu yao Dar lakini shughuli za uzalishaji wao na watumiaji wa bidhaa zao wako nchi nzima. Nitatoa mifano michache.

1) Bakhresa (Bilionea no 1mwenye kampuni zaidi ya 300) analipa kodi hapa Dar kutokana na biashara zake za mikate, mafuta ya kupikia, ice cream nk. Lakini ngano na alizeti iliyotumika kuzalisha bidhaa hiyo haijazalishwa hapa Dar, imetoka mikoani. Pili, watumiaji wa bidhaa hiyo siyo wa Dar tu, ni nchi nzima. Ila kodi analipia hapa Dar.

Mengi anapolipa kodi kwa biashara ya maji, coca cola analipia TRA Dar, ilipo makao makuu ya IPP. Lakini maji yake yananywewa na watz kutoka mikoa yote. Na kiwanda cha maji si lazima iwe Dar.

Vituo vya Tv, Radio,magazeti nk wanalipa kodi hapa Dar, lakini walaji wa bidhaa yao ni nchi nzima. TV inaoneshwa nchi nzima, magazeti yanasomwa nchi nzima. Nimetoa mifano michache tu.(soma mchango wa great thinker mmojawapo in Blue)
By Ndachuwa
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro iko Arusha lakini kwa kuwa Big Tax payer faili liko DSM; Leopard Tours nayo ni Big Tax Payer faili liko DSM; Tanzania Breweries wana plant Arusha na Mwanza faili liko DSM, Tanga Cement Big Tax payer faili liko DSM, Twiga Cement big tax payer faili liko DSM, Mabenki yote mafaili yako DSM ukiacha Community banks. Hili litarekebshwa na sheria ya majimbo 2016
Kwa hiyo, hoja hii ya Mkapa ( miaka ya nyuma) na Kikwete majuzi kuwa Dsm inachangia 80% ya pato la Taifa ni upotoshaji wa wazi ama ni uvivu wa kufikiri wa wasaidizi wao wanaohusika.

Nawasilisha.
 
JK Kwani huwa anatumia akili/mas...buri kufikiri?washaur wake ndo kina ritz
 
Ukiwa ndani ya chungu atafikilia ya chungu hicho tuu. Mawazo yao yote dar tu nakuongezea wafanyakazi wanaolipa kodi kila mwezi wapo dar tu au idadi kubwa ya wafanyakazi wapo dar. Hizi ni njia za kuhalarisha uonevu ili wa mikoa mingine wasidai haki zao. Si hoja ya nchi inayotaka kuendelea kama hivyo uingeleza ingekua London tu au marekani Newyork tu. mkuu wanatufanya wajinga
 

vipi jana ITV kwenye malumbano ya hoja hukusikika vizuri au????..... mana unajitaidi kwa kwenda itv tu
 
vipi jana ITV kwenye malumbano ya hoja hukusikika vizuri au????..... mana unajitaidi kwa kwenda itv tu

Mkuu,
Jana asbuhi nilikuwapo Tuongee Asubuhi, star tv saa moja na nusu na nitarudi tena. Kwa inakuuma kada wa ccm?
 
Nakupinga bakhresa hamiliki makampuni 300.

Si 300 ni zaidi ya 300. Ninakupa taarifa za uhakika. Siyo vizuri kutaja majina ya watu lakini ninafahamiana kwa karibu sana na watu wenye nafasi kubwa ktk makampuni ya Bakhresa.

 
kiukweli namshangaa sana Rais wetu anapopotosha jamii na kuongea bila kufanya Utafiti kwa wananchi wake.Mh. Kikwete amekuwa Rais wa kwanza Tz Kudanganywa kiurahisirahisi na washauri wake.
 

Wewe uliye na takwimu sahihi, tuambie Dar inachangia kwa asilimia ngapi katika pato la taifa.
 

hata samsung ni walipa kodi wazuri huko korea japo waraji wa bidhaa zao wako mpaka rufiji.
Sasa hapa sijui umewakilisha nini hasa.
 

Hujaitetea heading yako kabisa!
Dah, ulikaa chini ukafikiri na kuja na hoja hii kweli? Au umeamka na kuanza kuandika ndoto zako?
 
kiukweli namshangaa sana Rais wetu anapopotosha jamii na kuongea bila kufanya Utafiti kwa wananchi wake.Mh. Kikwete amekuwa Rais wa kwanza Tz Kudanganywa kiurahisirahisi na washauri wake.
 
Si 300 ni zaidi ya 300. Ninakupa taarifa za uhakika. Siyo vizuri kutaja majina ya watu lakini ninafahamiana kwa karibu sana na watu wenye nafasi kubwa ktk makampuni ya Bakhresa.


we jamaa unatunga maneno,sijui hata huko kwenye tv wanatumia vigezo gani kukualika.hebu tutajie japo makampuni hamsini ya huyo bakharesa ili tuone kama una hakika na unachokiongea.
 
Ingawa uchafu wa Mrisho unamfanya Benja aonekane msafi.... (ila sidhani kama argument waliyotoa hapa maana ilikuwa kwamba kila mkoa ukibaki na rasilimali zake Dar itafaidika zaidi) bali ni kwamba kule ndio inaitajika zaidi na ni more efficient

Kwahio hapo nadhani umepotosha mada ila binafsi naona suala hili tuangalia kwa long term effects na sio efficiency peke yake au wazalishaji wengi wapo wapi sababu long term ya kuzambaza ajira sehemu tofauti za nchi faida zake ni kubwa huko mbeleni sababu hata wasiochangia hata percent 10 nao ni watanzania
 
vyovyote ilivyo, lakini si jambo la msingi kukusanya nguvu za kiuchumi sehenu moja ya nchi, ni hatari sana. na nikipingamizi cha upanuzi wa maendeleo, hivyo kama hawa viongozi wanatumia akili waanze kuangalia jinsi ya kutawanya shughuli za kimaendeleo... nimekuwa nikifikilia Japan kuhusu sunam...kama japan wangekuwa na akili za kilofa kama hawa viongozi wetu ya kukusanya nguvu sehemu moja basi ingewezekana kuwa ndiyo anguko la Japan...pata picha leo kama sunami inatokea Dar wakati bomba la gesi limeisha leta gesi..., mambo yatakuwaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…